Ujumbe huo niiliona kama fulsa hivi kwasababu ulikua unaeleza kwamba kuna kampuni inaenda kuanzishwa na
kabla ya kuanzishwa Dar inatoa mafunzo kama miezi sita hivi na waliopata mafunzo ndio wataajriiwa. Kulikua kuna
namba zao pale kwenye ujumbe ili kupata maelezo zaidi.
Basi mimi nikachangamkia fulsa bila kulaza damu. Nikawaambia wazazi wangu ingawa walikua wabishi sana
kukubali lakini niliwaelewesha mpaka wakaelewa wakanipa pesa za kutosha kuishi Dar na za kulipia mafunzo
yatakayoendeshwa na kampuni maana ilikua sio bure. Nikafungua akaunti yangu ya binafsi ya benki kisha nikaweka
hizo hela. Baada ya hapo nikaenda Dar, Nikapanga chumba kimoja kwenye nyumba iliokua inavyumba vitatu
ambapo viwili vilikua pia vinawapangaji ambao walipanga kabla yangu. Siku ya kwaanza nilifika katika chumba
nilichopanga nikaweka mabeigi yangu humo nikalala. Siku ya pili nikanunua kitanda na vitu vingine vya muhimu
kwenya maisha ya kusoma ambayo naenda kuyaishi. Siku ya tatu ilikua ni jumatatu nikaanza kwenda kwenye
sehemu ya mafunzo ya hiyo kampuni. Nilikua naenda asubui narudi mchana mida ya saa 8 hivi.
Siku kama tano ivi zilipita bila kuwaona wapangaji wenzangu. Nilikua naona makufuli yamefungwa tu kila siku
lakini baada ya siku kadhaa nilipotoka kwenye mafunzo nilimkuta dada mmoja mweupe mzuri sana anafua nguo
karibu na mlango wa chumba kimoja kwenye hiyo nyumba niliopanga, kilicho tazamana na chumba chamgu. Alikua
amefunga khanga tu kifuani na amejiachia sana mpaka sehemu za juu ya usawa wa magoti zinaonekana. Nikajua
huwenda ni mke wa mpangaji wa chumba hicho maana chumba hicho kilikua kipo wazi muda huo. Nikamsalimia
“Habari Shemeji” akawa kama amesimama kufua hivi alafu akaniangalia vizuri usoni kwa macho yake mazuri alafu
akasema kwa sauti tamu sana “Maambo”. Mh basi me nikamjibu “Fresh tu” nikiwa nataka kufungua mlango kuingia
ndani akaniuliza “Ah wewe ndio umepanga chumba hicho?” nikamwambia “Ndio… wakati nahamia mwenye
nyumba aliniambia kunawapangaji wengine lakini nikawa nashangaa siwaoni”. Nilivyosema hivyo yule dada
akasema “Hahaha mimi nipo hapa nina mwezi sasa ila siku hizi chache nilikua nalala kwa rafiki yangu.
Nikamwambia “Anh na huyo mpangaji mwingine vipi?” akasema “Huyo kasafiri, nilimkuta anakaa hapa pekeake na
mimi nilikua mgeni kwake maaana mimi nina mwezi mmoja tu katika chumba hiki yeye nahisi ni mtu wa muda
kidogo hapa ila kwa sasa kasafiri”,. Nikamuuliza “Kwenye hicho chumba uko peke yako?” akatabasamu alafu
akajibu “Ndio, nipo pekeangu tu hapa hahaha”. Cheko na tabasamu lake tu vilikua kama vimeupasua moyo wangu
kwa furaha na kuamsha vihisia vya mapenzi juu yake.
Nilivyoona hivyo mimi nikasema “Anh sawa, we endelea kufua mimi niingie ndani” ili nikatishe maongezi kidogo
maana alishaanza kunichanganya kichwa na nilikua nimechoka muda huo. Yeye akasema “Sawa, mimi nipo…
ukinihitaji naitwa Salma” mimi hapo nikakumbuka sijamwambia hata jina langu, Nikamwambia jina langu alafu
nikafungua mlango kisha nikaingia ndani. Baada ya kuingia ndani nikatua daftari zangu pale ndani Huku kichwani
nikiwa nawaza “Huyu mwanamke anadawa nini? mbona mzuri alafu nilipokutana nae nimejiskia tofauti? yaani
nakutanane mara yakwanza na ananichanganya hivi… Au kisa sija mzoea? Mh itakua sijamzoea tu, Hana maajabu!
Alafu anaonekana kama mke wa mtu ila ananificha… hawezi ishi pekeake na uzuri huo”.
Sikua na ratiba ya kula muda huo maana huwa nikitoka kwenye mafunzo napitia kula kwanza kwa mama ntilie ndio
nakuja nyumbani. Tangu nifike hapo nilikua sipiki, nilikua nanunua chakula tu maana pesa nilikuanayo ya kutosha
na hata ingeisha nyumbani wangetuma tu. Vitu vikubwa nilivyokua nafanya nikiwa naishi hapo ni kunununua
chakula, kusoma mafunzo na kucheza magemu au kusikiliza muziki kwenye simu yangu.
