UTAMU WA JUMLA 02 (Simulizi ya Maandishi)


Wakati nakusanya nguo ghafla mlango ukagongwa “Ngo ngo ngo” na sauti ya Jimmy akisema “Oi wewe”.
Niligundua ni Jimmy nikasema “Oya… Umerudi sasa haha” akawa anasukuma malango huku anasema “Ahaha
nimekuja na shemeji yako huyu” huku akimruhusu mtu aingie. Mimi nikatupa macho kuangalia mtu anaeingia ni
nani, nikakuta ni Zuwena amevaa nguo nyeusi fupi alafu inaangaza kiasi ambacho baadhi ya sehemu zake za mwili
zinaonekana na Jimmy alikua anamshika kiuno alipokua akiingia ndani. Nilipomuona Moyo wangu ulidunda kwa
mshtuko “Nduh” na nikahisi kama kuishuwiwa nguvu hivi…
Nikaona bora nijikaze tu ila nisiwe na maneno mengi hapo maana nawezajikuta nimesema kitu kibaya. Nakumbuka
nilimsalimia Zuu kama ndio mara ya kwanza nakutana nae hapo. Na yeye alikua ananisalimia kama sijawahi ongea
nae kwa ukaribu. Baada ya kuwasalimia nikatoka nje na nguo nilizokusanya ili kuzifua na kuwaacha mule ndani.
Nilivyotoka tu, Jimmy aliufunga mlango ili mtu yoyote asiingie mule ndani na mimi sikua na hofu juu ya hilo
maana vitu vyote ambavyo vilikua vinahitajika ili nifue vilikua vinapatikana nje.
Nilichukua ndoo nikachota maji, nikavuta kiti pembeni ya chumba nilichukua nakaa alafu nikaanza kufua. Kichwa
changu muda huo kilikua hakipo sawa kabisa maana nilikua naona rafiki yangu Jimmy anaenda kula tunda la mtu
ninaempenda na kwakua sikumwambia basi nikaona acha niendelee kuumia moyoni tu kimya kimya huku nikifua
japo bado kichwani nilikua najiuliza “Amempataje huyu kiiumbe? Mbona sijawahi waona wakiwa karibu? Dah yani
Zuu nae inaonekana hanikubali kabisa maana aliponiona hata hakushtuka.ila namtamani sana huyu mwanamke”.
Wakati naendelea kufua ghafla nikaanza kusikia visauti toka ndani kupitia kidilisha kilichokua karibu na nilipokua
nafua. Mara ya kwanza nilikua nimevipuuza visauti hivyo nikawa nahisi ni Jimmy na Zuu wanaongea kawaida
kimahaba lakini baadae nikaanza kusikia sauti inaongezeka na inakua kama Zuu anabishana na Jimmy mule ndani.
Hali hiyo ilinifanya niache kufua nisogee zaidi kwenye dilisha nijue wanabishana nini humo ndani badala ya kuanza
mambo yao. Nilipotega sikio nikasikia Zuu akiwa na sauti kama amechukia hivi akisema “Usiniguse kwanza, Mimi
nataka uniambie ukweli kwanza… umesema hapa ni kwa nani?” Jimmy akawa anajibu “Kama nilivyokwambia
Zuwena, kwa rafiki yangu hapa… Kwanini unakua mgumu kunielewa” Zuu akajibu “We endelea kunidanganya tu, si
umeniona mimi mtoto mdogo? hiyo michezo naijua, usiniguse”. Nilimsikia Jimmy akisema “Tatizo huniamini…
Kama nilivyokwambia, mimi nakaa kule ila funguo kuna mtu ameondoka nayo ndio maana nimekuja kwa rafiki
yangu huku. Hata kodi ya hapa huwa nalipa mimi, huyo jamaa alietoka hapo nje huwa ni kama namsaidia tu maana
hayupo vizuri kipesa. Alafu nilishakwambia habari ya huyo jamaa hapo… Sasa kinachokufanya ubadilike sijui ni kitu
gani”. Nikakuta Zuu anamuuliza Jimmy “Yani umeniona mimi mjinga sana bora hata ungekua mkweli tu… Mimi
naona humu ndani kuna nguo zako ninazo zijua na hata viatu alafu bado unasema hapa sio pako. Sawa, kwasasa
naomba uniache niondoke maana nimekuchoka”. Mimi hadi hapo nikaanza kupata picha kidogo ya kinachoendelea
