Jinsi ya kumtuliza mpenzi wako mkikosana au kutoelewana

Kutokuelewana na kufanyiana makosa ni mambo ya kawaida na hutokea mara nyingi sana. Hakuna anaependa mambo hayo yatokee lakini mara nyingi hutokea bila kutarajia.


Kutokuelewana au kufanyiana makosa kunaweza fanya mahusiano ya mapenzi kutikisika na hata kuvunjika kabisa. Lakini hii inategemeana na jambo lililofanya wapenzi mufikie hatua mbaya na maamuzi au hatua muliochukua baada ya kukoseana au kutoelewana.


Katika mambo muhimu kujua katika Mahusiano ni jinsi ya kufanya mnapokoseana au kutoelewana na mpenzi wako. Ni muhimu Kwasababu kukosana na kutoelewana ni kama hakupingiki kwenye mahusiano, hutokea tu. Lakini ukiwa na ufahamu wa jinsi gani ufanye, itakusaidia kwenye kuweka sawa mahusiano kwenye hali hiyo.

Katika makala hii, tutajadili jinsi ya kumtuliza mpenzi wako mnapokosana au kutoelewana. Kwa kuelewa na kufuata mbinu sahihi, unaweza kusaidia kurejesha amani na kuimarisha uhusiano wenu bila shida.

SMS za kumfanya mpenzi wako afurahi BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kufanya kumtuliza mpenzi wako mkikosana au kutoelewana

Muombe msamaha

Baada ya kukosana au kutokuelewana kulikosababishwa na wewe ni vema ukamuomba msamaha mpenzi wako. Neno “Samahani” linaweza muweka sawa mpenzi wako na kumrudishia katika hali ya kwaida. Neno hili ni moja ya maneno yenye nguvu za kurekebisha hisia za mtu na kumuweka sawa mnapokua mmekosana.
Ukimkosea mtu bila kumuomba msahama anaweza kuwa na mawazo mengi sana. Wengine usipo waomba msamaha huwa wanakupangia vitu vingi kichwani ili kukulipizia. Lakini ukiomba msamaha baada ya kukosea inaweza fanya mwenza wako asifike mbali sana kimawazo.

Muache peke yake kwa muda

Kuna baadhi ya watu wakikosewa au wakitokewa na kutokuelewana huwa wanahitaji kuwa peke yao kwa muda ndipo watarudi sawa. Usipo mpa muda wa kuwa peke yake hata msamaha wako hawezi kuuelewa.
Sio kila mtu yupo hivyo ila kama ukiwa kwenye mahusiano na watu wa namna hii basi uwe unaheshimu muda wake wa kuwa peke yake pale ambapo hamuelewani au mmekosana. Unaweza ukamuacha peke yake wa muda alafu ukaanza kujisogeza tena kidogo kidogo.
Hii inaweza kuwa sio njia ambayo mtu unaweza fikili kuitumia kwa haraka haraka ila ni njia muhumu ya kuweka sawa kiakili baadhi ya watu mnapokosana.

Mzawadie kitu anachokipenda

Baada ya kukosana au kutokuelewana unaweza muweka mpenzi wako kwenye hali ya furaha kwa kumpa zawadi. Tafuta zawadi nzuri unayohisi anaweza ifurahia alafu mpatie.
Wote tunajua hakuna asiependa au kufurahia kupewa zawadi za gharama Duniani, lakini zawadi sio lazima iwe ya gharama. Zawadi nzuri inaweza kuwa kitu chochote kizuri kinachoweza ugusa moyo wa mtu. Kwaiyo jaribu kufikilia kitu chochote kizuri kitakacho ugusa moyo wa mwanamke au mwanaume umpendae. Kama ukikipata cha bei ndogo au kubwa, fanya kumpatia ili kumtuliza au kumuweka sawa.

Jinsi ya kum-surprise au kumshangza mpenzi wako bila kutumia Pesa BONYEZA HAPA>>>

Mwambie maneno mazuri ya upendo

Kwenye mahusiano ya mapenzi maneno ya upendo huwa yananguvu sana. Neno moja au mawili mazuri ya upendo yanaweza upasua moyo kwa furaha. Hasira na makasiriko baada ya kutoelewana au kukosana, vinaweza tulizwa na maneno matamu ya upendo.
Ukikosana na mpenzi wako au kutoelewana nae, unaweza tumia maneno mazuri au matamu kumuweka sawa. Unaweza mkumbusha jinsi gani unampenda, umuhimu wake kwako, uzuri wake na mambo mengine ya kuvutia au kugusa moyo.

Ni hayo tu katika makala hii, natumai unaweza kuwa umeelewa jinsi gani unaweza mtuliza mtu wako mnapokua hamko sawa. Napenda kusisitiza kwamba watu tupo tofauti hivyo ni vema kufikilia kidogo kama njia unayataka kuitumia inamfaa mwanamke au mwanaume umpendae.

Leave a comment