Mpenzi anaekupenda sana anaweza kukuacha kwasababu hizi

Watu wengi huamini katika mapenzi ya kweli, ambayo mpenzi anakukubali na kukupenda jinsi ulivyo, pamoja na mapungufu yako. Yani kila mmoja anakua anajua kuwa hakuna aliye mkamilifu. Na haya mapenzi ya kweli yanahitaji uvumilivu, heshima, na kujitolea kwa pande zote mbili. Huu ni Upendo hadimu sana na pindi unapopata aina hii ya upendo, unapaswa kuthamini na kuulinda kwa juhudi zote.

Ni kweli, hakuna uhusiano wa mapenzi unaoweza kuwa na watu wakamilifu wa asilimia mia moja maana sisi sote ni binadamu wenye makosa. Unaweza kufanya jambo baya au kuwa na tabia fulani bila kujua ambazo, zinamkera au kumuumiza mwanamke wako au mwanaume wako. Wakati mwingine, hata kama mpenzi anakupenda kwa dhati, mambo haya yanaweza kufikia hatua ya kumfanya ajisikie kutaka kujiondoa kwenye Mahusiano.

Katika makala hii, tutaangalia mambo machache ambayo yanaweza kumfanya mpenzi wako aachane na wewe, hata kama bado anakupenda. Ni muhimu kuelewa kuwa maneno, au maamuzi fulani yanaweza kuathiri mapenzi na kupelekea kuvunjika kwa uhusiano. Kufahamu haya kutakusaidia kuboresha au kauyaokoa mahusiano yako pindi yatakapokua kwasababu hizi.

SMS za kumchekesha mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Mpenzi anaekupenda anaweza kukuacha kwasababu hizi

Kutokujali kuhusu yeye au upendo wake

Awe ni mwanamke au mwanaume, usipoonesha kumjali, hatakama anakupenda anaweza kukuacha. Watu huonesha upendo lakini kama hautawajali wao na upendo wao, basi huondoka zao. Akiona anakutafuta, anakuzingatia na kukuoesha moyo wake unavyokupenda lakini wewe hauoneshi kuzingatia au kujali kwa chochote, kuna siku anaweza kuacha. Anaweza fanya hivyo hatakama moyo wake bado unakupenda.
Ni vema kutambua kuwa kila wanaotuonesha upendo huwa wanahitaji kuzingatiwa pia. Mioyo ya watu wanao tukumbuka na kutupenda hujisikia vizuri tunapo onesha kujali pia.

Dharau

Kwa mwanamke, dharau zinaweza fanya uachwe hatakama una uzuri wa hali ya juu. Kwa wanaume, dharau zinaweza fanya wanawake wajitoe kwenye mahusiano pia. Dharau ina athari kwenye mambo mengi sana hapa Duniani na ndio maana watu wote wanasisitizwa kuwa na heshima.

Kuonesha dharau kwenye mahusiano ya mapenzi, kunaweza mfanya mwanamke au mwanaume wako asiuone thamani yake. Kila mtu anatamani kuwa sehemu ambayo anathaminiwa au kuheshimiwa na sio sehemu anayodharauriwa. Kwaiyo, itafika wakati anaweza jitoa kwenye mahusiano hatakama bado anakupenda.

Kukosa uaminifu

Kama jinsi ilivyo ngumu kufanya kazi au biashara na mtu asie muaminifu, ndivyo ilivyo kwenye mahusiano. Watu wengi hujiingiza kwenye mahusiano wakiwa na matumiani ya kupata mtu ambae watamuamini kumkabidhi Moyo. Na hakuna mtu ambae anatamani kumpenda kwa moyo wote mtu ambae haaminiki kwenye mahusiano.


Endapo utakua na tabia nyingi za kukosa uaminifu kwa mpenzi wako, unaweza mpoteza hata kama anakupenda. Watu huweka mioyo yao sehemu iliotulia na wanayoiamini. Ni vema sehemu hiyo ikawa ni wewe.

Muelekeo wa maisha

Ukiwa kama Mwanamke au mwanaume, kuna umri ukifika ni vema unawa tayari unaelewa maisha yako, unajua muelekeo wa maisha yako na sehemu unahitaji kukifika au mambo unataka kupata. Ukiwa unaishi bila kuujali muelekeo wa maisha yako au unaelekea pabaya, unaweza poteza mpenzi wako hatakama anakupenda sana.

Kuepuka hili, tengeneza vizuri Maisha yako, kuwa mtu unaewaza mambo mazuri na kujiwekea mipango mizuri kuhusu maisha yako. Ukifanya hivyo, mpenzi wako atajiona mwenye bahati kuwa na mwanaume au mwanamke anaejielewa kama wewe. Na hata tamani kukupoteza maishani.

Uchafu au kutojipenda

Ni ngumu mpenzi wako kukuambia “Acha uchafu” au “Haujipendi, upo hovyohovyo” lakini wengi wanapenda usiwe hivyo. Kuwa mchafu na Haujipendi ni mambo ambayo yanaweza fanya mpenzi wako kukuacha na kuvutiwa kuwafuata wengine anaoamini wapo tofauti.


Kuzuia hilo ni vema wewe mwenyewe ukawa msafi wa mwili na mambo yako yote unayofanya. Hakikisha unaweka mwili katika hali nzuri, ondoa harufu na kujipenda kwa kujiweka katika muonekano mzuri kila mara. Kuzoeana na mpenzi wako kusifanye usahau kuwa msafi na kujipenda ni muhumu.

Ni hayo tu muhimu katika makala hii na natumaini yanaweza kuwa msaada kwako ukiwa kama mpenzi, mke au mume wa mtu. Lakini kabla haujaondoka katika ukurasa hii, fahamu kuwa kutomlidhisha mpenzi wako katika tendo, inaweza sababisha kuachwa pia. Kwaiyo hakikisha upo vizuri upande huu pia. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Leave a comment