humondani. Kwa maongezi yale nilio yasikia nikajua tu huenda Jimmy hadi amemfikisha hapo huyo mwanamke ni
baada ya kumdanganya sana na muda huo uongo wake uligundulika na jambo hilo lilpelekea mpaka huyo
mwanamke kutaka kutoka humo ndani.
Basi nikatoka pale dilishani nikarudi nilipokua nafua ili kama wanatoka wasijenikuta pale na kugundua nilikua
nawasikiliza. Baada ya dakika kama tano hivi nikasikia mlango unafunguliwa, wakatoka kama wapo vizuri tu japo
Zuu alikua na sura inayoonesha amekasirika na Jimmy alikua ni kama anaaibu kiasi kutokana na kilicho mtokea.
Nakumbuka waliniaga pale alafu wakawa wanaondoka na kuniacha nikwa nafua. Kiukweli siku walivyokua
wanaondoka waliniacha nikiwa na furaha sana moyoni kwangu kutokana na kutofanikiwa kufanya mambo yao
humo ndani. Nilikua napenda sana Jimmy afanikiwe kwenye mipango yake kwasababu ni rafiki yangu lakini kwenye
Suala la kumkamata Zuu, sikulipenda maana mimi pia nilikua nampenda sana Zuu japo sikumwambia.
Nilipokua nikiendelea kufua na kufurahia tukio lililotokea, gafla nikaanza kufikilia tena yale maneno nilioyasikia
dilishani na kuanza kuwaza “Inamana Jimmy amemwambia Zuu mambo mengi kuhusu mimi alafu mimi sijui… Dah
na najua hawezi kuongea ukweli au jambo la kunisifu, lazima alikua ananiponda ili aonekane ni mtu wa juu”. Na kweli baada ya tukio hilo chuoni kulikua na watu wengi wajua juu ya Jimmy na Zuu. Zuu alimchafua sana jimmy
hapo chuoni kwa kuwaambia watu vitu alivyokua anaambiwa na Jimmy. Kulikua na maneno mengi ya Jimmy
kujigamba kwa Zuu ambayo yalienea kwa watu pale chuoni ila moja ya vitu nilivyosikia mwenyewe Jimmy
alimwambia Zuu ni kwamba ananilipia kodi tu lakini hakai na mimi. Jambo hili liliniumiza sana maana nilihisi
huenda ndio chanzo cha Zuwena kunipuuza nilipokua namtafuta. Lakini kwakua Jimmy alikua ni rafiki yangu,
nilipuuzia na tukaendelea kuwa pamoja hapo chuo.
Pamoja na yote yaliotokea, sikuwahi mtafuta tena Zuu. Nilikua nimetulia na mpenzi wangu sara na alikua anasema
ananipenda kweli. Niliweka moyo wangu wote hapo huku nikiwa na soma sana lakini nilivyozama sana katika penzi
lake, nikakuta Sara anaanza kunibadilikia tena. Ghafla tu alianza tabia ya kutonitafuta mpaka nimtafute na hata
nikimtafuta anaweza sema atanitafuta lakini hafanyi hivyo. Hali hii iliniumiza sana maana nilikua najua kwamba ni
dalili ya kuwa Sara amepata mwanaume mwingine. Nilichanganyikiwa sana kipindi hicho mpaka masomo nilikua
naona hayaeleweki. Hakuniambia kwamba tuachane ila tabia yake ilionesha kuwa tayari ameishaniacha ila ni mmi
tu ndio sijui. Nilifuatilia nikakuta kumbe kapata Mwanaume mfanyakazi na anamiliki mpaka gari. Niliwahi shuhudia
kwa macho yangu Sara akiingia kwenye gari baada ya kutoka chuoni. Niliumia sana na nikaamua kukubaliana na
uhalisia kuwa nimeachwa ila moyoni nikajisemea “Siku nikipata ajira na kuwa na hela nitawakamata sana
wanawake… yani nitawala sana. Ntanunua gari na ntakuwa na wanawake kila kona… Siwezi mpa moyo wangu
mwanamke auchezee kama hivi, ntakuwa nao wengi ili niwachezee wao… Pesa nyingine nitakua natumia na
marafiki tu maana ni bora marafiki kuliko kuwa na mpenzi”.



