Nilihamia kwenye nyumba moja nzuri nikiwa napambana na maisha. Nilipata chumba kizuri sana, cha kisasa, lakini bei ya kulipia ilikuwa ndogo mno. Jambo Hilo ndio lililonivutia na nilivutiwa zaidi na utulivu wa nyumba yenyewe na upatikanaji wa huduma pia. Wenye nyumba walikuwa ni mume na mke, wakikaa peke yao bila mtoto yeyote. Kwa miezi michache, niliishi pale kwa amani bila shida yoyote, tukiheshimiana na wenye nyumba.
Siku moja, mtoto wao wa kike, Doris, alirudi kutoka masomoni. Hakuwa akiishi nao hapo muda mrefu kwa sababu alikuwa akisoma chuo, lakini alikuwa kwenye likizo kipindi hicho. Kabla hajaja nilikuwa nimesikia wazazi wake wakimzungumzia mara kadhaa, lakini sikuzingatia sana.
Aliporudi, mara ya kwanza kumwona nilishtuka kidogo. Doris alikuwa anamwili mdogo kiasi alafu mzuri wa kuvutia. Nilijikuta nashindwa kutomwangalia kila tulipokua tukipishana hapo nyumbani. Siku za mwanzo tulikuwa tukisalimiana tu kwa kifupi sana alafu bila mazungumzo hasa pale wazazi wake walipokuwapo karibu. Kuna wakati tulikuwa tunapitana kama hatuonani kabisa, kila mmoja anakua na mambo yake.
Siku moja, nilikuwa sokoni nikinunua mahitaji yangu ya kila siku. Wakati narudi, mvua ndogo ilianza kunyesha taratibu, lakini haikuchukua muda mvua ikaanza kuongezeka. Niliona ni heri nikimbilie nyumbani kabla haijawa kubwa kabisa. Wakati nakimbia, nilimuona Doris mbele yangu akitembea taratibu, akiwa amejifunika na mwamvuli. Bila kufikiria sana, niliamua kumkimbilia ili nijiunge naye chini ya mwamvuli wake.
Aliniona nikimkaribia, akaniangalia kwa haraka kisha akaniwekea mwamvuli vizuri ili utukinge wote. Nikiwa hapo, niliamua kufungua mazungumzo nea kwa kusema “Bora ulikuja na mwamvuli! Ulijuaje kama mvua itanyesha?” huku tukitembea.
Alitabasamu kisha akasema, “Niliona mawingu yanakusanyika, nikaona ni bora nijipange mapema kwa kuja na mwamvuli.” Sauti yake ilikua ya kuvutia sana. Nilijikuta nikiendelea kuongea nae kwa kumwambia, “Dah asante kwa kuniokoa. Huenda hua unaongea na Mungu wewe.”
Tulicheka pamoja, na mazungumzo yaliendelea kuwa mazuri sana. Safari ya kurudi nyumbani, ilionekana kama hitaisha haraka hivi… Na hatukutaka ifike mwisho. Doris alikuwa na harufu nzuri, na jinsi alivyoongea, nilivutiwa naye sana siku hiyo. Baada ya maongezi mazuri, alinionyesha kuwa anaweza kuwa rafiki na akanipa mpaka namba yake ya simu ili tuendelee kuchati kuwasiliana nae.
Tulipofika nyumbani, tulitengana kama hatukua wote. Kila mtu aliendelea na shughuli zake, lakini ndani yangu, moyo uliacha kuzingatia kazi yake ya kusukuma Damu, ukaanza kumpenda sana Doris.
Kwanzia siku hiyo, urafiki wetu uliendelea kukua. Nilianza kuwa mjanja, kila niliposikia wazazi wake wamemtuma sehemu fulani, nilihakikisha na mimi natoka kwa wakati huo ili tutoke pamoja. Hali ilifika mahali nilishindwa kuvumilia, nilimwambia kuwa na mpenda na nahitaji awe wangu.
Hakunisita hata kidogo, alikubali maana na yeye alikua ananipenda, na hapo uhusiano wetu wa siri ukaanza rasmi. Tuliendelea kuonana kisirisiri kila tulipopata nafasi. Tulikua tukitumia muda mwingi nje ya nyumbani ili kuepuka macho ya wazazi wake. Lakini kama unavyojua, hakuna siri inayodumu ikionwa na majirani. Majirani walianza kutusema, kwa wazazi wake Doris alafu wazazi walianza kututazama kwa macho ya mashaka. Walijaribu kutuchunguza lakini hawakuwa na ushahidi wa moja kwa moja, hivyo wakawa wanafikiria tu.
Siku moja, Mchana, Doris aliniambia usiku niache mlango wangu wazi, kuna jambo la kuniambia. Sikutaka kumuuliza sana, lakini nilihisi alitaka kufanya ninachokitamani kufanya nae lakini nakosa mbinu. Usiku ulipofika na watu wakiwa wamelala, nilihisi mlango wangu ukisukumwa, kisha nikaona anaingia Doris.
