Jinsi ya kupata Password ulioisahau (Ingia kwenye Akaunti yako)

Katika dunia ya sasa, usalama wa mtandaoni ni muhimu sana, watu wengi wanashauriwa kuwa na nywila (password) imara kwa kila akaunti wanayotumia. Nywila hizo zinalenga kuwalinda kutokana na hatari za udukuzi na wizi wa taarifa binafsi. Unaweza kulinda akaunti yako Facebook, TikTok na mitandao au tuvuti nyingine kwa password ngumu sana(Strong password) ili mtu mwingine asiingie. Hizi password au nywila ngumu mara nyingi zinakuwa na mchanganyiko wa herufi, namba, na alama maalum. Jambo hilo ni nzuri kwa ulinzi, lakini linawezafanya iwe rahisi sana kuzisahau..

Sote tumewahi kuwa kwenye hali ambayo tunajaribu kuingia kwenye akaunti fulani lakini tunakumbana na tatizo la kusahau password. Ni jambo linalokela sana, hasa pale unapokuwa na haraka ya kupata taarifa au huduma fulani mtandaoni kupitia akaunti yako . Nakuna muda, hata baada ya kujaribu mara kadhaa, hatukumbuki password sahihi ni ipi.

Bahati nzuri, kuna mbinu mbalimbali zinazoweza kukusaidia kupata nywila ulioisahau. Hizi mbinu ni rahisi na zinaweza kukusaidia kuingia tena kwenye akaunti zako endapo utapoteza password. Hapa chini ntunaenda kukueleza mbinu hizi.

Jinsi ya kutafuta Simu ilioibiwa BONYEZA HAPA>>>

Jinsi ya kupata Password ulioisahau (Ingia kwenye Akaunti yako)

Kipengele cha “Forgot Password?”



Katika ukurasa wa kuingilia kwenye Akaunti yako mara nyingi huwa wanaweka sehemu ilioandikwa “Forgot Password?”. Sehemu hii ni maalumu kwa kukusaidia ku-recover au kuirudisha akaunti ulioisahau password yake. Kwaiyo endapo utasahau password ya akaunti yako na ukaona sehemu ilioandikwa hivyo, basi gusa hapo kisha fuata maelezo utakayopewa ili kuingia kwenye akaunti yako tena.
Mara nyingi huwa wanakuomba uandike Email au Namba yako ili wathibitishe kuwa wewe ndie mmiliki wa akaunti unayotaka kuingia. Ukiwa na taalifa au vitu wanavyo hitaji, basi watakuruhusu uingie na kuweka password mpya ikiwezekana. Lakini usipokua na taalifa wanazo hitaji, itakua ni ngumu kukuruhusu uingie kwenye akaunti yako.

Kuorodhesha password zote za kichwani na kujaribu



Kama njia hiyo ya juu imeshindikana kwasababu flani, basi unaweza tumia njia hii. Chukua karatasi na kalamu kisha andika password zote unazohisi zinaweza kuwa sahihi. Andika ukiwa umetulia na usiache hata moja kichwani mwako. Baada ya kufanya hivyo, anza kujaribu taratibu moja baada ya nyingine.
Katika kujaribu, unaweza bahatika kuipata password yako sahihi kisha ukaingia kwenye akaunti yako.
Katika kuandika password, baadhi ya watu huwa wanapuuza herufi ndogo na kubwa za mwanzo wanapoandika password alafu wakiambiwa “password sio sahihi”, wanachanganyikiwa.
Sasa wewe, usikosee kwenye hili. Hakikisha unajaribu Password ikiwa herufi kubwa mwanzoni alafu ikigoma, afnza na herufi ndogo. Yaani mfano; Unaweza jaribu password kwa kuandika “Amina”,alafu ikigoma, andika “amina” na ujaribu tena.

Kipengele cha Akaunti manager



Kwasasa kwenye simu na vifaa kama PC huwa kunakua na kipengele cha “Password manager”. Kipengele hii huwa kinatuza password za akaunti mbalimbali ili kukusaidia kuingia kwenye Akaunti zako kwa haraka. Kipengele hiki kinaweza tumika kupata Password ulioisahau pia.

Kipengele hiki hakitunzi kila password bali kinatuza password ulizoruhusu kizitunze tu. Unaweza ingia kwenye upande wa “Password manager” kwenye kifaa chako ili kuhakikisha kama ipo au haipo.

Kwa simu za Android unaweza pata kipengele hiki katika “Settings”, upande wa Google kikiwa kimeandikwa “Password manager”.

Katika iPhone unaweza pata kipengele cha Password manager katika settings pia japo iPhone za hivi karibuni urahisi zaidi kwa kuweka app ya “Passwords” maalumu.



Ni hayo tu katika ukurasa huu wa The bestgalaxy, Endelea kuwa karibu nasi.

Leave a comment