Kama tunavyofahamu, AI au Akili bandia ni teknolojia inayowezesha mashine kufanya kazi zinazohitaji akili za kibinadamu, kama vile kutambua picha, kuelewa lugha, na hata uundaji wa content (maudhui). Hivi sasa, unaweza kutumia AI kutengeneza Video kwa kutumia picha flani au kuelezea video unayohitaji kwa maandishi pekee.
Yani kama unapicha unayotamani iwe ni video, AI inaweza fanya hivyo kwaajili yako. Na pia uweza kuipa maelezo kuhusu video unayohitaji kwa maandishi tu na ikakuundia hiyo.
Kuna huduma nyingi kwasasa zinawawezesha watu kutengeneza video kwa kutumia AI na video hizo zimesambaa sana mtandaoni. Kama ni mtu wa mitandao, unaweza kuwa tayari umewahi kuona video nzuri na ukaambiwa imetengenezwa na AI.
Kwa sasa Ulimwengu wa video za mitandaoni umekua ukihusisha sana AI katika kutengeneza video. Watu wanaotengeneza video katika YouTube, TikTok, Instagram na hata Facebook wamekua wanatumia sana AI kipindi hiki.
Sababu kubwa ya watu kutumia AI katika kutengeneza Video ni kuokoa muda na gharama pia. Mtu unaweza tumia AI ndani ya dakika 1 kutengeneza Video ambayo ingechukua pesa nyingi au siku nyingi.
Mfano; kwa kawaida ukihitaji video inayoonesha uwanja wa ndege na ndege zinavyoruka angani, utatakiwa kuingia gharama za kupata kamera, kupata kibali cha kuchukua video sehemu flani katika uwanja wa ndege. Hii inaweza kukuchukua siku kadhaa ili kukamilisha wazo zima la video yako.
Lakini kupitia AI, unaweza tengeneza Video hiyo ya uwanja wa ndege kwa dakika moja tu kwa kutumia hata simu ya mkononi.
Kwaiyo, AI Inafanya kuokoa muda, kupunguza gharama za uzalishaji wa Video, na kutoa fursa za ubunifu pia.
AI za kutengeneza picha kwa maneno BONYEZA HAPA>>>
Jinsi ya kutengeneza Video kwa maneno au picha kwa kutumia AI
Huduma za AI zinazowezesha watu kutengeneza video kwa AI zipo nyingi sana mtandaoni kwa sasa na zipo tofauti. Ukihitaji kutengeneza video kwa AI unatakiwa kwanza kuchangua huduma utakayotumia kufanya hivyo. Kwa hapa The bestgalaxy, tunakuelekeza Jinsi ya kutengeneza Video kwa kutumia KLING AI.
KLING AI imetengenezwa na kumpuni ya kichina iitwatwayo Kuaishou Technology. Imekua ikitumika kutengeneza video zinazo trend ikiwemo ile ambayo mahindi yanageuka kuwa samaki(kama umewahi ona unaweza nielewa).
KLING AI inawawezesha Watumiaji wake kuunda Video wanazozihitaji kwa kuweka picha au maelezo ya maandishi tu. Yani ukiipatia Picha ya watu wanaocheza Mpira, itakupa video ya watu waliopo kwenye picha wakicheza mpira. Na ukiipa maelezo ya maandishi yanayahusu kutengeneza “video ya watu wakicheza mpira” itakupatia video ya watu wakicheza mpira kama ulivyoeleza. Lakini lugha ya kiingereza ni Lugha unayotakiwa kuitumia ili kupata matokeo mazuri.
Huduma hii hutoa nafasi kidogo kwa watu kuitumia Bure kila siku lakini ukihitaji uhuru zaidi, utahitajika kulipia. Unataka kuijaribu KLING AI? Fuata hatua zifuatazo kuanza kutengeneza Video kwa maneno au picha na KLING AI bure kabisa.
- Ingia katika Tuvuti ya KLING AI
- Tengeneza Akaunti
Akaunti ikikamilika, Chagua “AI videos” katika ukurasa wa kwanza. - Baada ya kufanya hayo, utaletwa kwenye ukurasa wenye upande ulioandikwa “Text to Video” na upande “Image to Video”
- Upande ulioandikwa “Text to Video” utakua ukiutumia kutengeneza Video kwa kutoa maelezo ya maandishi ya video unayohitaji.
- Upande ulioandikwa “Image to Video” utakua ukiutumia kuweka Picha unayohitaji ibadilishwe kuwa video(kubadili picha kuwa video). Mbali na picha, unaweza ongezea na maelezo ya maandishi katika sehemu hii ili Video inayotoka iwe ni video unayohitaji.

Mbali na KLING AI, kuna AI nyingi mno ambazo watu hutumia kutengeneza video ikiwemo Midjourney(unalipia kuitumia). Tutakua tukizungumzia AI hizi na nyingine nyingi kwenye makala nyingine, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.
One thought on “AI: Kutengeneza Video kwa maneno au picha”