Mahusiano mara nyingi huanza kwa msukumo wa hisia kali. Yani kila mmoja anajihisi kuwa na haja kubwa ya mwenzake. Kila jambo linaonekana kuwa jipya na lenye kuvutia, Wapenzi wote wanajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha wanampendeza au kumfurahisha mwingine. Lakini, kadri muda unavyoenda, hali hii inaweza kubadilika, na baadhi ya watu huanza kuhisi kama hakuna mapenzi ya dhati kama awali.
Hii ni hali inawakumba watu wengi, hata walio kwenye ndoa za muda mrefu. Kuna wakati mtu anajikuta anaendelea kutoa upendo, lakini mwenzake haonyeshi kujali au kuonyesha hisia zozote za kurudisha upendo huo. Hali kama hii inaweza kumkatisha tamaa, kuleta Mawazo na kumfanya mtu ahisi vibaya, hasa pale anapokuwa amejitolea sana kwa ajili ya uhusiano hayo.
Katika Hali hii, kabla ya kuchukua hatua yoyote, ni muhimu kujua kwamba yapo mambo ambayo unaweza kufanya ili kuboresha hali hii na kufufua tena mapenzi kwenye uhusiano wenu. Katika makala hii, tutazungumzia mambo unayoweza kufanya ili kurekebisha hali hii ikiwa imekutokea ghafla kwenye mahusiano yako.
Ujumbe wa Mapenzi kwa umpendae BONYEZA HAPA>>>
Mambo ya kufanya kwa Mpenzi asieonesha kukupenda katika Mahusiano
Kuwa mpya au tofauti kwake
Kuna wakati mpenzi wako anaweza kuwa ameacha kukuzingatia kwasababu amekuzoea. Yani anaweza kuwa anaona vitu unavyofanya kwake au ukiwa nae ni vitu ambayo vinajitudia mpaka anakuona hauna cha kushangaza. Hapa nazungumzia vitu kama, jinsi unavyoongea nae, muda unaangeanae, zawadi zako, sehemu mnazoenda, ahadi unazoahidi na mambo mengine kama hayo.
Ikiwa tatizo ni ili, basi utatakiwa kuwa mtu mpya kidogo kwake. Yapindue mambo ambayo unamfanyia au mnafanya kwa pamoja. Na usiyapindue kwa ubaya, fanya baadhi ya mambo mzuri kwa kumjali lakini iwe ni tofauti na alivyozoea. Kufanya hivyo kwa mpenzi asieonesha kukupenda katika Mahusiano kunaweza mfanya aanze kukuzingatia kwa upendo.
Tafuta tatizo upande wako na wake
Kama kutokukuzingatia kwake kunaonekana kuwa ni jambo zaidi ya kukuzoea, basi jaribu kutafuta sababu ya hali hiyo. Kwanza kabisa jaribu kufikilia kama wewe ndie tatizo maana kuna mambo unaweza kuwa umemfanyia ndio maana hakuzingatii. Fanya kufikilia vitu alivyowahi kukuonya au ambayo unajua kabisa viko upande wako lakini yeye humchukiza. Ukipata tatizo upande wako, fanya kuliweka sawa.
Ukikuta upande wako hakuna sababu yoyote ya yeye kuwa hivyo, fanya kuhamia upande wake sasa. Jaribu kufikilia na kudadisi ni kitu gani kimembadilisha hivyo. Tafuta sababu ili ujue uitaweka vipi hali vizuri.
Ukifanikiwa kupata tatizo linalomfanya mpenzi wako asikuoneshe kukupenda, jaribu kuliweka sawa ikiwezekana hata kwa kumshirikisha.
Kaeni muongelee hilo tatizo kwa pamoja
Njia rahisi ya kumaliza matatizo ni hii maana inafanya wote mufunguke yanayofanya musiwe sawa na kujadili mfanye nini ili hali iwe sawa. Fanya kukaa na mpenzi wako muongelee tatizo ambalo unaliona kwenye mahusiano yenu. Hakikisha unamtafuta mida mizuri ya kuongelea mambo haya ili aweze kufungua yaliomo moyoni kwake.
Usipokaanae muda sahihi, anaweza kukuficha yaliopo moyoni mwake. Kama ni mume au mke wako, unaweza ongea nae muda wa kulala au mkiwa metulia baada ya kucheza michezo yenu. Kama ni wapenzi tu, unaweza tafuta muda wenu mzuri wenye utulivu kama mida hiyo nilioiieleza. Usitumie simu kuongea, kutaneni ana kwa ana muongee ndio mtaweza elewana vizuri.
Mwisho; Ningependa kukukumbusha kuwa usisahau thamani yako. Kuna mambo mengi ya kuvunja moyo katika Mahusiano yanaweza kukuvunja moyo ila usisahau kuwa kuitambua thamani ni muhumu. Ikiwa unaona dalili za kuwa mpenzi wako hataki tena mahusiano na wewe, ni sawa kuheshimu maamuzi yake. Unaweza muacha alafu ukamtafuta mtu mwingine anaeijua thamani yako.