Ikiwa unapambana kupata pesa na unapata lakini hauioni, hii makala ni ya kwako.
Kwanza unatakiwa kujua kuwa watu wengi wapo kwenye hali hiyo kwa sasa. Yani unaweza kuwa na pesa ndogo au nyingi zinazoingia lakini zinapita mkononi mwako tu na hazituli.
Pamoja na kwamba watu husema “Pesa sio Kila kitu” lakini unatakiwa kuelewa kuwa maisha ya sasa yanahitaji pesa. Hii ni kwasababu asilimia kubwa ya vitu vilivyopo kwenye maisha yetu, vinatumia pesa na vinadai pesa kabisa Yani.
Mfano; ukiwa umepanga nyumba unayolipa elufu 50 kwa mwezi inamaana katika Maisha yako Kila baada ya siku 30 unalipia elufu 50. Sasa hapo Ukijumlasha na mambo ya chakula, umeme na mambo mengine yanayojitokeza kwenye mwezi unaweza jikuta Kila mwezi unatakiwa kwenye mikono yako utoe pesa nyingi sana. Na hizo pesa zote unazotumia kwa ujumla wanaita “Gharama za maisha”. Hii inamaana maisha yana “Gharama”.
Mbinu za kutimiza malengo yako ya Mwaka BONYEZA HAPA>>>
Gharama za maisha na kiasi cha pesa unachoingiza
Gharama za maisha yako zikiwa ni kubwa kuliko kiasi cha pesa unachoingiza, unawezakuwa ni mtu unaeshika pesa lakini huzioni na unaangukia kwenye madeni. Yani unakua ni mtu unaetumia pesa nyingi kuliko unazoingiza.
Kujitoa kwenye hali hiyo unatakiwa kwanza kumuomba mungu akusaidie badala ya kukimbilia kwenye vitu kama pombe ili kumpunguza Mawazo.
Hatua ya pili, unatakiwa kutulia na kuiweka akili yako kwenye matumizi yako ili kuelewa kiasi gani unatumia kwa siku, mwezi na hata mwaka. Hapa utatakiwa kujua pesa kiasi gani unatakiwa kuwa nayo kwa mwezi ili uwe na mahitaji muhumu yote(Kodi, chakula n.k). Na pia unatakiwa kujua pesa kiasi gani huwa zinatoka mikononi mwako na kwenda kwenye vitu visivyo vya muhimu. Kiufupi unatakiwa kuzingatia pesa zinatokaje mikononi mwako.
Baada kujua pesa zinatokaje mikononi mwako, utatakiwa kuanza kuzizuia baadhi ya pesa zinazokwenda kwenye mambo yasio ya muhimu. Ni ngumu sana maana pesa nyingine unaweza gundua zinatoka mikononi mwako ili kuifurahisha Roho na imekua ni kama Tabia tayari kufanya hivyo. Lakini pambana sana kuzuia kwa kubadilisha tabia na kuepuka utoaji wa pesa usio wa muhimu sana.
Wakati ukiendelea kupambana kuzuia pesa zisitoke mikononi mwako kizembe, unaweza kuwa na hasira sana kuhusu pesa maana utakua unaona baadhi ya pesa zinaendelea kutoka mikononi mwako bila umuhimu na unashindwa kuzizuia. Lakini usikate tamaa maana jambo hili litakukumbusha kujiuliza “Nitarudisha vipi pesa zilizotoka mikononi mwangu bila umuhimu?”, Pia utajiuliza “Nifanye nini ili hizi pesa zinazokuja zisiwe zinatoka mikononi mwangu?”.
Unarudisha vipi pesa zilizotoka mikononi mwako?
Ni ngumu kurudisha pesa zinazotoka mikononi mwako ila unaweza anza kuzingatia utengenezaji wa pesa nyingi nyingine zitakazokuja mikononi. Yani hapa naongelea kuongeza kipato chako.
Mfano: kama ni mfanya biashara, basi unatakiwa kufanya bashara yako ikuingizie pesa nyingi zaidi. Na njia rahisi ya kufungua ubongo wako kwenye upande wakuongeza kipato ni kujifunza toka kwenye vitabu au watu wengine wanaoingiza pesa zaidi. Au unaweza anza kujaribu vitu mbalimbali ili kuitanua biashara yako iweze kuingizia pesa zaidi.
Kiufupi ni unatakiwa kutafuta njia za kuongeza kipato au pesa zinazokuja mikononi mwako huku ukiendelea kuzuia matumizi yasio na maana. Na ukifanikiwa kuingiza pesa nyingi kuliko unazotumia, utakua ni kama umefanikiwa kuzirudisha pesa zinazotoka mikononi mwako huku ukipata na nyingine za juu kwaajili ya mambo mengine.
Nini cha kufanya ili pesa zisiwe zinatoka mikononi mwako?
Kufanikisha hilo unatakiwa uwe unaweka pesa yako kwenye sehemu isiopungua thamani yake au uwe unaiweka pesa yako kwenye sehemu inayofanya pesa yako izalishe pesa nyingine.
Kiufupi ni utanatakiwa uwe unatuza pesa yako kwa kuweka kwenye akaunti au michezo ya kutuziana pesa. Wengine huwa wananunua mpaka viwanja ili kuitunza pesa tu isishuke thamani. Na pia unaweza iweka pesa yako kwenye biashara inayozalisha pesa zaidi ya ulioiweka.
Katika safari ya kuelekea mafanikio. Usisahau kuwa mungu atakusaidia ukijituma, na pia karamu na daftari ni muhumu kuvitumia kwenye mahebu yako ya kimaisha.
Mbali na hayo; kujiweka katikati ya watu wanapenda mafanikio ni muhimu. Hakikisha unakua na watu wanaopenda mafanikio kwenye maisha na sio waliokata tamaa. Ukishindwa kabisa kupata watu, wafuate wanao hamasisha kujituma na mafanikio kwenye maisha waliopo mtandaoni. Kama wewe ni kijana wa kiume unapenda kutiwa hasira sana za kutoka ulipo, unaweza wafuata hata wakina Chiefgodlove au Chimakeke. Pamoja na mabaya yao, hiyo ni moja ya kazi yao.
Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy!