Kuchati na mpenzi kwenye simu ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano na kujenga hisia za ukaribu kati yenu. Katika ukurasa huu, The bestgalaxy inaenda kukupa michezo michache ambayo mnaweza kucheza pamoja katika kuchati na Mpenzi. Michezo hii itasaidia kurefusha maongezi, kuburudisha na kuongeza furaha katika uhusiano wenu.
Kuna muda wapenzi mnaweza kosa kabisa mambo ya kuchati na hii hutokea mara nyingi. Lakini kama mmoja kati yenu atakua anauelewa juu ya michezo ya kuchati, mnaweza ianzisha na kufanya maongezi yaendele katika kuchati kwenu. Michezo hii ya kuchati ni mbinu nzuri ya kufanya maongezi yaendele katika kuchati kwa wapenzi. Kwa kiingereza michezo hii inaitwa “Texting Games” na ipo mingi sana japo hapa tutaangalia michezo michache tu.
Michezo hii michache ni rahisi na inahitaji muda mchache kumuelewesha mpenzi wako kama haijui unapotaka mcheze. Haina haja ya kuwa na vifaa maalum au kuwa pamoja kimwili ili kueleweshana. Endelea kusoma ili kuijuia na kuielewa michezo hii ya kuchati.
Jinsi ya kum-surprise au kumshangza mpenzi wako bila kutumia Pesa BONYEZA HAPA>>>
Michezo ya kuchati na Mpenzi wako wa kiume au wakike
Kwasababu nakupenda
Mchezo huu unachezwa na wapenzi ambao mnapendana alafu mmetulia mnachati kwa sms. Wapenzi mnatakiwa kuwa mnatumiana sms zenye ujumbe unaojumuisha maneno “Kwasababu nakupenda”.
Kwamfano; unaweza mwambia mpenzi wako “Nimekupa moyo wangu wote kwasababu nakupenda”. Huu ni mfano tu lakini mnatakiwa kutumiana sms za muundo huo zinazogusa mioyo yenu na kuelezea hisia zenu. Mchezo wa “Kwasababu nakupenda” unaweza kuwafurahisha na vilevile mtakua mnajenga mahusiano yenu kwa kuambiana mambo mazuri mnayoweza kufanya,mlio yafanya na mnayotaka kufanya Kwasababu ya upendo.
Maliza au taja wimbo
Mchezo mwingine ni huu unaitwa “Maliza au Taja wimbo”. Wapenzi katika mchezo huu mnakua manatajiana mistari ya nyimbo za mapenzi alafu kila anaetajiwa atatakiwa kumalizia mstari au kutaja jina la nyimbo aliotajiwa.
Kutuma mistari mitamu ya kisisimua, kutamfurahisha zaidi mpenzi unaechati nae kwenye mchezo huu.
Kwenye mchezo huu mnatakiwa kuwa ni watu mnaosikiliza na kufuatilia nyimbo za mapenzi. Kama ni watu wa namna hiyo, basi mnaweza furahia zaidi mchezo.
Jinsi ya kulinda Ndoto zako Maishani zisife BONYEZA HAPA>>
Kisia nilipo
Mchezo huu unachezwa na wapenzi na wanaucheza kwa kukisia mazingira ambayo wapo. Yani unaweza anza kwa kukisia sehemu alipo, anachokifanya na hata vitu vilivyo mzunguka. Yeye atakua anakwambia kama umekosea au umepatia.
Mtakua mnapokezana pale mmoja wenu anapopatia kukisia. Mchezo huu wa kukisia unakua mzuri zaidi kama watu wote ni wakweli alafu mnapendana kiasi cha kuweza kuumiza kichwa kufikilia na sio kutaja tu mnachojiskia. Kila mchezaji anatakiwa kufikilia jibu kulingana na anavyomjua mwenza wake.
Nishawishi tulale
Katika michezo, mchezo mzuri sana wa mapenzi katika kuchati ni huu. Mchezo wa “Nishawishi tulale” ni mchezo unachezwa wakati wa usiku unapochati na mpenzi.
Unachezwa kwa kuahidiana kuwa hamtalala na mtachati pamoja mpaka asubuhi. Kama mmoja anataka kulala kabla ya asubuhi, tatatakiwa kumshawishi mweza wake walale kwa kufanya au kumwambia jambo lolote litakalomshawishi mwenza wake.
Mtu anaetaka kulala aweza ahidi zawadi, akatoa maneno mtamu au jambo lolote litakalo mfanya mpenzi asietaka kulala, alale. Wachezaji wote mnatakiwa kujali sheria za mchezo na kutimiza ahadi zenu.
Mpelelezi
Machezo wa “Mpelelezi” ni mchezo wa kuchati ambao unahusu kuulizana maswali. Wapenzi mnakua mnapeana maswali kwa kupokezana na kila swali linatakiwa kujibiwa.
Idadi ya maswali inaweza kuwa 5 kwa kila mtu na hata 20 mkipenda. Kikubwa hapa ni kuulizana maswali mazuri yatakayo wafurahisha wote wawili.
Mchezo huu wa kuchati unaweza fanya watu mnaopendana mjuane zaidi ya mnavyojuana kwenye mambo mbalimbali. Ukipata nafasi ya kucheza mchezo huu, kuuliza maswali ya kusisimua na kujenga mahusiano yenu ni muhimu sana.
Michezo yote hii tulioiweka hapa ni rahisi sana kumfurahisha mpenzi wako wa mwanamke au mwanaume. Na huwa inafaida kubwa kwenye kujenga umahusiano ya wapenzi wanapenda kuchati. Unaweza ucheza na mume wako, mke wako bila tatizo lolote. Unaweza pia mtumia mwenza wako makala hii ili kuokoa muda wa kumulelezae ingawa ni vizuri kumuelekeza mwenyewe.
Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy!