Mambo ya kufanya Mpenzi akiwa hakupigii simu au kukutafuta

Simu imekuwa sehemu muhimu sana katika mahusiano ya siku hizi. Kupitia simu, wapenzi wanaweza kuwasiliana kwa urahisi, kubadilishana mawazo, na kueleza hisia zao bila kujali umbali uliopo kati yao. Kutopokea simu au kutokutafutwa na mpenzi wako kwa muda mrefu kunaweza kuleta wasiwasi, hasa katika mahusiano yenye mawasiliano ya mara kwa mara.

Kwa kuwa mazungumzo kupitia simu ni njia rahisi ya kutunza uhusiano, ni jambo la kawaida kwa mpenzi kujisikia vibaya au kutokuwa na amani mpenzi wake anapokaa muda mrefu bila kupiga simu. Kutozungumza kwa muda mrefu kunaweza fanya mtu kujihisi kutothaminiwa kwenye mahusiano yake ya mapenzi au kuhisi jambo jingine baya limeingia kwenye mahusiano.

“Kutokupigiwa simu na mpenzi” hali inayoweza kuwa na sababu nyingi na pia inaweza ikatokea kwa namna nyingi. Lakini badala ya kuwa na wasiwasi au kuchukia, kuna mambo kadhaa unaweza kufanya ili kuiweka sawa.
Ikiwa mpenzi wako hakupigii simu kwa namna yoyote na haujui nini Cha kufanya, hapa chini kuna jinsi tumeeleza mambo unayoweza kufanya.

Mambo ya kufanya mpenzi akiwa kakupigii simu au kukutafuta

Tengeneza tabia ya kumpigia sana wewe alafu ghafla uiache kwa muda

Unaweza kufanya Jambo hili kama mpenzi wako mpya anatabia ya kutokukupigia simu lakini ukimpigia, mnaongea vizuri tu na mahusiano yenu yametulia.
Utachotakiwa kufanya hapa ni kuzidisha kumjali na kumpigia simu za mara kwa mara alafu unaamua kutulia bila kumpigia ghafla. Jambo hili linaweza mfanya akupigie kujua ni nini tatizo maana sio kawaida yako.
Akikupigia kwa mara ya kwanza, inaweza kuwa ndio tabia yake ya kukupigia imeanzia hapo.

Maswali ya kumuuliza Mpenzi wako Mpya BONYEZA HAPA>>>

Kuwa na mambo mazuri ya kuongelea kwenye simu

Kuna watu muda huu, hawakupigii kwasababu hakuna jambo la kuongelea. Inaweza kuwa hivyo pia kwenye mahusiano. Mpenzi wako anaweza kuwa hakupigii simu mara kwa mara kwasababu mnakosa vitu vizuri vya kuongelea.
Kuna watu wengi tu huwa wanashindwa kuongea vizuri na wapenzi wao kwenye simu. Na baadhi ya wanaoongea, huwa hawaongei mambo mazuri ya kuvutia kiasi kwamba mpenzi awe anatamani kupiga simu na kuongea tena.

Kama unapitia jambo la kutopigiwa simu kwa namna hii, basi fanya kutengeneza uwezo wa kuongea na mpenzi wako kwenye simu mpaka awe anatamani kukupigia ili muongee.

Onana nae mzungumzie mahusiano yenu vizuri

Ikiwa hakupigii simu na hataki kuongea na wewe kwa namna yoyote ile kama mtu aliepandwa na hasira, basi hakikisha unamtafuta muonane ana kwa ana. Unaweza kumfuata mahari alipo na ukaongea nae kuhusu mahusiano yenu vizuri ili kujua nini tatizo. Kama utakua mbali nae, unaweza watumia ndungu au marafiki kumuuliza kuhusu tatizo linalomfanya asitake kuwasiliana na wewe.

La kumaliza ni kwamba, Kuna muda mtu anaweza kuwa hakupigii simu wala kupokea simu yako kwasababu ana matatizo yaliomkuta au yupo mazingira yasiomrusu. Hivyo uwe unafikilia upande huu pia kwa mwanamke au Mwanaume wako. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Leave a comment