Kuna nyakati ambazo marafiki wanaweza kuhitaji msaada wako wanapopitia changamoto katika mahusiano yao ya kimapenzi. Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba si kila mara unapaswa kutoa ushauri. Wakati mwingine, jambo bora zaidi unaloweza kufanya ni kumsikiliza tu rafiki yako bila kutoa maoni au mapendekezo yasiyoombwa. Na hata ukihitajitajika kutoa ushauri, unatakiwa kufikilia sana kabla ya kutoa.
Mahusiano ya mapenzi ni jambo binafsi na yana mambo mengi ambayo kila mtu anaweza kuwa na njia yake ya kushughulikia matatizo au kuchukua maamuzi. Unaweza kuwa na nia njema ya kutoa ushauri kwa mtu kuhusu mahusiano yake lakini baadae ukaonekana unania mbaya au ukagundua umewapeleka sehemu mbaya.
Kama umeletewa jambo na rafiki yako kuhusu mahusiano yake, hakikisha unalichimba kwa kina jambo hilo kabla hauja litolea ushauri. Baadhi ya mambo ambayo ambayo ukiletewa hautakiwi kukurupuka kuyatolea ushauri ni yafuatayo:
Dalili za Ex wako kukupenda BONYEZA HAPA>>>
Mambo hautakiwi kukurupuka kumshauri rafiki kuhusu mahusiano
Kuachana na mpenzi wake
Mahusiano ya mapenzi yanaweza pelekea rafiki yako kutaka ushauri ambao unahusiana na kuachana na ampendae. Kabla hauja mshauri lolote juu ya kuachana kwao, fahamu kuwa kugombana au kuyumba kwa mahusiano kunaweza kuwa sio mwisho wa mahusiano.
Watu wengi hugombana na kutoelewana kwenye mahusiano lakini baadae hutulia na kuwa sawa.
Sasa ushauri wako kwa wapenzi waliogombana ni vema ukawa ni ushauri wa kujenga mahusiano au kuwasaidia kurejesha amani kati yao. Ikishindikana kabisa au kukiwa na sababu ya msingi sana ndio unaweza washauri kuachana kama wanavyohitaji kufanya.
Hatua juu ya ujauzito wasio utarajia
Swala la kuzuia mimba zisizotarajiwa ni jambo la muhimu sana kushaurina na kuliongelea hata na marafiki. Lakini Swala la hatua za kuchukua juu ya ujauzito uliotokea bila kutarajiwa ni swala linanowahusu zaidi wapenzi na sio marafiki.
Kuna watu wengi hupata ujauzito katika hali ya kutotarajia, huzaa watoto na watoto hao huwa baraka ambayo hawakutarajia katika Maisha yao. Kwaiyo unapoletewa swala na rafiki kuhusu ujauzito ambao hawakutarajia ni vema ukawa upande chanya zaidi. Na kama utakua na ushauri hasi, basi kuwe na Sababu ya msingi sana.
Kutafuta ubaya wa mpenzi wake
Unaweza taka kumshauri rafiki yako kuhusu kuutafuta ubaya wa mpenzi wake lakini fahamu kuwa jambo hili sio la kurupuka. Anaweza kua hata anakuhusisha kabisa kumchunguza mpenzi wake lakini hautakiwi kuwa mstari wa mbele kwenye jambo hilo.
Kama rafiki anamchunguza sana mpenzi wake kwa kuutafuta ubaya au uzuri wake, hata akikwambia “yule mpenzi wangu nipo nae tu ila simpendi”, jua ni anampenda. Ni ngumu kumchunguza mtu usiempenda hapa Duniani.
Rafiki akiwa anasema hampendi sana mpenzi wake alafu anataka kufuatilia mambo ya huyo mpenzi (kama vile, sms au michepuko alionayo) jua tu ni anampenda ila naficha maumivu.
Kuwa na tahadhari unapotaka kushirikiana nae au kueleza mambo mabaya kuhusu mwenza wa rafiki yako. Ukikulupuka unaweza kuzua chuki au mgogoro zaidi.
Mwisho, ni muhimu kujua kwamba kila mtu ana njia yake ya kutatua changamoto za kimapenzi. Kuomba au kutoa ushauri ni jambo zuri pia lakini kwenye baadhi ya mambo, ushauri unatakiwa kutolewa bila kukurupuka.
Kuchepuka Kuna faida ila hizi ni hasara zake BONYEZA HAPA>>>