Maisha yangu yamekuwa si rahisi. Nimekulia mtaani, na kila siku ilikuwa ni kupambana ili nipate chakula na mahitaji ya kila siku. Mara nyingi nilikuwa nafanya kazi za vibarua sehemu mbalimbali. Mtaa wetu ulikuwa na maisha ya kawaida sana, watu walijitahidi kupambana kila siku ili kuishi, wengine wakiwa na biashara zao ndogondogo. Ni kama shughuri za kuimaisha hapo mtaani nilikutana na Mama Cheupe, mama mtu mzima kidogo aliyekuwa akiuza chakula kwenye kibanda maalufu katika maeneno yetu. Alikua na mwilini mkubwa alafu anajipenda sana.
Kwanza, aliniweka kama mteja wa kawaida tu. Nilikuwa napita pale kibandani mara kwa mara baada ya kazi, nikiwa na njaa. Mama Cheupe alikuwa mkarimu sana kwangu. Kuna wakati alikukua akiniuzia chakula kwa bei ya chini au hata kunipa bure kabisa. Ilikuwa ni kama alinijali kwa namna fulani, na nami sikuchukua muda mrefu kuelewa kwamba alikuwa akinisogeza zaidi kwake maana kujali kwake kulipita kiasi.
Siku moja, aliniambia nikipata muda niende nyumbani kwake. Mume wake alikuwa safarini kwa siku mbili, na alikuwa anataka tu niwe karibu nae eti ili nimpunguzie upweke. Nikiwa kijana mdogo, nilivutiwa na nafasi hiyo, japo moyoni nilijua ni hatari lakini moyo ulikua unatamani tu bila sababu.
Kwanzia hapo, mahusiano yetu ya siri yalianza. Kila mume wake akisafiri alikua akinitafua na kuniambie niende kwake. Tulikua tukishiri mapenzi, na mara nyingine nilikua nalala mpaka asubuhi. Nilikua na hofu moyoni lakini hiyo hofu ilikua ndio kama unaongeza ladha ya penzi hivi kwa muda huo. Alikua ananisifia sana huku akimponda mme wake. Pamoja na mwili aliokua nao, vita vikianza nilikua nahakikisha yeye ndio anachoka balaa. Kwaiyo alikua haishi kunisifu na kunihitaji. Alikua anashawishi sana.

Nilijua kuwa hili jambo ni hatari sana, na haliwezi kuwa endelevu. Kuna siku ilikuwa ni usiku nipo nimelala na yule Mama. Mume wa Mama Cheupe alikuwa amesafiri tena, nami nikaenda nyumbani kwake nifurahi na Mama Cheupe na kulala huo. Tulikaa, tukala na baadaye nikalala pale kama kawaida.
Lakini usiku huo mambo yalibadilika ghafla. Nikiwa nimelala, tulisikia hatua za mtu nje ya nyumba. Mwili wangu ukakosa nguvu, moyo ukadunda kwa kasi. Tulikua tu Mume wa Mama Cheupe alikuwa amerudi ghafla. Na sisi mara moja tulihisi kuna kitu hakiko sawa nje. Aliposogea karibu na mlango, mimi nilichanganyikiwa mno lakini Mama Cheupe alikua makini sana hata kuliko mimi. Nakumbuka alionyesha mlango wa nyuma wa nyumba hiyo ambao ni mbali na ule anaotaka kuingilia Mume wake.
Basi na mimi niliamua kufanya jambo moja tu ambalo ni kukimbia. Kwa haraka niliinuka kitandani, nikavaa viatu vyangu na kwa kasi nikatoka nje kupitia mlango wa nyuma. Ile nimeisha uacha mlango nikakuta mwanga mkubwa wa tochi umenimulika ghafla. Mh nilishtuka sana nikaanza kukimbia lile eneo huku nikiukwepa ule mwanga. Wakati nikifanya hivyo nilisikia kelele za mwizi zikitoka kwa aliekua ananimulika. Nilichanganyikiwa maana ilikua ni sauti ya Mume wake Mama Cheupe na alikua akiita watu.
Nilipiga mbio nikielekea vichochoroni, bila hata kugeuka nyuma mara nyingi. Nilikuwa na hofu ya kufa, nilihisi kama ndio nakufa hivyo maana kwa usiku ule, watu wakiamka watadhani mimi ni mwizi kweli alafu wanaweza niua bila kunisikiliza. Sikuweza hata kupumua vizuri mpaka nilipokuwa mbali na nyumba ya Mama Cheupe.
Nilivyofika ninapolala, sikua nikiamini hata kama nimepona. Nilikaa chini na kufikiria vizuri jambo lililonitokea maana lilikua linaenda kuchukua uhai wangu kabisa na sikua na uwezo wa kubisha kuwa si mwizi kwa usiku ule. Ni bola hilo jambo lingenikuta mchana kuliko usiku.
Siku iliofuata niliongea na Mama Cheupe. Aliniambia Mume wake hakugundua kuwa kuna jambo lolote lilikua likiendelea kati ya mimi na yeye usiku ule. Yani alichojua yeye ni kuwa kulikua na mwizi pale nyumbani na mwizi huyo ndio mimi. Inamaana hata ningekufa usingejulikana ukweli wowote kuhusu mimi. Usiku ungeyafunika yote yaliokua yakiendelea.
Kwanzia siku hiyo niliona japokua usiku unaficha mambo mengi na kuyafanya Matamu, lakini Usiku ni hatari sana. Unawezaje kuwaelewesha watu kuwa wewe sio mwizi wakati wanakuona unakimbia maeneo yao Usiku?🤔
