DAWA CHUNGU (Simulizi Fupi ya Kusoma)

Nina mke mzuri sana, na nampenda. Nina uhakika na yeye pia ananipenda. Tumebarikiwa na mtoto mdogo mmoja. Nafanya kazi, lakini kuna kipindi mambo yangu ya kikazi yalienda vibaya. Kipato kikawa kidogo sana. Mke wangu alianza kudai mahitaji ya nyumbani na mtoto kila wakati. Kila alivyodai, ndivyo nilivyoanza kumwona kama kero, maana hachoki kusema. Hali hii ilinipeleka kwenye uhusiano wa pembeni na binti mmoja mzuri, mdogo alafu mjanja mjanja, anayekaa mtaa wa tatu kutoka kwangu.

Nilikutana naye katika sehemu za starehe. Nilienda pale kupoteza mawazo kwa kunywa pombe kama wanavyoseoma. Tulipokutana huko, furaha yangu ilianza kufufuka hivi. Kila nilipopata pesa kidogo, badala ya kupeleka nyumbani, nilikua naenda kwenye sehemu za starehe, nampigia simu huyo binti aje tuwe wote. Yeye alinipa furaha zaidi kuliko mke wangu kwa kipindi hicho, maana tulilewa pamoja, tulikuatunacheka, na kufanya mambo mengi ambayo sikufanya na mke wangu. Mke wangu tukitulia alikua nawaza kunidai na kuniambie matatizo. Hali hii huwa inatesa sana.

Pamoja na yote hayo, bado nilimpenda sana mke wangu. Niliweka siri hiyo, sikutaka ajue chochote maana najua na yeye ananipenda sana ila maisha ndio yanatufanya tuwe kwenye hali hiyo. Mioyo yetu inapendana sana ila mifumo ya maisha ndio tatizo.

Siku moja kazini, mpango mmoja niliokuwa nao ulienda vizuri, nikapata pesa nyingi kiasi kwa mpigo. Nilikuwa na furaha kubwa, nikaingiziwa pesa kwenye simu. Badala ya kufikiria familia yangu au mke wangu, akili yangu ilikimbilia kwenye starehe maana ilikua ni kama nimezoea hivi. Mwanzo nilianza kwa lengo la kupoteza mawazo lakini mwisho ikawa tabia yangu bila kushtuka.

Sika hiyo nilipanga kujipongeza kwa kukutana na yule binti tufanye starehe. Nilifika kwenye sehemu ya starehe, nikapata chupa moja ya pombe na kuanza kunywa. Wakati nakunywa nikatuma ujumbe kwa yule binti “Njoo sasa, nina furaha sana kuliko siku zote, nataka uje tufurahi pamoja.” Siku jieleza sana maana niliongea nae kabla.

Kabla huyo binti hajajibu, nikakuta mke wangu anapiga simu. Siku taka kupokea, niliiacha ikiita huku nikiendelea kunywa pombe kidogo kidogo. Baada ya muda simu iliacha kuita, nikakuta ujumbe toka kwa mke wangu unaingipia. Sikutaka hata kufungua hivyo sikujua alichoniandikia. Baada ya dakika moja yule pinti alinijibu ujumbe niliomtumia.
Alinijibu kuwa alikuwa na matatizo yaliyohitaji kiasi fulani cha pesa. Alisema akiipata hiyo pesa popote, atakuja. Kwakua mimi nilikua na pesa, nikamwambia asiwe na wasiwasi, nitamtumia hiyo pesa ndani ya dakika tano.
Baada ya kumwambia hayo, nilianza mchakato wa kumtumia pesa yule binti. Nikachukua simu na kuandika kiasi cha pesa anachohitaji kisha nikatuma.
Baada ya kutuma tu, nikamuandikia yule binti ujumbe uliosemeka “Tayari nimeisha tuma. Itumie hiyo pesa kwenye hayo mambo yako yote alafu tufurahi wote maana ninafura na furaha yangu nataka nifurahi nikiwa na wewe mpenzi wangu” kisha nikautuma.

Lakini baada ya dakika nilishangaa kuona ujumbe wa shukrani kutoka kwa mke wangu. “Asante sana mume wangu. Sijui nikupe nini wewe mwanaume. Mungu akulinde na kukubariki sana pacha wangu. Najiona nina bahati kuwa na wewe”

Nilishangaa sana. Nilipochunguza, nikakumbuka kuwa sikuusoma ujumbe wa kwanza wa mke wangu. Nipousoma nikaona ulikuwa ni wamalalamiko mengi kuhusu mahitaji ya nyumbani na mtoto wetu.

Hapo akili yangu ilianza kukaa vizuri: kumbe pesa niliyotuma, nilimtumia mke wangu kimakosa badala ya yule binti! Mbaya zaidi, nilikuwa nimeandika kiasi kikubwa cha pesa kuliko nilivyokusudia. Sijui zilikua ni pombe au nini ila kukosea kuandika kiasi cha pesa kulifanya pesa nilioituma kuwa kubwa sana kuliko iliobaki kwenye simu yangu. Na kumbe hata ule ujumbe nilipotaka kumtaalifu yule binti,nimemtumia mke wangu pia.

Nilichanganyikiwa. Pombe kichwani ilikata ghafla. Nikabaki nimekaa pale, huku simu ya mke wangu ikiendelea kuingia na ujumbe wa shukrani ukija mmoja baada ya mwingine.
Hakukuwa na maneno mengi ya kumwambia. Nilijua ningesema jambo lolote, basi ningeharibu ndoa yangu. Ingenibidi nieleze hiyo pesa nyingi hivyo nilikua natuma wapi alafu pia ujumbe niliokosea kumtumia kwanini una neno “mpenzi”.
Nilijaribu kuwasiliana na watu wa mtandao kidogo ili warudishe ila nikaacha. Nikaona kama hiyo pesa imeokolewa na mungu maana kiasi kile cha pesa kingeenda kwa yule binti mjanja wa mjini, sidhani kama ningefaidika chochote. Bora mke wangu kaipata maana ni kama nimepunguza matatizo ya nyumbani kidogo.

Baade nilirudi nyumbani nikamkuta mke wangu anafuraha sana. Yani alikua ananiangalia hanimalizi maana hakutegemea jambo lile. Alikuwa amenipikia chakula kizuri, na kila kitu kilionekana kama sherehe humo ndani. Alinipongeza na kunishukuru kwa msaada wa kifedha ambao kimoyomoyo sikupanga kumpa. Akili yangu ilikuwa kwenye pesa yangu kuwa nimetuma kimakosa.

Sikuweza kurudisha pesa hiyo mikononi mwangu wala kuliongelea sana. Ila kufidia kidogo pesa yangu nilimkopa mke wangu kiasi kidogo baada ya wiki na akakubali bila kusita maana ananiamini. Hiyo pesa niliyokopa, sina mpango wa kuirudisha japo yeye anadhani nitarudisha.

Pamoja na yote siwezi jilaumu sana kuhusu tukio hilo maana lilimfanya mke wangu aanze kuelewa kidogo nikimwambia niko vibaya kwenye pesa. Alikua anaamini kuwa nikipata pesa huwa namkumbuka. Na kweli kwanzia tukio hilo limenitokea, huwa namkumbuka sana mke wangu. Ukimfanyia jambo lolote zuri la bila kutarajia huwa anachanganyikiwa kwa furaha.

Mwisho

Leave a comment