Basi siku zilisonga hapo chuo mpaka tukamaliza na kurudi nyumbani Tabora. Nakumbuka mimi na Jimmy tulirudi
nyumbani na tulikua tunaishi kwa wazazi wetu. Kwetu na kwakina Jimmy ni karibu sana. Kwao ni nyumba ya tatu
kutoka kwetu. Tulivyokua wadogo hatukua pamoja, familia yake ilihamia hapo kipindi nipo sekondari na yeye
alikua sekondari na tulipokutana tukawa marafiki mpaka tulipoenda chuo pamoja na kurudi pamoja. Tulivyorudi
tulikua mabishoo sana na tunapendeza juu mpaka chini kila muda na masimu yetu makubwa ya kupalasa.
Baada ya miezi kadhaa ishu ya chuo tukawa tumeimaliza kabisa tukawa tunamawazo ya kupata Ajira kichwani
mwetu kutokana na vyeti tulivyopata. Lakini tulianza kuona kama neno “ajira” linaongelewa kwenye ma TV alafu
hatuzioni mtaani na hata wakiziongelea kwenye TV mara nyingi wanasema “changamoto ya upungufu wa ajira”.
Jambo hili lilinifanya nijiulize “Inamaana pamoja nakuwa na vyeti Ajira naweza kupata au nisipate? Duh!”. Siku moja
nikakuta tu ghafla jamaa yangu Jimmy kasafili. Na hakuniambia kwamba anasafiri mpaka nilipomcheki kwenye simu
“Wewe uko wapi mwanangu, mbona haujaonekana leo” ndio akaniambia amerudi Dar. Mimi nikamuliza “Mbona
hukuniambia rafiki yangu?” akasema “Hahaha ilikua ni ghafla mzee, Nitakucheki tutaongea vizuri”. Mh Mimi
nikajua atanicheki kweli lakini haikua hivyo, siku zilizidi kusongea tu hanicheki na hata nikimcheki ananiambia
“ntakucheki”. Baadae nikakata tamaa kabisa ya kumtafuta maana nilikua najua nimuongo hivyo ukimsikiliza
unapoteza muda nikakata mawasiliano nae. Kiukweli baada ya Jimmy kuniacha kule Tabora nilianza kuwa na
mtizamo tofauti kidogo juu ya Marafiki, nilikua kama nimegundua kuwa marafiki hawajashikana na maisha yangu,
wanaweza ondoka muda wowote.
Nikaendelea kukaa pale nyumbani bila mafanikio ya kupata ajira na wazazi nilikua naona hawaniwazi tena kwenye
mambo ya pesa, wao walikua wapo tayari walipie mamilioni sehemu nisome au nipate kazi kuliko kunipa mimi pesa
ya hivi hivi tu. Kadri siku zilivyo zidi kusonga nilianza kuchakaa kimuonekano kutokana na kukosa hela. Wakati
nakuja kutoka chuo nilikua napendeza kiasi kwamba nikikutana na mtu ananiuliza “Hiyo sendo uliovaa mguuni
shingapi?” nikimwambia bei anasifia “Dah nzuri sana hiyo sendo!” lakini mambo yalibadilika kiasi kwamba
nakutana na mtu ananiangalia juu mpaka chini alafu anauliza “Hiyo gundi ni supagruu?” namuuliza “Wapi? hapa
kwenye sendo?” Anajibu ” ndio, hapo mguuni” namwambia “Ndio ni yenyewe” ananijibu “Gundi nzuri sana
hiyo!”. Kiukweli nilichakaa sana na hali hiyo ilinifanya niwe na kiu ya kufanya chochote nipate ajira na ilikua kama
bahati hivi nilikutana na tangazo ambalo liliingia kwenye simu yangu kama ujumbe. Ujumbe huo niiliona kama fulsa
hivi kwasababu ulikua unaeleza kwamba kuna kampuni inaenda kuanzishwa na kabla ya kuanzishwa Dar inatoa
mafunzo kama miezi sita hivi na waliopata mafunzo ndio wataajiriwa. Kulikua kuna namba zao pale kwenye ujumbe
ili kupata maelezo zaidi…

INAENDELEA….

Hii ni simulizi ya UTAMU WA JUMLA ilio katika maandishi. Ina uhusiano kidogo na Simulizi ya SUKARI YA DADA na MZIGO WA WAKUBWA. Inapatikana katika Sauti pia. Inavipande 11.

KUMBUKA: Hairuhusiwi kusomwa na mtu mwenye umri chini ya miaka 18.

Ukihitaji simulizi zote 3, Njoo WhatsApp

Leave a comment