Mambo yasiofaa kuwaambia Rafiki zako kuhusu Mpenzi wako

Katika Urafiki na Mahusiano ya kimapenzi, ni muhimu sana kujua mipaka ya mazungumzo na jinsi ya kuhifadhi baadhi ya mambo. Kuna wakati urafiki unaweza kuwa na umuhimu mkubwa katika kupeana mawazo lakini si kila kitu kinachohusiana na mpenzi wako kinapaswa kuwa sehemu ya mazungumzo na marafiki. Urafiki na mahusiano ya mapenzi, yote ni mahusiano lakini katika baadhi ya mambo, unatakiwa kutenganisha kabisa.

Kuna baadhi ya watu hupuuza kutenganisha mahusiano haya na mwisho wa siku hujikuta wanagombana na rafiki zao au wapenzi wao. Usipoweka mipaka katikati ya mahusiano haya, kunakua na asilimia kubwa ya kuingia kwenye ugomvi na marafiki au mpenzi wako. Na hakuana anaetaka jambo hilo litokee katika Maisha yake. Wengi tunapenda tuwe na amani na wapenzi wetu, na vile vile kwa marafiki zetu.

Kujua ni nini cha kusema na nini cha kuhifadhi ni Jambo muhimu katika kudumisha uhusiano na Marafiki zako huku ukiwa na uhusiano mzuri wa kimapenzi na wenza wako. Kuna baadhi ya mambo ukiepuka kuwaambia marafiki zako kuhusu Mpenzi wako, utakuwa unalinda sio tu heshima ya mpenzi wako bali pia uhusiano wako na watu wa karibu.

Kuchepuka kuna faida lakini hizi ni hasara zake BONYEZA HAPA>>>

Mambo yasiofaa kuwaambia Rafiki zako kuhusu Mpenzi wako

Mipango yenu ya baadae

Kama mmeongea mipango mingi na mpenzi wako, hakikisha unakua makini katika mazungumzo yako na marafiki ili usitoe mambo yote muliopanga. Inaweza kuwa ngumu kuwaficha marafiki zako kuhusu mambo mazuri muliopanga na mpenzi wako lakini ni vema kuwa hivyo ili kulinda mahusiano yako.
Marafiki wengi sana wanaweza kukuzunguka lakini sio kila Rafiki anaweza kuwa anania njema na mahusiano yenu. Na mtu asie na nia njema akiambiwa mipango yenu, inaweza kuwa rahisi sana kuharibu mahusiano yenu.

Ubaya wa mpenzi wako kimwili au kitabia

Hapa Duniani, wote tuna mabaya yetu na mazuri yetu. Inaweza kuwa sio ajabu kuona mabaya ya mpenzi wako kimwili au kitabia. Lakini mambo hayo hayatakiwi kuwa katika maongezi na rafiki zako. Kama kuna jambo lolote baya kuhusu mwenza wako na umeweza kulivumilia, basi fanya kumfichia Siri.


Unapotoa mabaya ya mpenzi wako kwa rafiki zako, kuna namna wote mnaweza shushwa thamani na watu wengine pindi mambo hayo yakisambaa. Yani unakua umeandika sifa mbaya kwa mdomo wako mwenyewe. Na kama umeshindwa tunza Siri ya mpenzi wako mwenyewe, usije walaumu watu wakiendelea kupeana Siri hiyo.

Matukio yake mabaya

Katika Maisha ya mahusiano kunaweza kuwa na matuko mabaya au ya aibu kuhusu Mpenzi wako ambayo umeyajua kwa kusimuliwa nae au kuyashuhudia. Mambo hayo ukiyaongelea kwa mtu mwingine zaidi yenu, jua kabisa kuna asilimia kubwa ya kuendelea kusambaza na kuwachafua wote.
Liwe ni tukio la kitandani au Maishani mwake, epuka kuliweka kuwa sehemu ya mazungumzo na marafiki zako.

Hali ya mpenzi wako kipesa Pesa

Mambo ya Pesa katika mahusiano yenu ni mambo yanayowahusu nyie na sio marafiki. Mpenzi wako akiwa na Hela au hana Hela, isiwe ni jambo la kuzungumza na marafiki zako. Mambo ya pesa husukuma watu wenye tamaa kufanya vitu vingi sana katika Maisha. Hapa Duniani kuna hata ndugu ambao hugeukana kisa pesa. Nadhani hata wewe umewahi sikia simulizi nyingine mbaya kama hizi zilizohushisha pesa.


Swala Mpenzi wako na Pesa linaweza kuwa jambo zuri kuliongelea lakini si vema kuliweka katika mazungumzo yenu ili kulinda urafiki wenu na vile vile kulinda mahusiano yako.

Ni hayo tu lakini kabla haujafika katika kituo cha mwisho wa makala hii, fahamu kuwa mambo tuliozungumza hapa hayatakiwi kukuzuia kuomba ushauri. Unaweza kuomba ushauri kwa rafiki zako unaowaamini Pele unapoona masaada kama huo unahitajika. Lakini kuwa makini sana na unachokiongea.

Leave a comment