Jinsi ya kupata Visa au Mastercard kirahisi kwaajili ya malipo ya mtandaoni

Kufanya malipo mtandaoni ni moja ya mambo ambayo ni vema kila mtu anaetumia mitandao akafahamu. Hii ni kwasababu kwasasa kuna mambo mengi katika mtandao huwa yanahitaji mtu afanye malipo ili kuyapata. Malipo ya mtandaoni yanaturahisishia kufanya manunuzi ya bidhaa mtandaoni na hata kulipia huduma nyingine.

Njia za kulipia au kufanya malipo mtandaoni kwasasa zipo nyingi sana. Kuna njia nyingine huwa ni salama na njia nyingine sio salama. Lakini watu wengi wanahitaji njia salama na rahisi ya kufanya miamala hii, hasa wanapotaka kutumia njia za kimataifa za kufanya malipo mtandaoni. Hapa ndipo kadi za malipo za Visa na Mastercard zinapokuja kuwa msaada mkubwa kwa watumiaji wa mtandao.

Kadi za malipo Visa na Mastercard zinazoweza kutumika mtandaoni zina faida nyingi, ikiwemo usalama na urahisi wa kufanikisha miamala kutoka sehemu yoyote duniani. Hii ni muhimu sana kwa wale wanaopendelea kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma tovuti tofauti za kimataifa mtandaoni. Kwa kutumia kadi hizi, unapata fursa ya kulipia mambo mengi sana mtandaoni. Kati ya vitu unaweza fanyia ni kulipia huduma za movies kama Netflix, unaweza nunua bidhaa katika masoko ya mtandaoni kama AliExpress au kupitia matangazo katika Facebook.

Kwaiyo kuna umuhimu wa kuwa na kadi ya malipo mtandaoni. Lakini si kila mtu anajua jinsi ya kupata kadi hizi kirahisi. Mara nyingi, watu hukutana na changamoto katika mchakato wa kupata kadi. Katika makala hii, tutakuongoza hatua kwa hatua njia rahisi ya kupata kadi ya malipo inayoweza tumika mtandaoni. Kujua hili kutakusaidia pindi utakapokua kwenye uhitaji wa jambo flani linalohitaji ufanye malipo mtandaoni kwa Visa au Mastercard.

Usitafute mambo haya mtandaoni utaibiwa BONYEZA HAPA>>>

Njia ya kupata Visa au Mastercard kirahisi kwaajili ya mtandaoni

Unapohitaji Visa au Mastercard ya haraka kwaajili ya malipo ya mtandaoni, fahamu kuwa unaweza ipata ndani ya dakika chache tu hapo ulipo. Unaweza tengeneza Visa au Mastercard (virtual cards) kwenye huduma ya mtandao wako wa Voda,Tigo na Airtel. Mitandao hii inakupa nafasi ya kutengeneza kadi ya malipo ya mtandaoni ndani katika chache tu.


Ukihitaji kutengeneza kadi kirahisi kwenye mtandao wako wa Simu unaotumia, pakua app ya Tigo Pesa, My Airtel au Mpesa. Baada ya hapo utatakiwa kujisajili kwanza na hiyo app alafu nenda katika kipengele cha kadi. Katika kipengele hicho utaweza kutengeneza kadi yako na hata kuifuta pindi utakapo maliza matumizi. Unaweza tengeneza kadi za kutumia muda mfupi na mrefu pia.

Hiki ni kipengele cha kadi katika app ya Tigo Pesa



Ila nashauriwa kuifunga kadi yako pindi unapomaliza matumizi ili kulinda pesa zisije katwa bila na huduma zako mbali bila lidhaa yako au kuibiwa waalifu.

One thought on “Jinsi ya kupata Visa au Mastercard kirahisi kwaajili ya malipo ya mtandaoni”

Leave a comment