Jinsi ya kupata Tiketi za Ndege za bei rahisi

Unapokua na mpango wa safari mbele yako, unaweza kuwa na uwanja mkubwa wa kuchangua ni usafiri gani utaoutumia kwenye hiyo safari. Lakini hiyo safari ikiwa ni ndefu, usafiri wa anga ndio unaweza kuwa ni chaguo sahihi kwako. Katika usafiri wa anga, kupanda ndege kutaokoa sana muda wako ambao ungeupoteza kwenye vyombo vingine vya usafiri kama vile Gari au Meli. Kwa mfano; Ukiwa na safari inayokuchukua masaa mengi au siku nzima kwenye gari, katika ndege safari hiyo inaweza kukuchukua Dakika au masaa machache sana.

Kwaiyo, pamoja na kwamba kusafiri kwa ndege huonekana kama ni gharama sana, Bado ni chaguo zuri kwasababu huokoa muda. Ndani ya dakika au saa unaweza kuwa umefika katika sehemu unayohitaji kuwa. Na hii ndio Sababu kubwa ya watu kutumia njia ya anga katika safari zao ukiondoa Sababu zao nyingine binafsi.


Sasa hapa chini kwenye ukurasa huu, tunaenda kufungua ubongo wako juu ya jinsi gani wanaweza pata ticket za ndege za bei rahisi ili usafiri bila kutumia Pesa nyingi.

Tunazungumzia hilo kwasababu watu hupata ticket za ndege kwa bei tofauti tofauti. Kuna watu hulipia pesa nyingi kupata au kubook Ticket na pia Kuna watu hupata ticket hizo kwa bei rahisi. Na ikiwa wewe unahitaji kupata Ticket za ndege kwa bei rahisi, tumia njia hizi chini.

Unaweza kubook ndege kwa App ya M-Pesa BONYEZA HAPA>>>

Njia ya kupata Tiketi za ndege za bei rahisi

Tafuta Tiketi Mapema

Ukihitaji Tiketi za ndege za bei rahisi, njia moja ya kuzipata ni kuwahi kuzitafuta. Yani tafuta Tiketi za ndege angalau hata mwezi 1 kabla ya safari yako. Mara nyingi Tiketi za ndege huwa zinakua bei rahisi kama siku ya kusafiri ipo mbali. Alafu tena bei huwa inapanda kadri siku ya kusafiri inapokaribia.

Kwaiyo kuwahi kuzitafuta tiketi kunaweza kukusaidia wewe kulipia pesa kidogo. Hii itakusaidia kuokoa pesa zako hasa kwenye zile safari zisizo za dharura.

Linganishia Bei za Ticket

Kama unasafari ya kwenda mahali flani, fahamu kuwa una uwanja mpana wa kuchagua ndege utayoitumia iwe ya shirika gani na hata ticket utaipata sehemu gani. Mashirika ya ndege yanaweza tofautiana bei na hata sehemu unazoweza pata Tiketi zinaweza tofautiana bei pia.


Kwaiyo ni vema ukawa na tabia ya kuangalia Tiketi unayohitaji inapatikana katika sehemu ngapi na tofauti ya bei Iko vipi. Alafu baadae uchague ambayo ni bei rahisi kwako na ulipie.

Kwasasa mtandaoni kuna tuvuti nyingi za kulinganisha bei za Ticket za ndege kwa wanao book ticket mtandaoni. Mfano mzuri ni hii iitwayo Skyscanner

Tumia Ofa au Punguzo

Kuzingatia Ofa au Punguzo kunaweza kukufanya upate ticket za ndege kwa bei rahisi pia. Punguzo la bei au Ofa zinaweza tokea kwenye mashirika ya ndege au tuvuti za ticket kwaajili ya kuvutia wateja wao.

Ukizingatia mambo kama hayo, unaweza kujikuta unaokoa pesa yako kwenye baadhi ya safari zako za ndege. Nasema hivyo kwasababu Ofa na Punguzo, mara nyingi hufanya ulipie pesa kiasi kidogo kuliko ambayo unapaswa kulipia kikawaida.

Safari siku au misimu isio na mambo mengi

Kama ulikua haujui, basi leo fahamu kuwa Bei za tiketi huwa juu wakati wa likizo, mwisho wa wiki, na kipindi cha msimu wa sikukuu. Kwaiyo ukihitaji kupata Tiketi za ndege zinazosafiri katika wakati huo, utalipia kiasi cha pesa kinachoweza kuwa cha juu kuliko kawaida.

Kusafiri siku za katikati ya wiki na vipindi vingine mbali na msimu wa sikukuu, kutakufanya upate ticket za ndege kwa bei rahisi. Hii ni kwasababu muda huo Tiketi huwa katika bei ya kawaida.

Natumaini mambo au njia hizi zitakusaidia katika kupata Tiketi bila kutumia Pesa nyingi. Kikubwa unatakiwa kuwa makini sana unapokata Tiketi ili kuepuka usumbufu unapotaka kukamilisha safari ulioipanga.

Leave a comment