Salma nae alikua ameongeza kitu katika maisha yangu ya pale maana ilikua kama nimepata rafiki wa kupiganae
stori mara moja moja nikiwa nyumbani. Mara nyigi nilikua nikikosa cha kufanya ndani natoka nje nikimkuta yeye
amekaa, anapika au anafanya kazi nyingine nje, tunapiga stori mpaka basi. Ila kiukweli Salma alikua ananivutia sana
maana alikua mzuri kupita maelezo. Alikua mweupe sana mwenye kifua kilicho simama vema na nzigo wa nyuma wa kutosha. Ukimuangalia usoni macho yeke ni makubwa alafu mazuri sana, tabasamu lake nlilikua linanimaliza na
akicheka ndio kabisa. Kuna muda nikiwa naongea na yeye akili yangu ilikua inahama najikuta namuangalia sehemu
kama kifuani au midooni mpaka najishtukia na yeyepia akiona hivyo alikua anaona viaibu kidogo.
Siku ya kwanza kuongea nae sana ilikua ni baada ya siku kama mbili hivi toka nikutane nae mara ya kwanza. Ilikua ni
mida ya jioni nimetoka kuangalia mpira, nimepitia kula chakula kwa mama ntilie ndipo nikaenda nyubani. Nilipofika
nyumbani nikamkuta amekaa mlangoni pake, mbele yake kuna jiko anapika chakula. Nilimsalimia akaitikia alafu
nikenda ndani nikachukua simu yangu ambayo kwa muda wote ambao sikuepo ilikua kwenye chaji. Baada ya
kuchukua simu nikaanza kucheza gemu nikiwa nipo ndani ya chumba changu lakini baada ya Dakika chache
wakakata umeme kukawa na giza mule ndani. Nikaamua kutoka nje nikakaa kwenye mlango tukawa tunaangaliana
na Salma akiwa amekaa mlangoni kwake na kwa muda huo alikua ameshikilia sahani mkononi anaanza kula.
Nikiwa nakaa pale mlangoni ili nianze kucheza gemu nikamsikia anasema “karibu tule” mimi nikajibu “Ah mimi
nimeshakula, asante”. Tukakaa kama dakika mbili hivi bila kuongea alafu nikasikia akijisemesha “Umeme nao
umetuachia giza bora warudishe mapema kabla simu yangu haijaisha chaji” mimi nikasema “Hahaha mimi simu
yangu inachaji yakutosha, wakate mpaka kesho tu” kusikia hivyo akacheka “Hahahahaha” alafu nikaongeza kusema
“Simu yangu hata nicheze gemu au kusikiliza muziki, kesho itafika ikiwa na chaji”. Nilipogusia muziki nikakuta
ananiambia “Enhe alafu kunanyimbo naomba unirushie kama unazo maana simu yangu mimi ni batani, siwezi pata
nyimbo mpaka niingiziwe”.

Nikamuliza “Unataka nyimbo gani?” akanitajia na kwakua hizo nyimbo nilikua nazo
nikamwambia “lete simu nikurushie”.
Akachukua simu akanyanyuka na kuja kunipa huku akiwa ameshikilia sahani ya chakula mkononi. Mimi
nikachukua simu yake na kuanza kurusha nyimbo huku yeye akiwa hajarudi mlangoni kwake, alikua amesimama
pale karibu yangu akisubiri simu yake maana jambo la kurusha nyimbo si jambo la kuchukua muda mwingi.
Nilipokua nikirusha nyimbo nikakutana na kitatizo kidogo ambacho kilinifanya nichukue muda kidogo kuliko
kawaida. Yeye alivyoona nachelewa, akaamua kukaa na mimi pale mlangoni pangu akawa anaendelea kula huku
ananiangalia ninachokifanya kwenye simu na kuendelea kuongea na mimi. Mh alikua amejisogeza karibu yangu na
tulikua tumegusana kabisa kiasi kwamba nilikua najikuta nahisi vitu tofauti na kitu ninachokifanya muda huo. Mwili
wake mlaini ulileta joto la ajabu mwilini mwangu alipokua karibu yangu maaana alikua ni mwanamke mwenye kila
sifa ya kuamsha hisia kwa mwanaume. Ukiachana na hayo yote, alikua ananukia vizuri.
INAENDELEA…
Zingatia hii: Tafadhali fahamu kuwa hadithi hii ni mali ya mwandishi. Hairuhusiwi kunakili hadithi yote bila idhini. Unaweza kushiriki au kuchukua sehemu ndogo ya hadithi, lakini si kuichukua hadithi kamili. Asante kwa kuheshimu kazi ya mwandishi!
One thought on “UTAMU WA JUMLA 03 (Simulizi ya Maandishi)”