SMS inaweza kuwa njia nzuri ya kueleza hisia za upendo na mapenzi kwa mwanamke au mwanaume umpendae. Sms kama sms zinamchango mkubwa katika mahusiano ya sasa maana ndio mara nyingi huunganisha wapenzi wakiwa mbali.
Katika makala hii, tumekuangalia jumbe mbalimbali za SMS ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kumwambia kuwa unampenda. Kuonyesha upendo kupitia maneno kunaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano na kuongeza ukaribu kati yenu. Kunaweza mkumbusha jinsi gani unampenda na unahitaji.
Kwenye mahusiano ya mapenzi, maneno ni kitu kikubwa sana. Maneno yanaweza yumbisha mapenzi na hata kuyaweka sawa pia. Soto tunajua kwamba wakati mwingine mnaweza kuwa kwenye mahusiano lakini yakawa yanayumba. Kumwambia maneno mpenzi wako ya jinsi gani unampenda kunaweza mkumbusha mpenzi wako kushikamana na kuwa pamoja kwenye mahusiano. Na pia kuna muda mpenzi anaweza kuwa na kiu ya maneno mazuri toka kwako lakini akashindwa kusema maana na yeye haelewi.
SMS za kumsifia mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Sms za kumwambia mpenzi mwanamke/mwanaume unampenda
- Yule mtu anaeweza ufurahisha au kuuvunja moyo wangu ni wewe. Kuwa nawe ni furaha ya moyo wangu, sitamani kuwa mbali na wewe.
- Kama kukupenda ni ujinga basi nakubari kuwa hivyo. Penzi lako limeushika moyo wangu mpaka naogopa. Ukiona chozi langu la maumivu ya mapenzi limenidondoka jua ni wewe. Na ikitokea hivyo naomba usije sahau kuwa hata wakulifuta pia ni wewe. Nakupenda sana.
- Nakupenda Toka moyoni, Ukaribu wako huichemsha damu. Kuwa na Wewe ni Ndoto yangu tamu, staki kukatishwa mpenzi maana hainiishi hamu.
- Penzi lako limenipeleka kwenye ulimwengu wa mapenzi ambao sikuwahi jua upo. Unanipa Raha, nakua na furaha kama mtoto.
- Zawadi kubwa ninayotamani kuendelea kupata toka kwako ni upendo wako. Moyo wangu umeisha lidhia kuwa na wewe maishani, na wewe ukibadilika tu, jua unaniumiza mwanzako.
- Duniani karibu kila mtu ana anae mpenda kwa dhati toka moyoni na yupo akili kila mara. Katika Maisha yangu mtu huyo ni wewe!
- Wanaweza kuwa wamekwambia au umesikia maneno mengi kuhusu mimi. Ila naomba upuuze na usikilize moyo wangu unasema nini sasaivi. Moyo wangu usema unakupenda wewe!
- Nimekua nikipenda kuangalia vitu vizuri na vyakupendeza ili nifurahi. Tangu nilipokutia machoni sina haja ya kuangalia chochote kizuri mbali na wewe ili nifurahi. Macho na kila kitu toka kwako hunivutia.
- Ninapomaliza kuongea na wewe kwenye simu hua nakata simu lakini natamani kuendelea kuisikia sauti yako tena. Sijawahi kuichoka sauti yako maana ni faraja ya moyo wangu. Nakupenda sana.
- Sijawahi jihisi mpweke nikiwa karibu na wewe mpenzi. Naweza umia kwa kupoteza vingi maishani ila nitaumia zaidi nikikupoteza wewe kipenzi. Maana nanipa sababu ya kufurahia maisha.
- Moyo wangu hupitia mambo mengi maishani. Lakini dawa yake kila mara huwa ni wewe. Unajua jua kuugusa bila kuushika. Unagusa sehemu wajinga hawawezi fika. Nitakupenda mpaka mwisho wa Maisha.
- Siri ya furaha yangu ni kuwa na wewe. Najiona wa thamani kwasababu yako. Moyo wangu umenitoraka, upo kwako. Umeuvuta kwa Raha za penzi lako. Nakupenda sana Mpenzi.
SMS hizi ni nzuri kwako? Kama ni nzuri unaweza tumia Bure kwa unaempenda. Usisahau kuangalia sms nyingine za mapenzi ndani ya The bestgalaxy na useache kuifuatilia pia. Asante sana kwa muda wako ulioutoa kusoma makala hii.
