Kama unatumia simu ya smartphone ya Android, unapaswa kufahamu kuwa unaweza tumia app ya sms za kawaida zaidi ya ilivyozoeleka. Unaweza tuma jumbe za maandishi, sauti na hata kutuma video au kupokea vitu hivyo kwa watu wengine. Kama ilivyo kwenye app ya WhatsApp au Telegram ndivyo app yako ya sms za kawaida inaweza tumika. Hapa The bestgalaxy unaenda kujuzwa kuhusu jinsi ya kufanya hivyo ila kabla ya yote hebu tuelewe maana ya “RCS messaging” kwanza.
“RCS messaging” (Rich Communication Services) ni njia mpya ya kutuma na kupokea jumbe kati ya simu za smartphone. Njia hii hua inatumia data(internet) badala ya SMS za kawaida kwenye Lain yako. Kupitia huduma au njia ya RCS messaging, watu wanaweza tumiana vitu vingi ikiwemo video, picha na Audio. Kwa watu wa iPhone jambo kama hili walikuanalo kwenye app ya iMessages japo kuna utofauti.
Jinsi ya kutuma picha, video, sauti au kwenye app ya sms za kawaida (Android)
Unaweza kutuma picha, video au sauti kwenye app ya sms za kawaida kupitia RCS messaging. Kufanya hivi ukiwa na simu ya android utahitajika kutumia app ya sms ya Google). App hii inaitwa “Google messages”, inapatikana playstore. App hii kwenye baadhi ya simu inakuepo tu bila kuiiingiza(kuiinstall). Lakini kwenye simu nyingine inakua haipo hivyo, tutatakiwa kuingiza mwenyewe kutoka Playstore.
Kama unataka kuingiza app ya Google messages au kuanza kutumia RCS messaging kwa ujumla, unaweza fuata hatua zifuatazo;
- Ingia Playstore utafute app inayoitwa “Google messages” kisha iingize kwenye simu. Kama tayari unayo fanya ku-Upate tu.
- Baada ya hapo ifungue na kukubali Sheria za RCS messaging kwakubonyeza “Agree”. Kama itakuomba nafasi ya kuwa “Default SMS app” utatakiwa kukubali pia.
- Baada ya yote kuwa sawa app ya Google messages, app hiyo inaweza kukuomba namba ya simu kwaajili kuanza kutumia RCS messaging. Jaza namba ya simu na baada ya hapo ukiwa na namba ya mtu ambae pia ameset RCS kwenye simu yeke, mtafurahia kutumiana video, picha na video kupitia app hiyo.
- Kama haujaletewa sehemu ya kujaza namba, gusa profile au icon inayopatikana juu upande wa kulia kwenye app ya Google messages. Baada ya hapo ingia kwenye kipengele cha Settings cha app ya Google messages kisha changua RCS Chats na uiwashe RCS. Katika kuiwasha utaulizwa namba ya simu. Baada kuweka sawa namba ya simu utakua tayari umeanza kuitumia RCS messaging kwenye simu yako.

Faida za kutumia RCS messaging ni kupata uwezo wa kutuma na kupokea picha na video zenye ubora wa juu, Kuona mtu anapo andika ujumbe “Typing”. Mbali na hayo, mtumiaji utaona SMS ulizotuma kama zimefika au kusomwa(Delivery receipts). Unaweza kuunda magroup pia.
Kama utakua unahitaji mwanga zaidi katika hili, unaweza wasiliana na The bestgalaxy ukasaidiwa.
Jinsi ya kupata namba zilizofutika kwenye simu BONYEZA HAPA>>>