Kuna utofauti wa simu za bei ya kawaida na bei kubwa?

Simu za smartphone Kuna watu huziweka kwenye makundi mawili. Kuna simu huangaliwa kama za bei kubwa(Bei ghali) na pia kuna simu huangaliwa kama ni za bei ndogo(kawaida/rahisi).


Wakati mwingi, watumiaji wanapotaka kufanya uamuzi wa kununua simu mpya, wanajiuliza kama wanapaswa kuchagua kifaa cha bei rahisi au kuwekeza katika kifaa cha bei ya juu. Hatakama hawana uwezo wa kumikili simu za bei ya juu hununua simu za bei rahisi na kuendelea kuzitolea macho simu za bei ya juu.


Simu za bei ya juu zinaweza kuwa chaguo zuri sana kwa mtu. Lakini itakua vizuri zaidi kama utajua tofauti zinazoitofautisha simu ya bei ya juu na bei rahisi.

Mambo unayotakiwa kujua kuhusu simu za mkopo BONYEZA HAPA>>>

Simu za bei ya chini na Simu za gharama

Makampuni kupanga bei ya simu

Simu za smartphone huwa zinaundwa na vitu vingi sana. Mpaka simu ya smartphone imetangazwa na kampuni kuwa imetolewa na watu wanaweza nunua, huwa inakua imeundwa na vitu vingi tena kutoka kwenye Makampuni mbili mbali. Vitu kama vioo, battery, processor au camera, vinaweza kuwa vimeundwa toka kwenye Makampuni mengine.


Kampuni ya simu inaweza kuwa imetumia gharama nyingi sana kupata vitu hivyo kwenye Makampuni mengine na utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu. kwaiyo inapoiuza simu hua inaangalia gharama hizo na gharama nyingine za utengenezaji ili kupanga bei itakayorudisha gharama za utengenezaji na kuleta faida pia.

Utofauti kati ya simu za bei ya juu na bei ya chini

Kampuni kama itatumia Teknolojia ya hali ya juu na vitu bora katika utengenezaji wa simu inaweza kuwa imetumia gharama kubwa pia. Jambo hili linaweza fanya simu iwe Bora alafu iuweze kwa bei kubwa. Hivyo simu za bei kubwa mara nyingi zinakua Bora na zimeundwa vizuri kuliko simu za bei ya chini japo sio zote.

Simu za gharama zinaweza kuwa na uwezo wa kufanya vitu vikubwa kwa haraka, Camera zenye ubora na vipengele vingine bora au vizuri kwa mtumiaji.

Lakini Kampuni huwa zinajua kuwa sio kila mtu anaweza fikia gharama za hiyo simu bora yenye gharama kubwa.

Huwa mara nyingi kampuni zinapotoa simu moja mpya, zinatoa matoleo mawili, matatu au zaidi. Matoleo haya hutofautiana bei na hata ubora au vitu utakavyofurahia ndani yake. Kunakua na matoleo ya juu ambayo huwa na bei ya juu na huongezwa majina kama vile “Pro” “Utra” au “Max” alafu pia kunakua na matoleo ya bei chini yanayoweza kuitwa “Mini”. Mfano kwenye kampuni ya Samsung kuna simu inaitwa “Samsung Galaxy S24”, lakini inatoleo la juu kabisa linaitwa “Samsung Galaxy S24 Utra”

Mbali na matoleo tofauti ya simu moja, Kuna kampuni hutoa aina ya simu ziliozo rasimi kabisa kwa lengo la kuuza bei ya chini.

Kuna watu husema “Simu za kichina ni bei rahisi alafu hazidumu” lakini ukweli ni kwamba china hutafuta njia za kupunguza gharama za utengenezaji wa vitu ili kuuza vitu kwa bei ndogo ambayo ni rafiki kwa mtumiaji. Lakini pia China huwa ina simu au bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo hudumu ila hupatikana kwa bei kubwa pia.

Unapaswa kuchagua simu gani?

Hakuna ulazima wa kuwa na simu yenye gharama kubwa wakati hauna uwezo au matumizi makubwa. Na pia hakuna ulazima wa kuwa na simu ya bei ndogo wakati unauwezo wa kuwa na simu ya bei kubwa yenye uwezo unaouhitaji. Kiufupi kuchagua simu ipi ya kununua ni uamuzi wako. Lakini kabla haujachagua simu simu, tambua unataka nini kwenye simu. Kama umepata simu inayokupa unachokitaka, haijalishi ni bei ya chini au juu, hiyo ni simu bora kwako. Ni vema ukaangalia zaidi kama inaendana na matumizi yako na sio kuwalidhisha watu.

Leave a comment