UNANIITA? (Simulizi Fupi ya Kusoma)

Nilikua kijana mdogo tu niliyepambana kujenga maisha yangu. Kazi yangu ilikuwa ni kuendesha pikipiki, yaani nilikuwa bodaboda hapa mjini. Siku moja, nikiwa kazini, alinisimamisha dada mmoja ili nimpeleke kwake. Nilisimamisha pikipiki yangu, nikambeba na safari ikaaanza kuelekea kwake. Huyu dada alikuwa mweupe, mzuri sana, na ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona.

Njiani, alianza kulalamika kuhusu bodaboda wake wa kila siku; alisema amemchoka kwa sababu huwa anachelewa na hapendi muonekano wake maana hajipendi kabisa alafu akanisifia mimi kuwa ni asafi. Aliponisifia kwa usafi na jinsi nilivyopendeza, nilijisikia vizuri. Alisema anatamani bodaboda wake awe msafi kama mimi. Nilikuwa na tabia ya kujipenda na kujiweka safi kila siku, nikiamini kwamba kuwa hivyo kunaweza kufungua milango mingi maishani.

Tulipofika kwenye nyumba yake, niliona ni nyumba kubwa yenye wigo mrefu. Sikuingia ndani ya wigo, nilimshusha nje ya nyumba na akanilipa pesa yangu. Aliomba na namba yangu ya simu, akisema atakuwa akinipigia kila anapohitaji bodaboda. Nilijisikia vizuri kupata mteja mpya.

Siku iliyofuata, mchana, nikiwa kwenye kijiwe cha bodaboda, simu yangu iliita. Ilikuwa ni Zena, yule dada mzuri niliyembeba jana. Aliniomba nimfuate nyumbani kwake, alikuwa anaenda sehemu. Nilifika kwake na kumpigia honi nikiwa nje. Wakati nasubiri, nilitupia macho ndani ya wigo kupitia nafasi ndogo ya geti. Niliona gari moja kali sana likiwa ndani na nikajiwazia, “Hivi kwa nini hawa matajiri wanapanda bodaboda wakati wana magari ya kifahari? Ningekua mimi, Hilo gari lisingetulia hapo”

Baada ya dakika chache, Zena alitoka nje akiwa amependeza sana. Nilijiweka vizuri na kumkaribisha kwenye pikipiki. Tukiwa njiani, aliongea na simu kwa sauti ya upole, lakini niliweza kusikia sauti kubwa ya mwanaume akimjibu kwa hasira: “SIMESEMA NITAKUPIGIA! KWA SASA NINA KAZI NYINGI WE MWANAMKE! SIKU NIKIRUDI, TUTAONGEA VIZURI MAANA NINA KAZI ZA WATU HUKU. YANI KICHWA KINA MAMBO MENGI SANA” Huyo mwanaume alionekana kumuumiza Zena, na baada ya kukata simu, Zena alionekana kuwa na huzuni.

Nakumbuka akaniuliza, “Hivi nyie wanaume mnataka nini? Mwanamke anapokupenda mnamuona kama hana thamani.”

Mh mimi nikasema “Mh kwanini unasema hivyo?” akasema “Wanaume mnatesa sana mwanamke anaewapenda… Yani mwanamke akiwapenda na kuwa muwazi, huwa mnamuona mjinga sana”. Mimi nikasema “Hahaha hiyo inategemeana na Tabia ya mtu. Mwanaume wengine huwa wanawapenda wanaowapenda”. Niliposema hivyo yule dada akasema “Dah huyu mwanaume wangu ananiumiza sana mpaka naanza kuchoka”. Mimi nikacheka tu “hahaha” maana hayo ni mambo yake binafsi na hata sikutaka kumuuliza sana kuhusu huyo mwanaume.

Lakini yeye akaendelea kuongea kwa kusema “Yani Tangu amenioa, Hana muda wa kunizingatia. Anakua anazingatia kazi zake alafu ananiona mimi kama msela wake tu. Hana maneno mazuri ya kuongea ili hata nijisikie tupo kwenye mahusiano. Akiwa mbali na nyumbani huwa hajibu sms wala haniruhusu kuongea nae vizuri kwenye simu. Sijui anataka nini? Yani naona kabisa hanipendi huyu mwanaume maana ananitesa.”

Mh mimi hapo nikacheka tena tu “hahaha” maana hayo ni mambo yake binafsi lakini hakuishia hapo, akiniuliza “Wanaume wote ndio muko hivyo kweli?”. Mimi nikasema “Hapana ila unaweza kuta yupo na kazi nyingi ndio maana yupo hivyo. Hata mimi nikiwa naendesha pikipiki huwa nashindwa kuwasiliana sana na watu kwenye simu zaidi ya abilia wangu”.
Nilipo sema hivyo, akaniambia “Lakini si ukitulia hata mida ya usiku unamtafuta mpenzi wako, unaongea nae vizuri?”. Nikamjibu “Ndio, na sio lazima usiku. Nikipata muda hata huo huo mchana huwa naongea nae vizuri tu” Yule dada akajibu “Mimi huyu mwanaume hayupo hivyo. Akirudi nyumbani huwa anasema anachoka sana, nisimsumbue hata kwa kumgusa. Alafu akiwa kazini hataki kuongea sana kwenye simu”.

