Wanasema mwaka mpya huja na mambo mapya. Unapoanza mwaka, watu wengi hujiwekea malengo wanayotaka kutimiza ndani ya mwaka huo. Jambo hili huwa linafanywa na watu wengi sana Duniani lakini kufikia malengo hayo mara nyingi inakua sio rahisi kama wanavyotarajia. Katika mambo mapya mwaka mpya unayokujanayo huwa unajumuisha na changamoto mpya zinazoweza kuweka ugumu kutimiza malengo.
Lakini Swala la watu kushindwa kutimiza malengo ya mwaka, lisiwe chanzo cha kushindwa kuipamga au kuendelea kuipambania mipango yako ya mwaka. Jambo hili linatakiwa kuwa ni chanzo cha kuweka umakini katika mipango ya mwaka na kuhakikisha unapambana sana kuiitimiza.
Ni muhimu kuwa na mbinu sahihi za kuhakikisha kwamba malengo yako ya mwaka hayabaki kuwa ndoto tu, bali yanakuwa uhalisia. Katika kurasa hii ya The bestgalaxy, tutajikita kwenye mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kutimiza malengo yako ya mwaka. Mbinu hizi zimewekwa hapa ili kukupa mwanga utakaokisaidia katika safari yako ya kufikia mafanikio unayoitaka kuyapata ndani ya mwaka. Kila mbinu itakusaidia kuweka malengo yako kwenye mstari sahihi kama utaitumia kwenye safari yako.
Jinsi ya kuzilinda ndoto zako Maishani zisife BONYEZA HAPA>>>
Mbinu za kutimiza Malengo yako ya Mwaka
Kuandika mipango yako na hatua
Watu wachache sana wanauwezo wa kukamilisha mipango ya muda mrefu bila kuandika. Wengi wasio andika huwa na malengo yanayo badilika badilika mpaka mwaka unaisha hawajui jambo gani walilopanga mwanzo wa mwaka.
Kitendo cha kuandika malengo yako huwa kinasaidia kutosahau kirahisi ulichokusudia kukifanya katika mwaka. Na hata ukisahau unaweza kumbuka picha nzima ya lengo lako kwa kusoma ulipoandika.
Ukishaandika hakikisha unakua na tabia ya kuandika mambo yako kwenye kila hatua unayopiga. Jambo hili litakusaidia kutimiza malengo yako ya Mwaka na hata usipotimiza utakua na mambo ya muhimu sana ulioyaandika kwaajili ya maisha yako ya Mwaka mwingine.
Kiufupi usiache kutumia karamu na karatasi kwenye maisha yako maana kichwa unachotegemea kukutunzia vitu vyako kinaweza kumbana na mambo mengi maishani. Mambo ya mitandao, matatizo ya familia na changamoto nyingine zote zinasubiri kuingia kichwani mwako.
Kuweka malengo chini ya miezi mitatu
Unataka kukifika mwezi wa 12 ndio uanze kufikilia kama mwaka huu umezembea au vipi? Acha hiyo tabia. Anza kujiweka malengo madogo ya miezi mitatu yatakayokua yakuonesha kama umezembea kabla haijafika mwezi wa 12. Yani gawanya lengo lako la mwaka kwenye miezi mitatu mitatu alafu kila mwizi mitatu ikifika unatulia unajiuliza “Nipo ninapotakiwa kuwa au nimezembea? Nifanye nini?”. Kufanya hivi kutakufanya uongeze umakini kabla ya mwaka haujaisha. Kama malengo yako yanaruhusu, unaweza weka hata miezi miwili na ikawa msaada kwako.
Fanya mambo kwa kasi kabla ya muda
Ikiwa unamipango migumu uliopanga na unatamani kuzitimiza, njia nzuri ya kuzitimiza ni kuanza kuipambania kwa kasi mapema. Yani kama kunajambo unatakiwa kulifanya kila siku ndani ya siku Saba(7) ndio ulitimize, Anza siku ya kwanza kwa kufanya kazi ya siku tatu. Kama ni kuweka pesa kiasi flani kila siku, Anza kwa kuweka pesa nyingi zaidi ya hiyo ya siku moja.
Kiufupi ukipata nafasi ya kufanya vitu vya kesho au kesho kutwa katika siku ya Leo, basi fanya Leo maana kesho kunaweza kuwa na changamoto ambayo bado haujaijua.
Kufanya hivi kutafanya uweze kupambana na changamoto katika safari yako bila kuiathiri sana safari uliojiwekea. Na vile vile tabia hii inaweza kukujenga ukawa mtu makini sana kwenye mambo yako.
Ahadi ya kubeba kila changamoto bila kukata tamaa
Usije msingizia mtu tena kuhusu wewe kushindwa kutimiza malengo yako. Jitahidi kubeba kila kitu kigumu utakachokutana nacho bila kutaka tamaa.
Tambua kuwa hakuna mwaka ambao hautakuja na changamoto. Hata waliofanikiwa wamefanikiwa lakini bado wanapambana na changamoto. Adui mkubwa wa malengo ya mwaka ni muda. Uheshimu muda maana ukizembea alafu muda wa mwaka uliojiwekea ukiisha, utakua umepunguza mwaka moja kwenye maisha yako ya Duniani lakini haujafanikiwa kukifanya unachokitaka. Sasa upo tayari kupoteza mwaka mwingine wa Maisha yako kumlaumu mtu au watu?
Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kama makala kama hizi zinakua msaada kwako. Usisahau kuwa karibu nasi kwenye mambo mengine na kwenye mitandao ya kijamii pia.
Jinsi ya kutengeneza Logo ya biashara au binafsi BONYEZA HAPA>>>