Basi utulipiga stori humo ndani kwa visauti flani ya chini chini mwisho tukaanza kutamani kushikana. Ndani ya muda mchache tukawa tayari tunaucheza mziki humo ndani. Huo mziki Doris alikua anataka sana na Kila nikibandika alikua analalamika lakini hataki nibandue. Doris alionekana kuwa na kiu ya kucheza na nami mziki mpaka ananivuta kwake. Niliendelea kufurahia kuwa naye huku nikiwa na hofu ya wazazi wake kujua. Nilikua najitahidi sana mziki usisikike nje usiku mpaka tukamaliza kucheza, akarudi kwao.
Hiyo ilikua ni siku ya Doris kutoroka kwao na kuja kwangu lakini hakuishia hapo, alikua akipata nafasi usiku anakuja kila mara.
Baada ya kuja mara kadhaa, wazazi wake walijua wazi kuwa kuna kitu kinachoendelea kati yetu. Walichukia sana na wakanipandishia bei ya chumba ghafla ili nihame. Walifikiri ningeshindwa kumudu kodi mpya na kuondoka, lakini mimi niliendelea kuishi pale…
Doris, kwa upande wake penzi lilimchanganya mpaka alifikia hatua ya kukataa kurudi chuo. Alianza kuwajibu wazazi wake vibaya kila walipomwonya kuhusu mimi na nilikua nasikia kabisa. Kila mara walipojaribu kunizungumzia vibaya, Doris alikuwa anatetea sana. Aliwahi hata kuwatishia kujiua kama watajaribu kututenganisha. Kwa kweli, nilianza kuwa na hofu kwa jinsi uhusiano wetu ulivyokuwa unazidi matarajio yangu. Mimi nilijua yatakuwa mahusiano ya kawaida tu alafu tutakuja kuachana baadae kama mahusiano yangu mengine ya huko nyuma.
Wakati hayo yote yakiendelea, siku moja Doris aliniambia kwamba ana ujauzito. Hapo ndipo moyo wangu ulianza kudunda kwa kasi sasa. Sikutarajia habari kama hizo kwa wakati ule alafu yeye alikua anataka azae kabisa. Nilihisi kama maisha yangu yakuwa yenye majukumu makubwa. Niliona kabisa kwenye maisha nitateleza na kuanguka na huyu Doris ni utelezi utakaoniangusha.
Katika hayo Mawazo, wazo la kumkimbia lilinijia maana niliona ndio njia sahihi ya kujiokoa muda huo. Nilianza kupanga kimya kimya jinsi nitakavyohama na kuanza maisha mapya sehemu nyingine. Nikapata chumba mbali na hapo alafu nikaanza kuhamisha vitu kwa Siri Kila usiku unapoingia.

Baada ya kuhamisha baadhi ya vitu vyangu muhimu kwa siri, niliondoka ghafla bila kumwambia. Nilihamia mbali ila sio sana. Nilikua nikifikiria kwamba pengine nikiwa huko nitakua na nguvu ya kumkataa Doris na ujauzito wake alafu nitaanza upya maisha yangu. Lakini usiku huo huo wa kwanza baada ya kuhama, nilikosa usingizi. Nilijikuta nikiwaza sana kuhusu Doris na jinsi alivyokuwa tayari kufanya kila kitu kwa ajili ya upendo wetu. Moyoni mwangu nilihisi kama nilikuwa napanga kufanya kosa kubwa.
Nilikua nikikumbuka jinsi alivyokua anavimba kwa wazazi wake kwaajili yangu, jinsi alivyonipenda, alivyoacha upendo wake kwangu umuendeshe bila kujali chochote kiasi kwamba wazazi wake walifikiri nimemloga. Moyoni mwangu, nilihisi kumwacha Doris kwa sababu ya ujauzito ingekuwa dhambi kubwa sana. Maumivu ambayo niliona naenda kumpa nilihisi kabisa hata mungu awezi nisamehe. Hivyo niliamua kupuuza maamuzi yangu.
Usiku huo huo nilimwandikia ujumbe Doris atoroke kwao aje sehemu niliopo. Baada ya kuja nilimshawishi tuanzishe maisha yetu pamoja. Na kweli, Doris alikubali japo alikua anaogopa kidogo. Tulikio yafanya sio mzuri sana lakini ndio tulianzakuishi pamoja kama mke na mume, ingawa hatukuwa tumehalalisha uhusiano wetu.
Wakati tuliendelea na maisha yetu, wazazi wake walianza kuachana na chuki zao kwangu. Waliniona nikijitahidi na kumtunza binti yao mpaka wanakosa sababu ya kunichukia . Hatimaye walinipa baraka zao, na nikamfanya Doris kuwa mke wangu rasmi.
Sasa tunaishi kwa furaha kama familia. Maisha ya kuishi pamoja Kuna muda yakuwa ni magumu kama haujajipanga lakini namshukuru mke wangu Doris kwa kuwa na mimi mpaka sasa tunamaisha mazuri kidogo.
Mwisho