Kuvamiwa kwa akaunti ya WhatsApp na jinsi ya kuirudisha katika usalama

Baadhi ya watu hutumia WhatsApp bila kujali usalama wa akaunti zao. Kujali usalama wa akaunti ya WhatsApp ni jambo muhimu sana maana kunaweka mambo yako katika hali ya usalama na vile vile unakua unawakinga watu unaowasiliana nao wasipate matatizo kupitia namba yako.

Akaunti ya WhatsApp inatakiwa kulindwa maana inaweza vamiwa na watu wabaya katika mitandao waitwao “hackers” au “Wadukuzi”.
Baada ya akaunti yako kuvamiwa na watu hawa, unaweza kuwa unaendelea kuitumia bila kujua au unaweza ipoteza ghafla kwa kushindwa kuingia kwenye akaunti hiyo. Kiufupi hii inategemeana na njia waliotumia kuivamia akaunti yako na kufanikiwa kuingia.

Kwaiyo moja ya dalili kubwa ya kuwa imevamiwa, ni kukuta akaunti yako inafanya mambo ambayo haufanyi. Mfano unaweza kuta sms zimetumwa kwa watu lakini binafsi wewe haukuzituma. Mbali na dalili za mtindo huo, kukuta unashindwa kuingia kwenye akaunti ghafla ni moja dalili za kwamba akaunti yako inaweza kuwa imedukuliwa.

Lakini haya maswala hayatakiwi kukuogopesha ila unatakiwa kuwa makini katika kuzingatia usalama wa akaunti yako. Kuna mambo mengi tuliyajadili katika makala ilioelezea jinsi ya kuangalia kama akaunti ya WhatsApp ni salama au laa. Kama haukusoma makala hii, unaweza ipitia ukaelewa zaidi juu ya hilo.

Kuvamiwa na kuilinda akaunti yako ya Whatsapp kwa sasa

Hapa tuzungumzie namna ambayo watu wengi hupoteza akaunti zao za WhatsApp Katika kipindi hiki.

Katika mitandao, kuna link ambozo unaweza bonyeza ukapelekwa kwenye kurasa, zikakudai namba ya simu ya WhatsApp na baada ya kuweka namba, unapokea sms kwenye simu yako ambayo ina Code ambazo wanasema uwape ili kuthibitisha.
Ukiwapa hizo code tu, akaunti yako ya WhatsApp inakuzuia usiingie na hata ukifanikiwa kuingia unaweza kuta mambo wengi ambayo hauja yafanya wewe yamefanyika au yanaendelea kufanyika.

Mbali na kubonyeza Link za mtandaoni, unaweza fuatwa na mtu tatika mitandao na akakuomba umpe Code ulizopokea kwenye simu yako alafu ukimpa tu, unapoteza akaunti.

Kuilinda akaunti yako dhidi ya njia hii ya uvamizi

Kuepuka kuvamiwa kwa akaunti yako kupitia njia hii, hakikisha hauweki namba yako ya simu kwenye tuvuti au kurasa ambazo haujazijua kiundani. Ukibonyeza Link ambayo hauimani na ikakudai namba yako, usiweke maana unaweza kuwa ni mtego wa kupoteza akaunti yako. Mara nyingi huwa wanadanganya kupata pesa za bure au vitu vingine vya Bure.

Pia kujiweka salama zaidi, hakikisha unakua makini na akaunti za rafiki zako unaochati nao. Kama utaona akaunti ya rafiki yako inafanya vitu ambayo sio kawaida yake kufanya, fahamu kuwa anaweza kuwa amevamiwa.

Mbali na hayo, unasisitizwa kutumia WhatsApp zilizo rasimi ili kujihakikishia usalama zaidi. Whatsapp nyingi zisizorasmi huwa sio salama kwa akaunti yako.

Jambo la kufanya ili kuirudisha akaunti ya WhatsApp iliochukuliwa.

Uzuri wa WhatsApp ni kwamba unaweza irudisha akaunti yako kwa kutumia namba ya simu. Hakikisha unaiingiza namba yako ya simu kwenye WhatsApp yako ili utumiwe tena Code alafu baada ya hapo utazijaza Code walizokutumia kisha utafanikiwa kuingia kwenye akaunti yako tena.

Ukikuta akaunti yako imezuiwa na WhatsApp (banned), unaweza toa maelezo kwenye kisanduku cha ku-request review. Utaeleza kuwa akaunti yako ilidukuliwa, umepambana kuirudisha lakini umeikuta banned (ni vizuri ukiandika maelezo hayo kwa kiingereza).
Wakiangalia vizuri maelezo yako na kulinganisha mambo yaliotokea kwenye akaunti yako, wataondoa ban na kuruhusu uitumie kama kawaida.

Leave a comment