Mh mimi sikutegemea kabisa huyo dada mzuri kukutana na changamoto kama hizo. Mimi kwa uzoefu wangu nikiwa kama mwanaume nikamwambia “Jaribu kuwa una mtumia Ujumbe wa kuamsha hisia au kama unaongea nae uwe unaongea vitu vya kuamsha hisia. Mimi hata nikiwa kwenye kazi nikiona mpenzi wangu kaniletea hivyo vitu huwa najikuta namzingatia kuliko kazi hahaha”.

Huyo dada akajibu “Vitu vya kuamsha hisia kama Vipi sasa?” Nikaona aidu kumuelekezea moja kwa moja, nika mwambia tu “Hahaha Yani sijui nikuelezee vipi… Ila nyie wanamke ndio mnavijua sana hivyo vitu” akatulia sekunde chache alafu akasema “Anha sawa, nimekuelewa…. Nimewahi mfanyia lakini kwakua umeniambia, nitajiribu nione kama itasaidia”

Baada ya kumpeleka saluni kama alivyotaka, nilimuaga alafu nikaja kumrudusha nyumbani tena kisha kuendelea na kazi zangu. Zena alinilipa vizuri na nilirudi kijiweni. Siku mbili baadaye, usiku wa saa nne, nilipokea ujumbe kutoka kwa Zena: “Umelala?” Nilimjibu kwa kumwambia kuwa “Sijalala, Bado niko kazini na baada ya dakika chache nitakua nikiwa kwenye safari ya kumpeleka mteja sehemu flani hivi. Nikitoka huko ndio natarudi nyumbani kulala maana najisikia vibaya sana, Leo nitawahi kulala.”

Akaandika tena, “Pole, unajisikia vibaya, unaumwa nini?” Nikamwambia “Uchovu wa kawaida wa kazi ya bodaboda, ila Leo umezidi. Viungo vya mwili vyote vinauma”. Aliniambia, “Pole sana, lakini si una mpenzi wako akukande mwili?”

Nilicheka kidogo mwenyewe, maana ukweli ni kwamba sikuwa na mpenzi. Mpenzi wangu aliniacha mwezi uliopita bila sababu yoyote, lakini sikuwa na nia ya kumwambia hilo Zena maana hayamuhusu. Niligeuza mazungumzo na kuuliza kama alihitaji nikambebe tena kwa pikipiki. Akaniambia, “Hapana, mda huu niko tu peke yangu nyumbani, najihisi upweke mpaka nimeona nikujulie hali.”.
Kwakua muda huo mimi nilikua naenda kupeleka mteja sehemu na pikipiki, nilimwambia Zena “Sawa, ila sasaivi ndio naenda kumpeleka mteje hivyo nitakutumia ujumbe baada ya dakika chache ili tuendelee kuwasiliana” akajibu “Sawa, hapa silali, nitakusubiri mpaka unitumie ujumbe”. Mimi nikajibu “Hahaha Sawa, usijali”.

Basi nikaacha maongezi nae hapo alafu nikaenda kwenye kazi. Nilivyorudi nikapitiliza kulala tu bila hata kumtafuta kwenye simu.

Asubuhi ilipofika, nilikuta Zena amenitumia ujumbe mara nyingi sana usiku na hiyo asubuhi alinitumia tena ujumbe wa salamu za asubuhi. Nilipomjibu, alinipigia simu hapo hapo. Aliniuliza kwa kama kautani hivi kuwa “Mbona jana hukunitafuta tena? Au ulikuwa na mpenzi wako?”
Nilicheka na kumjibu, “Hapana, Samahani sana. Nilipotoka kule Uchovu ilizidi zaidi nikajikuta nimepitiliza kulala. Yani Uchovu ni mwingi mpaka muda huu bado najisikia vibaya na sijui nafanyeje.”

Akasema, “Mh kama bado unajisikia vibaya, njoo jioni kwangu nikupatie dawa” Nikamuulaza “dawa gani hiyo?” Akasema “Ni mafuta flani hivi unayapaka kwenye viungo vinavyouma huku unakanda mwili na maji ya moto. Utamwambia mpenzi wako aitumie kuviweka sawa viongo vyako.” Mh mimi kusikia mambo ya hayo na Sina hata huyo mpenzi, nikamwambia tu “Sawa, nakuja kuchukua jioni”
Baada ya kuongea hayo tulikata simu nikaenda na kazi za Kila siku. Lakini hiyo siku nilikua napokea sms nyingi toka kwa Zena. Na nilikua na jibu maana niligundua ni mtu mpweke sana na ameanza kama kunipenda hivi. Mimi kumpenda nilikua nampenda ila namuheshimu kidogo kama dada alafu pia ni mke wa mtu.

