Kuanza uhusiano mpya ni jambo zuri ambalo huambatana na furaha, lakini pia mwanzo wa mahusiano ni wakati kufahamiana vizuri. Tunafahamu kuna watu ambao huanza mahusiano wakati wameisha fahamina vizuri, lakini pia kuna watu wengine huanza kufahamina vizuri baada ya kuingia kwenye mahusiano(katika hatua za awali).
Katika hatua hizo za awali za mahusiano, mazungumzo yanakua na nafasi kubwa ya kujenga msingi wa mawasiliano bora. Watu huulizana maswali ambayo yatasaidia kufahamiana zaidi na kuelewa malengo, matamanio, na mawazo ya kila mmoja. Maswali yanaweza kuwa njia bora ya kuanzisha mazungumzo na kuchunguza ikiwa mnalingana kihisia, kiakili na hata kimaisha.
Kila mtu huwa na mambo yake tofauti anayotaka kujua kwa mpenzi mpya, lakini kuna mambo ya msingi ambayo kila mtu anapaswa kujua kuhusu mwenzi wake mpya ili kujenga mahusiano imara na hata kuepeka baadhi ya mambo mabaya. Mwanaume au mwanamke kujua tabia, malengo, na mtazamo wa mpenzi wake kunaweza kusaidia kuunda uhusiano imara zaidi na kuepuka mambo mabaya yanayoweza jitokeza mbeleni.
Mara nyingi, watu huingia kwenye mahusiano bila kuzungumza masuala muhimu mwanzoni na baadae hupata changamoto nyingi kwenye mahusiano yao. Kuuliza maswali mwanzoni kunaweza kufungua mambo mbalimbali juu ya mahusiano ulioyaanzisha.
Kati ya maswali muhumu sana kumuuliza mpenzi mpya kwa kipindi hiki ni yafuatayo hapa chini:
Maswali ya kumuuliza Mpenzi wako Mpya (mwanamke au mwanaume)
Una Mpenzi?
Baadhi ya watu huona kumuuliza mpenzi mpya “Una Mpenzi?” ni jambo baya lakini si kweli. Mara nyingine kuuliza swali hili, kunaweza kukufanya utambue uko kwenye mahusiano nae kama mtu pekee au Kuna mtu unamuibia mpenzi wake. Ni Bora ukauliza tu na hatakama atakwambia hana mpenzi wakati anae, hofu na wasi wasi vitakua kwake na sio kwako.
Na akikwambia anae mpenzi, basi unaweza kuwa makini huku ukipambana kuonesha upendo wako ili kumfanya asigeuke nyuma.
Kama utashindwa, pia ni sawa kuheshimu maamuzi yake. Ila fahamu tu kuwa, kujua jambo hili litakufanya uepukane na migogoro ya mapenzi. Na pia hatakama ikitokea amekusaliti na kwenda kwa mpenzi wake, moyo wako utakua kuna jinsi upo vizuri kidogo maana ulikua unajua.
Ndoto yako kubwa katika maisha ni ipi?
Kuuliza kuhusu ndoto za mpenzi wako mpya, kutakufanya umfahamu kwenye upande wa maisha. Mara nyingi watu tunaishi tukikimbiza ndoto zetu na ni ngumu sana kumuelewa mtu anavyopambana kama haujui anakimbiza ndoto gani.
Swali hili linaweza kukufanya uelewe mpenzi anapambania nini maishani. Hii itafanya ukimuona anapambana, utakua unajua ni kitu gani anafanya na hata kumsaidia ikiwezekana.
Kama ataongelea ndoto za kuwa na familia, basi huo ndio wakati mzuri wa kupanga mipango yenu ya kuwa pamoja.
Umewahi kupima HIV?
Swala la HIV (Virusi vya Ukimwi) ni jambo muhimu kama unajali afya yako na ya mpenzi wako. Kama hauna HIV, ni vema ukamuuliza mpenzi wako mpya kuhusu kupima HIV ili ujue hata analichukuliaje ilo swala. Mara nyingi huwa watu hawasemi ukweli lakini kitendo cha kumuuliza kutafanya hata akiwa na HIV awe makini au afikilie mara mbili anaposhiriki tendo na wewe.
Kama wewe ndie una HIV, Bado kunaweza kuwa na umuhimu wa kuuliza maswala ya haya ili ikitokea bahati mbaya umempatia HIV, aelewe kuwa lengo lako ilikua ni kumuokoa asipate.
