Kutengeneza pesa ukiwa kama Mwanamuziki ni ndoto ya watu wengi. Ndoto hii inaweza kuwa inaonekana ni ngumu kuitimiza lakini kwa kiasi flani mitandao au internet, imewawezesha wanamuziki wengi kutimiza ndoto zao. Kuna njia nyingi sana zinaweza muingizia pesa Mwanamuziki katika Internet kwasasa.
Mbali na kuingiza pesa, internet au mtandao, umekua na mchango mkubwa sana katika muziki. Zamani mtu akiwa anataka kusambaza muziki wake alilazimika kutumia nguvu na gharama kubwa kuusambaza muziki ukiwa kwenye vifaa kama CD au Tape. Lakini hivi sasa, Mwanamuziki anaweza sambaza Muziki wake mtandaoni ukawafikia watu wengi kwa muda mfupi bila kutumia nguvu kubwa.
Nafikiri hata wewe umeisha wahisikia nyimbo nyingi za wasani wa hivi sasa hufikia mamilioni ya wasikilizaji ndani ya masaa 24 tu. Jambo la nyimbo kuwafikia mamilioni ya watu katika masaa 24 lilikua ni jambo ngumu sana hapo zamani.
Kiufupi ni kwamba, nyakati hizi zimefungua njia nyingi za wasani wa muziki kuonesha kazi zao kwa watu na kutengeneza pesa. Hapa The bestgalaxy tunaenda kukupa njia za kutengeneza pesa mtandaoni ukiwa kama Mwanamuziki Muimbaji. Hii inaweza kuwa na msaada sana kama utakua ni mwimbaji uliedhamilia kutengeneza pesa online (mtandaoni).
Njia za kutengeneza pesa mtandaoni ukiwa Mwanamuziki (Muimbaji)
Kulipwa na platform za kusikilizia muziki
Kuweka nyimbo zako ulizoimba katika platform za kusikilizia muziki kama YouTube, Spotify na Boomplay, kunaweza kuingizia pesa pindi utakapo pata wasikilizaji wengi. Hii ni njia ya kisasa ya kuuza muziki katika kipindi hiki na wasanii wengi wakubwa wanaitumia kupata mamilioni ya pesa inazowawezesha kuishi maisha ya ndoto zao.
Mara nyingi, pesa unayopata katika platform hizi huathiliwa na mambo kama idadi ya wasikilizaji na nchi wanayotoka. Lakini unapoanza ni vema ukaweka mbali kidogo maswala ya pesa alafu ukatumia platform hizi kujenga Brand tu.
Kutangaza biashara za watu katika kurasa
Ukiwa mwimbaji mzuri unaefuatiliwa na watu mpaka katika kurasa za mitandao ya kijamii, unaweza tumia kurasa hizo kutengeneza pesa. Watu au wafanya biashara wanaweza kuwa wanakulipa ili kutangaza biashara zao katika kurasa zako. Ukiwafanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa, unaweza wavutia watu wengi wakafanya deals zitakazokufanya uione thamani ya kufanya Muziki wako.
Kuimba ukiwa LIVE kwenye platform zenye zawadi
Kuna Platform zinazomruhusu mtu kuwa LIVE kupitia kamera ya simu au vifaa vingine alafu watu wanakua wanamuangalia anachofanya na kumpa zawadi wakipenda(Mfano: TikTok). Ukiwa kama Muimbaji, unaweza kutumia “LIVE” kama sehemu ya kufanyia performance za nyimbo zako. Watu wengi wapo kwenye mitandao kama TikTok wanaingia LIVE na kuimba nyimbo zao zinazogusa mioyo ya watu mpaka wanatoa zawadi.
Zawadi hizi zinaweza kuwa ni pesa nyingi sana kama watu wanaokuangalia watakua wanakuunga mkono kwa unachofanya.
Kutumia muziki kuonesha huduma zako nyingine mtandaoni
Kuna huduma yoyote unayoitoa na inaweza kupa pesa mbali na Muziki? Kama unayo, Muziki wako ukifanikiwa kufanya vizuri mtandaoni basi tumia shughuri zako za kimuziki kutangaza huduma hiyo mtandaoni. Ukichanganya vitu hivyo vizuri, unaweza nufaika na Muziki wako kuliko kitu chochote kwenye muziki. Watu wengi waliofanya hivi na kufanikiwa, huielewa nguvu yao na kueshimu sana muziki.
Wakati ukiendelea kuyafikilia hayo yote tulioyaweka hapa juu, ni vema ukajua kuwa kila njia iliopo hapa, inakuhitaji upambane kidogo maana sio rahisi japo inawezekana. Ila ukifanikiwa unaweza kuwa unaetengeneza mamilioni ya pesa kwa mwezi huku ukiishi maisha ya ndoto zako.