App nzuri za simu katika kufanya mazoezi ya mwili

Kuna app nyingi ambazo tunaweza ziingiza kwnye simu zetu na zikawa msaada kwenye vitu au mambo tunayofanya kwenye maisha. Hapa kwenye ukurasa huu The bestgalaxy tumekusanya app chache zinazoweza saidi katika upande wa mazoezi ya mwili. Nadhani wengi tunajua umuhimu wa mazoezi ya mwili katika maisha ya mwanadamu, hasa katika kipindi hiki chenye mambo mengi yanayohatarisha afya ya mwili wa binadamu.

Binadamu wa sasa tumezungukwa na vyakula pamoja na tabia nyingi zisizo rafiki kwa Afya zetu, ukiwa kama mwanadamu wa kipindi hiki unashauriwa kufanya mazoezi ili kuuweka mwili sawa na kuepuka baadhi ya magonjwa. Kabla ya kwenda moja kwa moja kuangalia app hizi, nakukumbusha kuijenga na kuendelea kuilinda tabia ya kufanya mazoezi maana ni jambo la maana usiloweza kujutia maishani.

Home workouts app: credit

App nzuri za simu katika kufanya mazoezi ya mwili(Android na iOS)

Home workouts

Hii app ni maarufu sana katika upande wa app za mazoezi za simu. App ya Home workouts imejikita zaidi katika kusaidia watu wanaotaka kufanya mazoezi ya mwili wakiwa nyumbani. Inakupa mbinu za mazoezi ya kufanya ili kuweka misuli ya mwili vizuri, kupunguza uzito au kupunguza mwili. Inakuonesha jinsi unavyoweza fanya yote hayo ukiwa nyumbani bila kwenda GYM zilizo mbali na ulipo. Inaweza simama kama mwalimu au msimamizi wako wa mazoezi ya nyumbani ukiwa kama Mwanamke au Mwanaume unaempenda mazoezi.

Workout for Women

Hii app ni kwaajili ya mwanawake unaehitaji kufanya mazoezi. Kama wewe na mwanamke unaetaka kufanya mazoezi ya mwili lakini unakosa muda wa kutoka ulipo na kuelekea GYM, basi app hii inaweza kuwa masada zaidi kwako. App ya Workout for Women inasimama kama mwalimu wa nyumbani wa mazoezi ya kuweka mwili sawa. Inakupa mazoezi ya kupungiza tumbo, kuongea makalio na kufanya ujihisi mwepesi. Workout for Women inakupa mbinu za kufanya mazoezi hata ukiwa kitandani hivyo itakua ni juu yako tu kutenga dakika chache kujiweka sawa kila siku.

Strava

Strava ni app maalumu kwa watu wanaopenda kufanya mazoezi lakini mazoezi haya sio ya sehemu moja. Hii ni kwaajili ya mazoezi kama kukimbia au kuendesha baisikeli. Wengi hufanya mazoezi haya asubuhi au jioni ili kuwema miili yao sawa. App hii inasidia mtu kupima umbali anaokimbia kila siku na kujua anakimbia kutoka wapi kwenda wapi.

Inaweza kuunganishwa na saa za kidigitali zinazofahamika kama “Smartwatch” japo sio zote. Inasaidia kuangalia maendeleo katika mazoezi yako hirahisi kwenye simu. Unaweza angalia hata Hali ya mapigo yako ya moyo unapofanya mazoezi (Hii itakuitaji utumie Heart rate monitor au Smartwatch).

GYM DONE

App hii imejikita zaidi kwenye upande wa mazoezi ya GYM. Ni app inayoweza kukuongoza unapofanya mazoezi kwenye chumba Cha GYM kwakutumia vifaa mbalimbali. Kwenye app ya GYM Done unaoneshwa mbinu au namna ya kutumia vifaa vya GYM kuweka vizuri misuli ya sehemu tofauti za mwili. Mtumiaji unaweza pia kujiweka mipango yako ya mazoezi ili kukamilisha malengo yako.

App za mazoezi ya mwili zimekua zikitumika na mamilioni ya watu wanapofanya mazoezi na zimekua msaada mkubwa katika kujenga afya ya mwili. Ni app hizo tu katika orodha yetu lakini fahamu kuwa kuna app nyingi nzuri kwa mazoezi ya mwili. Endelea kuwa nasi kwa mambo mengine zaidi.

Leave a comment