Kuchepuka kuna faida ila hizi ni hasara zake

Kuchepuka, au kumsaliti mpenzi wako(mume/mke), ni jambo ambalo limekuwa na athari kubwa sana. Ingawa inaweza kuonekana kama jambo la siri na linafaida, lakini ukweli ni kwamba kuchepuka kunaweza kuwa na madhara makubwa na yakudumu maishani mwawahusika.


Sababu za kuchepuka zinaweza kuwa ni mtu kutoridhika na mahusiano ya mapenzi alionayo na kutafuta furaha ya muda mfupi pembeni. Mbali na Sababu hiyo, kuna sababu nyingine nyingi zinawezapelekea mtu kuchepuka. Kuchepuka kuna faida zake na moja ya faida ni kupunguza msongo wa mawazo hasa kama mpenzi wako hakujali.

Watu wengi huenda kwenye michepuko kupata amani ya moyo au kujipumzisha kwenye mahusiano walionayo kwasababu mbalimbali. Pamoja na jambo hili kuwa na faida lakini haina maana ni jambo zuri. Na kuna baadhi ya watu hufanya hivyo lakini kiundani ni hawapendi kuchepuka.

Madhara ya kuchepuka yanaweza kuonekana katika pande mbalimbali za maisha, zikiwemo afya ya kiakili na kimwili, mahusiano ya kifamilia, na hata nafasi ya mtu katika jamii. Watu wanaochepuka hawafikirii matokeo ya muda mrefu ya vitendo vyao, na hivyo kujikuta wakisababisha maumivu na matatizo ambayo hayawezi kutatulika kwa urahisi.

Katika makala hii, tutajadili kwa undani hasara chache zinazoweza kutokana na kuchepuka. Tunafanya hivi kutoa mwanga juu ya jinsi gani vitendo hivi vinaweza kuathiri maisha yetu na wale tunaowapenda.

Jinsi ya kumtuliza mpenzi wako mkikosana BONYEZA HAPA>>>

Hasara za kuchepuka kwa mwanamke au mwanaume

Kupata magonjwa

Kuwa na mchepuko ni kufungua mlango wa magonjwa kwenye mwili wako na familia yako pia. Kuna magonjwa mengi mtu unaweza pata kwa mchepuko na kumpelekea mpenzi wako pia. HIV na magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kumpata kirahisi mtu mwenye mchepuko na kuiathiri familia yake pia.
Kama ni mtu useihitaji magonjwa haya na unataka kujikinga basi unashauriwa kutochepuka. Kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako ni njia ya kujikinga na magonjwa kutoka nje ya mahusiano yenu.

Kumuumiza mpenzi wako au familia

Watu wengi wanapochepuka huwa wanahisi endapo mpenzi atatambua kuwa anachepuka ndipo ataumia. Lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wakianza kuchepuka huanza uonesha tabia tofauti kwa wapenzi wao. Tabia hizi tofauti huwa zinaanza kumuumiza kabla haya ukweli haujajulikana.


Kama mpenzi wako anakupenda na anakujua vizuri, ni ngumu sana kumficha unapopata mchepuko. Tabia na baadhi ya mambo yako mengi yatabadilika japo hautajitambua. Hali hii itamuingiza kwenye mawazo na maswali mengi ya kumuumiza.
Tabia hizi zinaweza fikia hatua ya kuidharau familia na kufanya mambo mabaya bila kujitambua.

Kuwa mtumwa wa Siri

Kuwa na mchepuko ni Siri ambayo inaweza kukufanya uwe mtumwa kwenye maisha yako. Siri ya kuwa na mchepuko inaweza zaa Siri nyingine inayoweza kufanya usiwe huru kwa mpenzi wako. Kuna watu hutamani mpaka kuiacha michepuko yao lakini wanashindwa kutokana na kuwa watumwa wa siri. Mchepuko unaweza kukujia juu na kutishia kufichua Siri kwa namna mbalimbali ili tu uendelee kuwa mtumwa.


Mbali na hayo, kuwa na mchepuko kunaweza pelekea mtu kupata mtoto wa nje na kuwa mtumwa wa Siri hiyo. Kiufupi Siri ya kuwa na mchepuko inaweza zaa Siri nyingine nyingi zitazokufanya mtumwa unaepambana kufunika vitu ulivyofanya gizani kila siku.

Mfano mzuri wa jambo hili upo katika simulizi ya WEUSI WEUPE, wanawake wengi kwenye simulizi hii waligeuka watumwa wa siri.

Kupata msongo wa Mawazo

Wakati mwingine msongo wa Mawazo unaweza tulizwa na mchepuko lakini sio nyakati zote. Kuwa na mchepuko kunaweza ongeza au kuleta msongo mwingine wa Mawazo. Kuna mambo mengi sana kutoka kwa mchepuko yanaweza kukueletea mzongo wa Mawazo. Mambo kama magonjwa, fumanizi na hata ujauzito unaweza tokea na kukupa msongo wa Mawazo.

Kuyumba kiuchumi au kusahau maendeleo yako

Uchumi wako unaweza athiriwa na mambo yako ya mahusiano ya mapenzi. Mchepuko unaweza kukufanya utumie pesa vibaya au kukupumbaza usifanye mambo ya maendeleo na mpenzi wako. Kuna wanaume hujikuta wanapeteza pesa nyingi za maendeleo kwa michepuko. Na pia kuna wanawake hujikuta wamepoteza pesa au mali za familia kutokana na michepuko.

Kiufupi michepuko inaweza onekana mizuri lakini matokeo yake ni mabaya. Na ubaya mambo ya Siri ni kwamba yakienda vibaya yanakua makubwa sana.
Ni hayo tu katika The bestgalaxy, Endelea kuwa nasi.

Leave a comment