Jinsi ya kupata Mpenzi mtandaoni (Tafuta mchumba)

Kutafuta mpenzi au wachumba mtandaoni(Online) imekuwa njia maarufu sana katika Maisha ya sasa maana teknolojia imegusa hata kwenye upande huu pia na upande huu unaitwa “Online Dating”. Katika miaka ya hivi karibuni, kuna watu wengi ambao wamepata wake au waume wao wa maisha kupitia mitandao. Yani walianza uhusiano mtandaoni na wakafikia hatua ya kufunga ndoa kabisa.

Lakini pamoja na mafanikio yanayopatikana kwa baadhi ya watu, kuna changamoto nyingi zinazowakabili wale wanaotafuta wapenzi au wachumba mtandaoni. Watu wengi wanazama mtandaoni kutafuta wenza lakini wanajikuta katika mikono ya watu wabaya.

Si kila mtu unayekutana naye mtandaoni anakuwa na nia nzuri. Kuna wale ambao wanadanganya kuhusu utambulisho wao, huku wengine wakiwa na nia ya kujinufaisha tu. Hali hii inaweza kusababisha watu kuogopa kujihusisha na uhusiano wa mtandaoni kwa kuhofia kuvunjwa moyo au kudhulumiwa.

Mbali na changamoto za namna hiyo, Kuna watu ambao wanatamani kujua jinsi gani wanaweza fanya ili kutafuta au kupata Mpenzi mtandaoni lakini hawajui. Kutojua jambo hili vizuri, imekua ni changamoto kubwa kwao.


Hapa katika makala hii tunatoa mwanga juu ya mbo hilo ili kusaidia kila mtu kuelewa vizuri na kuanza kufurahia matunda ya Teknolojia Katika upande huu. Hii ni kwa Wanaume na Wanawake pia.

Namna ya kupata au kutafuta Mpenzi mtandaoni

Njia maalufu Duniani ya kupata au kutafuta wapenzi online ni mtandaoni wa Tinder. Tinder ni mtandao unaowakutanisha watu wanaotafuta wapenzi katika sehemu mbalimbali hapa ulimwenguni. Mtandao unamfanya mtumiaji awe karibu na watu wengine wanaotaka wapenzi uwaliopo karibu.

Kuna mitandao mingi sana hufanya hivi lakini Tinder ni mtandao maalufu sana katika ulimwengu wa kutafuta wapenzi. Tinder ina mamilioni ya watu wanao iamini na kuitumia.


Ukihitaji kutumia Tinder kirahisi, unaweza ipakua App ya Tinder kwenye simu yako kwanza.
Baada ya kuiweka app ya Tinder kwenye simu yako, fuata maelezo yafuatayo;

  • Ifungue na uanze kujisajili.
  • Katika kujisajili utatakiwa kuandika taalifa zako ikiwemo jina, picha zako zaidi ya moja na Namba yako ya simu.
  • Akaunti ikikamilika, utakua na uwezo wa kuanza kuitumia app hii kuona watu wanahitaji wapenzi. Lakini kwenye simu, yako app itakuhitaji uwashe “Location” ili upate kirahisi watu waliokaribu na wewe.
  • Utakua unaziona picha za watu alafu una-Like kwa kubonyeza alama ya moyo kama utampenda mwenye picha hizo. Ikiwa na yeye ata-Like zako, mnaweza anza mazungumzo.
App ya Tinder


Jambo la muhimu kujua hapa ni kwamba App hii inaonekana kama kuitumia ni Bure hivi ila sio bure. Ili kuifurahia bila vikwazo, unatakiwa kulipia na unaweza lipia hata kwa wiki tu. Ukilipia unapata uhuru zaidi katika kutafuta mpenzi na kuchati na watu. Na katika kuitumia Bado umakini unahitajika maana unaweza kutana na watu wabaya wakakuingiza mjini.

Njia nyingine rahisi za Bure za kutafuta wapenzi Online

Mbali na mitandao kama Tinder, unaweza itumia mitandao ya kijamii hii tulioizoea. Facebook au WhatsApp inaweza kuwa katika ya mitandao unayaweza kutana na watu lakini pia unaweza jipatia mwenza kupitia kwenye magroup ya mahusiano au mijadala mbalimbali. Kama ni mtumiaji wa WhatsApp, unaweza fuata hatua zifuatazo kutafuta mpenzi mtandaoni kirahisi;

  • Fuatilia magroup ya WhatsApp yanayokusanya watu wa mtaani kwako, mkoa wako, kazini, kanisani au shule yako alafu ujiunge nayo.
  • Ukijiunga, kwenye group hizo utakua karibu na watu wanaoweza kukujua au vutiwa na wewe. Kuwa mtu unae chati ili watambue uwepo wako kwenye group.
  • Jaribu kujenga mahusiano na watu unaovutiwa nao kwenye group hizo alafu kuzeni uhusiano huo mpaka muanze kuchati inbox alafu muwe wapenzi.

Mambo ya kujua unapotaka kumtongoza mwanamke Mtandaoni BONYEZA HAPA>>>

Njia hii ni njia nyepesi sana ya kupata Mpenzi mtandaoni. Na naweza kusema ni njia salama zaidi maana unakutana wa watu halisi waliokaribu na wewe. Hata kama hauwajui vizuri, Bado ni ninja rahisi kwakua mnaweza kukutana kirahisi kutokana na ukaribu. Lakini endapo utajiunga kwenye group za watu wasiokaribu na wewe na hamjuani kabisa, inaweza kuwa rahisi kuibiwa au kutapeliwa.

Pamoja na changamoto nyingi, bado kuna nafasi ya kupata mapenzi ya kweli mtandaoni(kwenye internet). Kufanikiwa kunategemea jinsi unawasiliana, uvumilivu, na uwezo wa kuchunguza vizuri kuhusu mtu unaemuhitaji. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Leave a comment