SMS za kumchekesha mpenzi wako

Kumfurahisha mwanamke au mwanaume wako ni moja ya njia bora za kudumisha upendo na furaha katika mahusiano. Kutuma ujumbe mfupi wa kumchekesha ni njia rahisi na ya kupendeza ya kumfanya mpenzi wako afurahi. Ujumbe huu unaweza kumfanya atabasamu bila kutarajia, hata kama ana siku ngumu au anapitia changamoto fulani.

Katika makala hii, tumekusanya orodha ya SMS za kuchekesha ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako ili kuleta tabasamu la bila kutarajia usoni mwake. Ujumbe huu si tu utaimarisha uhusiano wenu, bali pia utaleta ladha na ucheshi ambayo watu wengi huipenda katika mahusiano. Kumfurahisha mpenzi wako kwa njia ya kumtumia sms za ucheshi, kunaweza weka hata ugumu kwa mpenzi wako kusahau.

Kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye orodha, fahamu kuwa jambo hili linatakiwa kufanywa kwa kiasi tu. Usizidishe utani au vichekesho kwenye mahusiano ya mapenzi. Unatakiwa kujua wakati gani unafaa kufanya utani au vichekesho kwa mpenzi wako.

Soma Simulizi ya Sukari Ya Dada BONYEZA HAPA>>>

SMS za kumchekesha mpenzi wako (Mwanamke au Mwanaume)

  • Tangu uliponiambia “Nakupenda”, nahisi kama Dunia yote hii ni yangu mimi na wewe alafu Hawa wengine wapangaji wetu😂
  • Kitoto kidogo kilimwambia baba yake “Baba ivi wewe umezaliwa wapi?” Baba akajibu “Nimezaliwa Mbeya”. Mtoto akasema “Mama nae kazaliwa Mbeya?” Baba akajibu “Hapana, amezaliwa Tanga”. Mtoto akauliza “Na Mimi jee?” Baba akajibu “Dar”. Mtoto akasema “Mh Sasa tulikutanaje????” Baba cheko😂😂
  • Kabla sijakwambia “Nakupenda” nilikua nikijaribu mara nyingi sana kutaka kukuambia. Lakini kila nilipotaka kukuambia, nilikua nasahau maneno yote kama mtoto aliesahau alichotumwa dukani😂😂
  • Wewe kwangu ni kama WiFi tu. Ukinisogelea mtandao unapanda “Pap!”😂
  • Nikiamka asubuhi huwa nakuangalia wewe hapo kama umeamka salama na bado unanipenda. Yani kiufupi nakuangalia moyo wangu kama unadunda😂😂
  • Kuna mtoto wa mtu nampenda hapa mpaka nahisi nimelogwa. Au nikuulize wewe mwenyewe vizuri tu, ulienda kwa mganga gani kuniloga?😂😂
  • Watu watatu washamba walisafiri, walipofika kwa ndugu yao mjini wakapewa soda wakasemezana kuwa “Ni tamu sana”. Walipokua wakiondoka, mmoja alitia kizibo cha kisoda kwa siri kwenye mfuko. Baadae walipotoka nje akamnong’oneza mwenzie “Mwenzio nimechukua mbegu nikapande”😂😂.
  • Usiku nimeota nipo na wewe umenikiss alafu umeniambia chukua hii laki 5 kama zawadi. Nilivyoona unanipa hela nikashtuka 😂😂
  • Nilipokuona mara ya kwanza nilirudi nyumbani salama ila moyo ndio sikurudi nao. We mwizi uliniibia moyo mpaka nikakupa mazima😂
  • Jana nilipanga Leo nikupe 50,000 kama zawadi. Lakini mapenzi upofu mpenzi wangu, hapa pesa yenyewe hata siioni, nakuona wewe tu😂
  • Najua wivu ni mbaya kwenye mapenzi ila utanisame tu. Yani tangu niione, natamani kuifunga hiyo kitu nifaidi mimi tu😂
  • Mtu akituangalia tunakua kama watu wa heshima. Kumbe kuna muda mimi na wewe baby wangu tuna ruka ruka kama Spider-Man😂😂
  • Niliwaza kuanza kukupa Tsh 5000 Kila ukitabasamu maana unaupa Raha moyo wangu. Lakini nikaona nitafirisika maana unatabasamu kila mara na kunipa Raha hatari😂😂
  • Malaika wenzako wapo kupeperuka angani huko, wewe nimekukamata kimapenzi huku😂
  • Kwajinsi ninavyokupenda, ukiniacha nitajiribu kukuloga mpenzi wangu sikufichi😂
  • Nikifanikiwa kuwa Raisi wa nchi, utapenda nikupe Mkoa gani kama zawadi we mwanaume?😂😂
  • Kuna mlevi alikamatwa akikojoa eneo la Shule na Mwalimu mkuu akaulizwa “Hilo bango hapo limeandikwaje?” Mlevi akamjibu ‘Limeandikwa USIKOJOE HAPA’ Mwalimu akajibu “Kwahiyo umefanya nini hapo? Unataka nikupeleke polisi?” Mlevi kwa makini na upole akajibu “HAKI YA MUNGU NILIKUA NAJUA NDIO JINA LA SHULE!” 😂😂
  • Kwa jinsi ninavyo kupenda na ulivyo muhimu kwangu, Usije waza mimi kukuacha wewe. Kwani wewe unaweza kuacha kupumua?😂
  • Unanifanya nijione mwenyewe bahati kuwa na wewe mpaka natamani ni nimshukuru Ex wangu kwa kuachana na mimi😂
  • Umeshawahi kutembea bila viatu kwe barabara ya kokoto? Hiyo ndiyo hali ya moyo wangu bila wewe😂
  • Hebu fanya kuziba pua na mdomo kwa muda wa dakika 10 hivi. Hivyo ndio huwa nahisi nisipokuona au kuisikia sauti yako kwa muda My love😂
  • Kila ukijubu SMS moyo wangu kwa furaha unalia “Pah!” Umeniloga eti?😂😂
  • Hebu jibu sms haraka kabla sijakufuata. Yani nikikumiss kama hivi, Naweza hata kupaa nitue hapo😂

Katika huu mwisho wa orodha yetu, napenda kukukumbusha kuchagua wakati mzuri wa kumtania au kumchekesha mpenzi wako kwa SMS. Wakati mzuri ni ule muda ambao unahisi mpenzi wako anaweza soma SMS zako na kucheka. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine mazuri zaidi.

Michezo ya kuchati na Mpenzi wako kurefusha maongezi BONYEZA HAPA>>>

Leave a comment