Kila mtu anatamani kuwa na mpenzi mwaminifu na anayejali, kwani uaminifu ndio msingi wa mahusiano yenye furaha na utulivu. Si mwanaume wala mwanamke, wote wanapenda huwa na mahusiano na mtu asiewasaliti. Hisia za upendo na kuaminiana, hujenga mahusiano imara ambayo hutoa faraja na usalama wa moyo kwa wapenzi wote wawili. Hakuna anayependa kuwa na mashaka au wasiwasi kuhusu tabia za mwenzi wake, hasa linapokuja suala la kuwa na mpenzi mwingine. Hii ndio maana mwanzo wa mahusiano wapenzi husisitiza sana kutosalitiana kwa kuambiana maneno kama “Nitakupenda milele… Sina mwingine zaidi yako… Siwezi kukusaliti”.
Lakini wakati mwingine, hali ya kusalitiwa hujitokeza, na hii inaweza kuwa ngumu sana kwa aliesalitiwa kukubaliana nayo. Watu wengi hujawa na maumivu makubwa wanapogundua kwamba wamechezewa au kudanganywa na mtu alieshika furaha ya moyo wao. Hupata hisia zinazovunja moyo na kuumiza, na mara nyingi hisia hizi humfanya mtu kujiuliza kama anapaswa kuendelea na uhusiano huo au kuachana nao kabisa.
Uamuzi wa kumwacha mpenzi kwa sababu ya usaliti ni jambo zito maana ni kuharibu kabisa uhusiano uliokuwepo bila kujali mmetoka wapi. Ni muhimu kufikiria kwa makini kabla ya kuchukua hatua yoyote ili kuhakikisha kuwa unafanya uamuzi sahihi maana sio kila kusalitiwa kunatakiwa kuwa mwisho wa Mahusiano. Katika makala hii, tutaangazia mambo ya kujiuliza au kufikiria kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho.
Jinsi ya kujua kama mpenzi ulienae anakupotezea Muda tu BONYEZA HAPA>>>
Mambo ya kufikiria kabla ya kumuacha mpenzi kwa kukusaliti
Ni kweli?
Kuna mambo au matukio yanaweza kukufanya uamini kuwa mpenzi wako anakusaliti au amekusaliti lakini ikawa sio kweli. Ni ngumu kuamini kuwa mpenzi wako hajakusaliti wakati umeyaona mazingira ya kukusaliti. Watu wengine huwa Wanaamini kuwa wamesalitiwa hata kwa kuambiwa tu au kusikia maneno ya watu. Unachotakiwa kujua ni kwamba kuna wakati inaweza kuwa sio kweli.
Ni vema kabla ya kufanya uamuzi wa kumuacha kipenzi cha Roho yako, ukathibitisha ni kweli amekusaliti au hajakusaliti. Usije muacha mpenzi wako sahihi kwa vitu vya kuhisi au kusikia. Ukiona mambo yanakuchanganya, unaweza kukaa nae mukaongea kuhusu unachohisi au ulioyasikia kisha ukaangalia anayachukuliaje hayo mambo na yeye.
Chazo ni wewe, yeye au mtu mwingine?
Wengi likitokea jambo la kusalitiwa huwa tunaona mbaya ni aliesaliti lakini kuna wakati mtu mbaya unaweza kuwa ni wewe uliesalitiwa au akawa mtu mwingine tu mbali na nyie.
Ukiwa na uwezo au moyo mkubwa, unaweza jiuliza nini chanzo cha usaliti uliofanyiwa. Kuna watu wengi tu huwa wanasalitiana kwenye mahusiano lakini baadae wanagundua nini chanzo, wanarekebisha walipokosea alafu wanaendelea na mahusiano. Unaweza gundua kuwa wewe ndio umesababisha yeye kufanya hivyo au Kuna mtu mwingine ameamua kuwavuruga.
Jambo hili limejitokeza kwenye simulizi fupi iitwayo “SIRI NA SHEMEJI” na inaweza kuwa vizuri sana kama utafuatilia simulizi hii.
Bado anakupenda na anajutia kukusaliti?
Kuna watu wanasema “Usimwamini au kuendelea na mwanamke au mwanaume aliekusaliti”. Lakini kiukweli kwenye jamii zetu mambo ya kusalitiwa hutokea kwasababu mbalimbali na watu husameheana na kuendelea kujenga mahusiano yao kama hakuna kilichotokea.
Kabla ya kumuacha au kumsaheme mpenzi aliekusaliti ni vema ukajiuliza “Bado anakupenda?” na pia usisahau kujiuliza kuwa “Anajutia kukusaliti?”. Kama unaona kabisa mtu bado anakupenda sana na hataki kukupeteza kwenye maisha yake, kumsamehe unaweza kuwa uamuzi mzuri. Ila inabindi ujilidhishe kabisa ili usijejutia uamuzi wa kumsaheme.
Pia Jambo limejitokeza kwenye simu fupi iitwayo “SIRI NA SHEMEJI” na inaweza kuwa vizuri sana kama utafuatilia simu hii ili kuelewa zaidi.
Unaweza kusahau na kumpenda bila kujali?
Baada ya mpenzi wako kukusaliti, angalia moyo wako kama unaweza sahau yote na kuendelea kumpenda. Kama unaona kabisa hauwezi kumsamehe au kusahau alichofanya, ni vema ukamuacha tu maana ulionayo moyoni yanaweza pelekea kufanya jambo baya kwake kama kisasi.
Kwaiyo ni vema ukajipima kwanza kama unaweza sahau yote na kuendelea kupendana nae kama hakufanya kitu kibaya kwako. Yani kama umemsaheme, usije waza mabaya yake tena.
Hautakua wakwanza kufanya hivo, watu wengi hufanya kwa wapenzi wao, waume zao au mwake zao. Lakini ukiona hauwezi, jiweke mbali nae maana kuna siku moyo unaweza kukusukuma kumfanyia mabaya.
Ni hayo tu katika ukurasa huu wa The bestgalaxy, lakini kama ni mtu anaependa kuelewa zaidi, unaweza soma Simulizi ya “SIRI NA SHEMEJI” ili kuburudika huku ukiongeza uelewa kuhusu swala hili.