Katika ulimwengu wa kidijitali, ununuzi na utafutaji wa bidhaa au huduma mtandaoni umekuwa jambo la kawaida kwa watu. Lakini, pamoja na urahisi na faida zinazotokana na kutumia mtandao kwa shughuli hizi, kuna hatari nyingi wanazokumbana nazo watumiaji.
Moja ya hatari kubwa ni utapeli au wizi wa mtandaoni. Hii hua inatokea kutokana watu wasio waaminifu kutumia mbinu mbalimbali kuwalaghai wale wanaotafuta vitu au mambo flani mtandaoni. Utapeli wa mtandaoni umeongezeka kwa kasi sana katika miaka ya hivi karibuni na Hali hii ipo online dunia nzima.
Matapeli wanatumia teknolojia za kisasa na mbinu za ujanja ili kuwaibia watu taarifa zao za kibinafsi na fedha. Tatizo hili ni inasemekana kuwa ni gumu kumalizika maana Teknolojia inapokua, haiimarishi vifaa vya ulinzi tu, inaimarisha na mambo yao pia. Jambo la muhimu kupunguza jambo hili ni kila mtu kuwa makini na ufahamu wa mambo ya Teknolojia na usalama.
Mambo ya kuzingatia unaponunua bidhaa mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Kutafuta vitu hivi mtandaoni kunaleta hatari kubwa ya kutapeliwa au kuibiwa
Kupata App au software za bure
Kama kuna app au software yoyote inayouzwa au kulipiwa ni vema ukafuata utaratibu rasimi wa kuipata na sio Bure. Njia nyingi za kupata app au software hizo za Bure sio salama. Unaweza pata sehemu ambayo inatoa Bure lakini ukiingiza software au app hiyo kwenye kifaa chako inaiba taalifa zako na kuweka hatarini mambo yako pamoja na watu unaowasiliana nao. Sio rahisi kufahamu hili kama hauna ufahamu juu ya usalama kwenye upande wa Teknolojia ila unaweza epuka hatari hii kwa kutoingiza za app za Bure ovyo.
Mikopo ya haraka bila utambulisho
Kuna watu huwa wanatafuta mikopo ya hataka lakini hawataki kutoa taalifa zao nyingi kuogopa kutafutwa wakishimdwa kulipa. Sasa jaribu kufikilia ungekua wewe ndio unaekopesha ungeweza kumpa mtu pesa nyingi bila kumjua vizuri? Au bila kutafuta atakaposhindwa kulipa?
Ni wazi kuwa inaweza kuna ni jambo gumu kidogo hata kwako. Sasa endapo ukitafuta mtandaoni Mkopo mkubwa ambao unasema kuwa utapewa bila mtoa Mkopo kukujua vizuri basi fahamu kuwa unaweza kuwa hatarini. Unaweza kuwa hatarini kwasababu mtoa Mkopo wa mtindo huo kwa asilimia 60 anaweza kuwa ni Tapeli. Mtoa Mkopo wa kweli anataka akujue vizuri ili iwe rahisi kukupata na hii ndio maana hata app za mikopo huwa zinachukua taalifa nyingi kwenye simu unapozitumia. App za mikopo zinaweza chukua mpaka namba za watu ulizonazo kwenye simu.
Kutengeneza pesa nyingi mtandaoni kwa haraka au rahisi
Kama ni mtu unaefuatalia mambo ya kutengeneza Pesa na kujiweka sawa kiuchumi basi unaweza vutiwa na “kutengeneza pesa mtandaoni “. Jambo hili linaweza kuwa ni rahisi sana kuliongea lakini linaweza kuwa sio rahisi kwenye matendo.
Kuna Platform zinaweza kukuambia kuhusu kutengeneza nyingi rahisi lakini safari ikawa ngumu ila kukawa na ukweli ndani yake. Pia kuna Platform nyingine nyingi zinaweza sema hivyo kukuvutia ili zikutapeli. Hivyo ni vema kuwa makini unapokua kwenye upande huu.
Kuona sms za mtu mwingine bila kugusa simu
Watu wengi hutamani kujua juu ya hili na kuna maelezo mengi kuhusu jambo hili katika internet. Maelezo mengi yaliopo mtandaoni juu ya kuchunguza mtu mwingine sio ya kweli na yanaweza kukuweka kwenye hatari ya kutapeliwa au kuibiwa. Kuna maelezo yanaweza kukufanya uibiwe pesa, uharibu simu yako na hata kuvujisha vitu(sms,picha au video) vyako vya kwenye simu au simu ya mlengwa.
Unasisitizwa kuwa makini unapofanya au kutafuta mambo mtandaoni ili kuwa salama. Lakini pia ukipata matatizo kwa bahati mbaya unatakiwa kutokata tamaa. Usiruhusu mambo hayo yakuzuie kufaidika na mtandao.