Tai au Eagle ni ndege maarufu kwa uwezo wake kwenye mambo mbalimbali na amekua akiongelewa sana. Baadhi ya watu hutumia ndege huyu kama alama za kuonesha ujasiri, nguvu na ubora. Lakini pia kunawatu humtumia ndege huyu kama mfano katika Maisha na mafanikio.
Kutumia mfano wa tai kama alama ya mafanikio ni njia bora ya kuelewa mambo muhimu yanayoweza kutusaidia kufikia sehemu flani maishani. Ili kufanikiwa, Kuna muda ni kweli tunahitaji kuiga tabia na sifa fulani za tai ambazo ni zenye thamani na zinazoweza kutupeleka mbali. Kati ya sifa hizo ni hizi hapa chini.
Jinsi ya kulinda ndoto zako zisife maishani BONYEZA HAPA>>>
Sifa za kumuiga Tai ili kufanikiwa kwenye maisha
Kuwa na Maono na Mtazamo wa Mbali
Tai ana uwezo wa kuona mbali sana, hadi kilomita 5! Hii inampa nafasi ya kuona mlo wake au adui akiwa mbali. Ili kufanikiwa, ni muhimu kuwa na maono ya mbali na kutazama mambo kwa upana. Jiulize: unataka kufikia nini maishani, na ni vikwazo gani vinaweza kujitokeza? Kama tai, kila mara angalia mbali zaidi ya hali ya sasa, na ujipange kulingana na unachokiona mbele.
Kuanza upya
Kuna wakati Tai hutenga muda kujibadilisha kwa kung’oa manyoya yake ili kufanya manyoya mengine mapya yaote. Hii ni muhimu kwetu pia; wakati mwingine ni lazima tuondoe tabia, mahusiano, au mawazo ambayo yanatuzuia kusonga mbele. Wakati mwingine, uamuzi wa kuacha kile kinachoturudisha nyuma, ndicho kinachoweza kutupeleka mbali zaidi. Hivyo tunapaswa kuishi kwa mfano huu katika mambo yetu ya kila siku.
Kukabiliana na Changamoto
Tai huwinda nyoka kwa kuruka chini na kuwashika kwa makucha yao, kisha kuruka juu huku nyoka akihangaika. Kisha tai wanaweza kuponda au kung’oa kichwa cha nyoka huyo na kukimeza kizima wakiwa bado wanaruka.
Tai huenda juu kwasababu ndio sehemu ambayo anaijua vizuri lakini nyoka hawezi kuhimiri. Tunawezasema Tai huwa anampeleka nyoka sehemu ambayo anaijua vizuri na ile inaruhusu yeye kushinda vita kirahisi.
Hii katika maisha inatukumbusha kuwa bora katika upande wetu na kutumia tulichonacho kuzishinda changamoto zinazokuja bila kuogopa. Tumia ulichonacho kuwa unapohitaji kuwa, au nenda katika sehemu inayoruhusu kupata unachohitaji. Na pia ondoka sehemu inayosababisha ushindwe.
Kwahivyo, ukitaka kufanikiwa, kuwa kama tai: mtazamaji wa mbali, mwenye moyo usiotetereka, na mwepesi wa kubadilika.