Umejifunza nini kutoka kwenye mahusiano yako ya zamani?
“Mahusiano ya zamani” yamefanya watu wawe na mitazamo mingi sana mibaya kuhusu Mapenzi. Yani, kuna watu mahusiano yao ya zamani yamewafunza kutopenda tena, kutomwamini mtu kwenye mapenzi, kuamini mapenzi ni pesa tu na hata kuamini kuwa wanatakiwa kuacha kabla hawajaachwa maana mapenzi ni maumivu tu.
Sasa swali hilo linaweza kukufanya uelewe mpenzi wako mpya anamtazamo gani kuhusu Mapenzi. Kama atakua na mtazamo mbaya, unaweza mfanya abadilishe mtazamo wake kwa kumuonesha upendo wako wa tofauti huku ukimwambia mapenzi hayapo jinsi anavyofikilia.
Wengi ukiwaonesha mapenzi ya kweli huwa sawa kabisa na hubadilisha mitazamo yako ikawa mizuri mpaka mwisho.
Lakini kuna mwingine baadae ataanza kuendeshwa na mitazamo yake mibaya juu ya mapenzi na mpaka ukashindwa kumweka sawa. Huyu utajua tu kuwa tatizo ni mahusiano yake ya zamani.
Vitu au mambo gani haupendi na nini unapenda?
Ni muhumu kumuuliza mpenzi wako mpya maswali ambayo yatakufanya ujue mambo au vitu gani anaependa. Ni vema kumuuliza vitu au mambo gani huwa hapendi. Katika upande wa “Kupenda”, Unaweza kumuuliza kuhusu chakula, sehemu anazopenda kutembelea, nyimbo anazopenda kusikiliza, filamu anazopenda kuangalia, mchezo anayopenda na mambo mengine. Katika upande wa “Kutopenda” unaweza muuliza mambo kama Tabia, vyakula na mambo mengine unayotamani kujua anayapenda au vipi.
Tukitimiza mwaka 1 wa kuwa pamoja tufanye nini kusheherekea penzi letu?
Swali hili limekaa kama ahadi ya utani hivi. Lakini mara nyingi huwa linafanya muwekeane ahadi ya kulituza penzi lenu jipya mpaka lifikie mwaka. Kama mnapendana kweli, basi mtasafiri kimawazo na kuyaona mahusiano yenu yakidumu zaidi ya mwaka pamoja hatakama sasaivi ni mapya.
Katika mwaka kunaweza kuwa na misukosuko mingi sana lakini wazo la kwamba umekubaliana kuafnya kitu flani baada ya mwaka, ilaweza wafanya mshikamane.
Hii ni njia nzuri sana ya kuweka matumiani ya kuwa pamoja. Watu wengi ambao hawajaoana huwekeana ahadi ya Ndoa, lakini ndoa inaweza chukua muda kutimia. Ila hii njia ya kufurahia kila mwaka inakua inawapa matumaini huku mukiendelea kusubiri siku ya ndoa.
Mnaweza kuwa mnafurahia kwa kupeana zawadi au kwenda matembezi ya pamoja kwenye sehemu tofauti. Sio lazima utumie gharama sana au kuwashirikisha watu siku hiyo.
Maswali hayo tulioyazungumza hapo juu, ni mzuri sana kwa mwanamke na Wanaume pia. Hivyo, usisite kumuuliza mwenza wako mpya kama utapata nafasi inayomuhusu kuyauliza. Mbali na maswali hayo ukuna maswali mengine hapa chini ambayo hatujayapa maelezo ila unaweza muuliza mpenzi wako mpya.
- Unapenda kufanya nini ukipumzika?
- Mahusiano mazuri kwako yana maanisha nini?
- Ni kitu gani kinaweza kukufurahisha hata ukiwa hauna furaha?
- Kuna kitu chochote unatamani nifahamu kuhusu wewe mpenzi?
- Hivi mpenzi, nikifungua moyo wako ndani yake unahisi nitaona nini?
Ni hayo tu katika ukurasa huu ulioletwa kwako na The bestgalaxy. Usiache kutembelea The bestgalaxy kila mara unapo pata nafasi ili kujifunza mambo mengi kuhusu mahusiano na Mengineyo. Usisahau pia kuchukua simulizi ya Mapenzi ya SUKARI YA DADA ambapo utapewa na simulizi nyingine kama zawadi.
