Kubadilisha namba ya WhatsApp inaweza kuonekana kama kazi ngumu na yenye kuleta wasiwasi wa kupoteza mazungumzo yako muhimu, picha, video, groups na vitu vingine. Lakini, ukifuata hatua sahihi, unaweza kufanya mabadiliko ya namba kwa urahisi bila kupoteza chochote. Ni muhimu kwa kila mtumiaji wa WhatsApp kujua njia sahihi ya kubadili namba ili kuepuka kupoteza vitu muhumu.
Wapo watu ambao hubadilisha namba bila kutumia njia sahihi na huishia kupoteza vitu muhumu. Kwa kuliona hilo The bestgalaxy, tumeamua kuwasaidia watu hawa na watu wengine wasio jua njia sahihi.
Katika makala hii, tunakupa hatua za jinsi ya kubadilisha namba yako ya WhatsApp bila kupoteza data yako(Android). Kama hajui kuhusu hili na unataka kubadilisha namba, hapa utapata mwongozo wa kufanikisha unachohitaji. Lengo ni kuhakikisha unafanya mabadiliko haya kwa usalama, huku ukiendelea kufurahia matumizi yako ya WhatsApp.
Jinsi ya kuchati alieku-block WhatsApp BONYEZA HAPA>>>
Jinsi ya kubadilisha Namba ya WhatsApp bila kupoteza Vitu (Android)
Kwanza unatakiwa kujua kuwa Akaunti yako ya WhatsApp na namba yako ya simu ni vitu viwili tofauti. Unapotumia WhatsApp inamaana una Akaunti ya WhatsApp iliofungukiwa kwa namba ya simu. Na namba ya simu inaweza badilishwa bila kubadilisha akaunti yako ya WhatsApp. Hii itakufanya usipoteze vitu vyako(Chats, Groups, na vingine). Kufanya hivi, fuata hatua zifuatazo;
- Ingia kwenye WhatsApp na ubonyeze Vidoti vitatu vilivyopembeni juu.
- Chagua “Settings” kwenye orodha ya chaguzi utazoziona.
- Chagua “Account” kwenye chaguzi zitazokuja tena Kisha bonyeza “Change number”.
- Bonyeza kitufe kilichoandikwa “Next” Kisha andika namba mpya na namba ya zamani kwenye ukurasa utaoletewa.
- Baada ya kuandika namba kwa usahihi utatakiwa kubonyeza “Next” ili kuendelea na uthibitisho namba hizo. Utatakiwa kuthibitisha namba hizo kwa kupokea code watakazozituma. Ukiweza kuthibitisha, WhatsApp wataweza kubadilisha Namba yako na kama utashindwa kuthibitisha, hautaweza kubadili namba.

Uzuri wa kubadilisha Namba kwa njia hii ni kwamba, Rafiki zako na watu wengine ulioungana nao kwenye WhatsApp watajulishwa. Wataambiwa kuwa umebahatisha namba alafu watapewa na namba yako mpya ya WhatsApp.
Epuka kufanya mabadiliko kama haya kama hutumii WhatsApp rasimi.