Unajuaje kama Ex wako anakupenda? Dalili ni hizi

Mahusiano ya mapenzi yanaweza kuwafanya watu waamini kuwa watakua pamoja milele lakini sio kila mahusiano hufikia huko. Baadhi ya watu hushindwa kufikia malengo ya mahusiano yao baada ya kukumbana na mambo ambayo hutikisa au kuvunja mahusiano. Lakini pia sio kwamba Mahusiano yanayodumu huwa hayapitii mambo kama hayo, hupitia mambo magumu. Kuna watu huvunja mahusiano kabisa na kuitana “ex” lakini baada ya muda hurudiana tena na kuendelea kuwa pamoja. Kiufupi kurudiana na mpenzi wa zamani ni jambo la kawaida ambalo watu hufanya.

Kama bado mpenzi wako wa zamani unampenda, kujaribu kumuelewa mpenzi wako wa zamani inaweza kuwa ni changamoto. Wakati mwingine, mpenzi wako wa zamani anaweza kutoa dalili za kukupenda lakini kichwani kwako ukawa unawasiwasi na hauzielewi. Hapa katika The bestgalaxy, tutazungumzia kuhusu dalili za mpenzi wa zamani(ex wako) kukupenda. Kujua dalili hizi husaidia kumuelewa au kujua kama bado mpenzi wako anakupenda na kuna nafasi ya kurudisha upendo wenu ikiwa na wewe Bado unampenda.

Kujua dalili hizi kunaweza kukupa uwezo wa kujua hisia zake na kusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu kurudisha uhusiano wenu. Wakati ukifanya hayo, ni vema kufahamu kuwa maamuzi ya kurudisha na mpenzi wa zamani yanaweza kuwa maamuzi mabaya pia kama hautafanya utafiti vizuri juu ya lengo lake kwako.

Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Dalili za mpenzi wa zamani kukupenda

Kuweka ugumu katika mawasiliano

Kuna watu mkiachana huwa wanakata njia za mawasiliano haraka na kukuwekea ugumu wa kuwapata lakini moyoni wanaokua bado wanakupenda. Mtu hufanya hivyo kwa msukumo wa hasira tu au ili aone unamtafuta na ajiridhishe kuwa anamuhitaji. Anaweza kublock kwenye simu na kukuwekea ugumu wa kukutananae lakini siku akiona umepambana na kukutananae mkaogea, atajisikia vizuri kuliko kawaida.

Mara nyingi hii hutokea endapo wewe ndio chanzo cha mahusiano kuvunjika. Adhabu anayokupa ni kuwa mbali na wewe kwa kukata ukaribu ili angalau uone umuhimu wake na kutambua makosa yako. Kupambana kumtafuta kunaweza fanikisha kurudisha uhusiano wenu.

Kukutafuta au kufungua njia za mazungumzo

Mpenzi wa zamani anaweza kuwa anakutafuta kwa njia mbalimbali na kufungua njia za mazungumzo kati yenu. Hii inaweza kuwa dalili ya mpenzi wa zamani kutamani murudiane. Anaweza kuwa anafanya hivi baada ya kukumbuka ukaribu wako na Mapenzi yenu kwa ujumla.


Kukupigia simu, kukutumia sms, kukuondolea block kwenye simu au kutafuta vinjia vingine vya kufanya maongezi na wewe ni ishara za kutaka murudiane. Wengine huwa wanashindwa kuficha kabisa hisia zao na kutaka mzungumzie mambo ya mahusiano yenu. Hapa ndio utasikia akisema mambo kama “Ulienae kwa sasa anafaidi… Umenifanya mapenzi niyaogope… Msalimie mpenzi wako” ili tu muongelee mahusiano yenu.

Wivu unapokua karibu na watu wengine

Njia rahisi ya kujua ex wako anakupenda au hakupendi ni wivu. Ni ngumu sana kwa mpenzi wa zamani kukuficha wivu wake anapo kuona na watu wengine. Kama hakupendi, anaweza asiwe na wivu ila kama anakupenda, moyo wake hauwezi muacha salama pindi unapooneka upo karibu na watu wengine. Anaweza kukosa amani au kufanya jambo lingine linaloonesha anawivu na wewe. Kama ni mtu wa “WhatsApp Status” basi wivu juu ya jambo aliloliona kwako atauweka kwenye Status yake kwa maneno ya kukuumiza au kuonesha ameumizwa.

Yupo makini sana na wewe au mambo yako

Ex anaekupenda anaweza igiza kukupuuza lakini hawezi kukupuuza kirahisi. Unapoongea nae anaweza igiza kukupuuza lakini huwa anazingatia kila neno. Mkiwa sehemu moja anaweza igiza kutokukuzingatia lakini macho na akili yake inakua kwako. Kuna muda unaweza gongana nae macho akiwa anakuangalia alafu akazuga kufanya mambo mengine. Yote ni kwasababu anakupenda na upo kwenye akili yake.

Ni hayo tu katika makala hii ya The bestgalaxy, kama utapenda unaweza Endelea kusoma makala nyingine. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi huku ukijiunga nasi kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a comment