Ujumbe wa Mapenzi kwa umpendae (Meseji)

Natumaini unafahamu kuwa kutuliza akili na kutuma ujumbe wa mapenzi kwa umpendaye inaweza kuonekana kama jambo la kitoto lakini ni muhimu sana kwenye mahusiano. Ujumbe wa maneno ya upendo unaweza kuwa na uzito mkubwa kuliko tunavyodhani. Na hii ndio maana mara nyingi The bestgalaxy tunakuandalia makala zinazohusu mambo yanayohusu ujumbe wa mapenzi.

Wanawake na wanaume, wote hufurahia sana wanapopokea ujumbe wa mapenzi, haijalishi wana umri gani. Hata watu wenye umri mkubwa wanapoona maneno machache ya upendo kutoka kwa watu au wapendwa wao, hufurahi na kuhisi kuthaminiwa.

Mtu unaweza mtumia umpendae Ujumbe wa aina hii hatakama tayari mupo kwenye ndoa. Kikubwa ujumbe huo uwe mzuri na umpate mke au mume wako kwenye wakati mzuri atakao furahia.

SMS za kumchekesha mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Katika ulimwengu wa sasa, ujumbe mfupi ndio mzuri kuliko Ujumbe mrefu sana. Ujumbe wa maneno machache ya upendo unatosha kufikisha hisia zako na kumfurahisha bila kuhitaji maneno mengi. Ni njia bora ya kuonyesha kuwa unamjali mtu bila kutumia muda mwingi. Lakini hii haina maana kuwa ujumbe mrefu hauna umuhimu, bado unaumuhimu mkubwa sana. Kama unapenda kumtumia mpenzi wako ujumbe au sms ndefu za upendo, basi isiwe kila muda au mara kwa mara.

Ujumbe wa mapenzi kwa umpendae

  • Nikikwambia “Nikinywa maji nakuona kwenye glasi” najua utanicheka na hautaniamini. Lakini hiyo sentensi huwa inaana “Nakuwaza kila wakati”. Na ni kweli na kuwaza kila wakati kwasababu nakupenda sana kipenzi.
  • Umenipa Raha ya ajabu. Umeniacha sina usemi kama bubu. Ladha sio Sukari, sio Asali na ni zaidi ya “Tamu”.
  • Yani muda huu nimetulia hapa, watu wanaweza sema nawaza hela. Kumbe nakuwaza wewe kipenzi cha Roho yangu. Vipi Hali yako we malaika?

  • Jinsi ninavyokupenda ni kama nilikuweka ndani ya moyo wangu alafu funguo za moyo nimepoteza. Siwezi ingiza tena mtu na huwezi toka bila maumivu mpenzi, UMENIWEZA!

  • Moyoni ni nakupenda, akilini naamini kuwa tunapendana. Mambo ni mengi sana ya kufanya tusiwe sawa. Ila unapo lala au kuamka, usisahau kuwa nakupenda sana.

  • Ukisema “Nakupenda” nahisi furaha sana moyoni. Ukiwa karibu, huwa staki uende mbali. Wewe ni kile chakula naweza shiba na nikaendelea kukitamani.


  • Wanasema “Mtu hauwezi kuiona raha ya Dunia bila kuwa na furaha”. Mimi nasema siwezi kuiona raha ya Dunia bila wewe. Kwasababu wewe ndie furaha yangu, nakupenda kuliko unavyo fikilia.

  • Nakushukuru kwa kila tabasamu, kila kumbatio, na kila neno zuri uliloniambia. Nakuona kama ni zawadi ambayo kila siku inanikumbusha thamani yangu. Nakupenda sana na naomba usije choka kunipenda.

  • Nahisi umenizamisha kwenye usingizi mzito sana. Najiona kama naota ndoto tamu na ndoto hii, ni kuwa na wewe kipenzi. Ikiwa kweli hii ni ndoto, basi iwe hivi milele maana nikiamshwa nitaumia.

  • Nikikwambia “Siwezi kuishi bila wewe” unaweza nicheka kwa kuhisi ni uongo. Lakini mimi nakwambia hivyo nikiwa na maana “Siwezi kuishi maisha ninayotaka bila wewe”. Mimi nataka niishi maisha ya kupendana na wewe milele. Sasa nitawezaje kuyaishi bila wewe?
  • Nikikukumbuka sana, moyo wangu hunipa masharti ya kutimiza ili nipate FURAHA. Sharti la kwanza ni kuwa karibu yako na ikishindikana, basi nikupigie simu nisikie sauti yako. Uwe unapokea simu sasa mpenzi, utaniua mwenzako.

  • Binadamu tumeumbiwa makosa mpenzi, huenda kunakitu nakosea maana mimi si malaika. Lakini kumbuka nina Moyo, mpenzi. Na huo moyo unamapenzi ya dhati na wewe.


  • Upendo wako ni amani katika Dunia iliojaa vurugu na kelele nyingi juu ya MAPENZI. Wakati watu wangine wanatafuta wapenzi wanaojua mapenzi, mimi nasherekea kukupata kipenzi changu.
  • Nakupenda sana mpenzi. Yani hata kama wewe ungekua ni Mti alafu mimi ni ndege nilietua kwenye Mti kwa bahati mbaya katika matembezi. Bado ninge hamia kwenye mti huo mazima maana unakila ninachotaka.

Ni jumbe hizo tu katika ukurasa huu ila kuna makala nyingi unaweza soma katika The bestgalaxy ili kupata sms au Jumbe nyingi zaidi za mapenzi. Endelea kuwa karibu na sisi na pia usisahau kufuatilia mambo mengine ikiwemo simulizi.

Leave a comment