Jioni ilifika nikaenda kwake mpaka ndani. Nilikuta anaangalia TV na nilivyofika akanipa chakula. Baada ya kunipa chakula, nikiwa nakula, nikamuona kama anajiandaa kwenda kuoga hivi maana aliingia chumbani na kutoka na kinguo chepesi alafu kifupi sana. Kwa juu kilikua ni kama vikamba vimepita mabegani.

Nilivyomuona anatoka chumbani hivyo nilimtolea macho ya kutamani maana alikua na mwili mzuri. Moyo wangu ulidunda sana sana baada ya kuona kama anakuja kwangu hivi.

Kumbe kweli, yule dada alifikia mpaka nilipokaa huku akiwa naniangalia machoni toka mbali. Nakumbuka alipokuja karibu yangu akaniambia “Umeniita?”. Nilishangaa sana kusikia hivyo maana Sikua nimemuita hapo. Na moyo wangu ulikua unadunda kwa kasi sana kutokana na matamanio yangu muda huo. Macho yake yalikua yamelegea sana alafu asilimia kubwa ya sehemu za juu ya magoti zilikua zinaonekana.

Mdomo ulikua mzito sana muda huo. Jambo aliloniuliza nililikataa kwa kwa gigugumizi sana “hapana… Sija… Sija… Sijakuita mbona” nilivyosema hivyo, akaacha kusogea nilipo, akasema tu “anha sawa, labla nimesikia vibaya” kisha akaanza kwenda chumbani kwake tena.

Aliniacha pale moyo unadunda sana alafu nilikua sielewi maana sahihi ya jambo alilolifanya. Macho yake hayakuacha kuuangalia mwendo wake wa kujitikisa alipokua akielekea chumbani.

Yani hata chakula nilichokua nakula muda huo nilikiacha kwa muda, nikawa nimeganda nawaza maana ya tukio lile.

Baada ya kama ya dakika 3 hivi, Nikakuta kuna ujumbe mpya umeingia kwenye simu na mtumaji alikua ni Zena. Nilifungua huo ujumbe nikakuta umeandikwa “Njoo huku chumbani unisaidie kitu flani”. Mh nilishtuka nikajua tu kinachoendelea hapo ni kutegana na sio kingine. Nilimjibu “Kitu gani hicho?” Akajibu “We njoo basi, Acha woga”.

Basi sikua na jinsi, niliamua kunyanyuka na kuanza kuelekea kwenye hicho chumba. Nilopofika Mlangoni, nikapiga hodi, akaniambia “Sukuma tu mlango, ingia”. Na Mimi kweli nikafanya hiyo ili kuingia ndani.

Sikutarajia kuwa nitaingia kwenye mitego yake kirahisi hivyo. Ila ndio hivyo, nilishaingia tayari kwenye mtego na nilikua nimeisha tekwa hisia.

Humo ndani hatukua hata na cha maana cha kuongea. Tulikaa kwenye kitanda na sikumbuki tuliongea nini ila nakumbuka tulianza kurukiana rukiana humo ndani na yule dada.

Tukitumia muda mrefu sana humo ndani maana huyo dada alikua ni hatari sana. Nilijikuta silazi Damu kabisa.

Mwisho tulimaliza alafu akanilaza na kuanza kunikanda na maji viungo vilivyokua vinaniuma kama alavyokua akiongelea. Hicho kitu nilikua sijawahi fanyiwa. Huyo dada alifanya viungo viwe vizuri mpaka nikatamani ningekua ndio mume wake.

Siku hiyo nilitoka humo ndani nikiwa tayari nimeingia kwenye penzi na uyo Dada. Huyo dada alikua anasema ananipenda kuliko mume wake. Kwanzia hapo, tuliendelea kuwasilina kupitia simu na kuna muda tulikua tunakutana na kufurahia mambo yetu.
Tuliendelea kuwa na mawasiliano, na mara kadhaa tulikutana tena. Lakini mambo yote yalibadilika nilipopokea simu ya vitisho kutoka kwa mtu aliyedai kuwa ni mume wa Zena. Aliniambia ameunganisha simu ya mke wake na anaona ujumbe wote tunaotumiana. Alinipa onyo kali kwamba kama sitamuacha mke wake, atanichukulia hatua mbaya.

Niligundua kuwa nilikuwa kwenye hatari kubwa. Niliamua kumkwepa Zena, nikabadilisha hata namba yangu ya simu ili kuepuka mawasiliano naye. Japokuwa nilikuwa tayari nimempenda, nilijua kwamba kuendelea naye kutaharibu maisha yangu na ya kwake pia maana mume wake anapesa.
Mpaka sasa moyo yangu unampenda yule dada na natamani ajue hilo. Natamani ajue kuwa napenda kumuona na furaha, hata kama siyo nami.
Namfikiria na namuombea awe na furaha kwenye ndoa yake. Nilitamani sana kuwa naye, lakini niliamua kuheshimu ndoa yake. Hata sasa, bado sijapata njia ya kumsahau kabisa, lakini najua kuwa penzi letu haliwezi kuendelea.

Mwisho

2 thoughts on “UNANIITA? (Simulizi Fupi ya Kusoma)”

Leave a comment