Katika safari ya mapenzi, ni muhimu kujua kama mpenzi ulienae anakufaa kwa muda mrefu au anakupotezea muda. Wengi tunajua mahusiano ya mapenzi yanaweza anza popote na yanapoelekea inabidi yawe ni mahusiano ya kuwa pamoja katika Maisha. Hata dini huwa zinasimamia juu ya hili ndio maana watu wanaopendana kidini wanatakiwa waingie katika ndoa na kuishi pamoja.
Katika kutafuta mpenzi ambae utakua nae kwenye maisha, unaweza kutana na watu wengi, ukaingia nao kwenye mahusiano na musifanikiwe kuwa pamoja maishani. Endapo utatumia muda mrefu kuwa na mtu au mpenzi ambae hawazi kuwa nawewe maishani unaweza jilaumu baadae kwa kupotezewa muda. Jambo hili ni baya kwa mwanamke na hata mwanaume.
Bahati mbaya ni kwamba inaweza kuwa ngumu kujua moja kwa moja mtu ambae hatafika na wewe mbali. Lakini uzuri ni kuna ishara unawezeza kuziona zinaweza kuwa ni ishara za mpenzi ulienae kukupotezea muda. Ishara hizi The Bestgalaxy tumeziweka hapa chini.
Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>
Jinsi ya kujua mpenzi ulienae anakupotezea muda
Kufanya mahusiano yenu siri.
Ukiwa kwenye mahusiano ya dhati mara nyingi huwa manashindwa kujizuia kuyaonesha kwa watu wengine. Lakini kama utakua kwenye mahusiano na mtu anekupotezea muda atakua makini sana kufanya mahusiano yenu yasijulikane na wengine. Anaweza hata kukuambia usimwambie mtu kuhusu mahusiano yenu ili mue kwenye mahusiano ya Siri. Sasa swali hapa ni “kitu gani kina mfanya awe makini na usiri?”. Mara nyingi inakua ni kwasababu anampenzi mwingine anaemuheshimu kuliko wewe. Kama ni mwanaume anaweza kukupa pesa na kila kitu cha gharama ili mladi mahusiano yawe Siri. Hii inaweza kuwa ni ishara kuwa hana mpango na wewe na anakupotezea muda.
Mnatafutana kwa haja za mwili au pesa.
Sawa mnaweza kuwa kwenye mahusiano ya mapenzi na mnaambiana “nakupenda” kila mara lakini kitu gani kikubwa huwakutanisha na kufanya mkumbukane? Kama ni shida za pesa au shida za mwili basi hizo ni dalili mbaya. Mapenzi kuwa pamoja maishani ni zaidi ya pesa na tamaa za mwili. Kama hakuna kitu kinachowaweka pamoja mkakumbukana mbali pesa au shida za mwili basi mnaweza kosa hata uwezo wa kuwa pamoja maishani. Ukiona dalili hii kwa mpenzi wako, kuwa makini maana si nzuri.
Mambo ya kuepuka katika Mahusiano BONYEZA HAPA>>>
Huficha mambo yake na hataki kujua sana kuhusu wewe.
Kwenye mahusiano mtu anaekupotezea muda huwa hataki ujue vitu vingi kuhusu yeye. Anaweza kukuficha kuhusu ndugu zake, sehemu anayotoka na hata jina lake kamili. Mbali na hayo hata ikija kwa upande wake utaona hajishughulishi kujua kuhusu wewe sana. Anaweza asitake kujua kitu zaidi ya jina lako na namba ya simu. Hataki kukuingiza sana kwenye maisha yake na pia hataki ingia sana kwenye maisha yako kwasababu anajijua kuwa kwako si wakudumu.
Hajali kuhusu wewe kwenye vitu muhumu.
Unaweza umwa au kuwa na jambo la muhimu lakini asijishughulishe kwa chochote. Kiufupi unaweza kuwa nae kwenye mahusiano lakini haoni kama mambo yako yanamuhusu sana. Anaweza kuwa Hana wivu kabisa na wewe.
Hii ni dalili ya kuwa yupo kukupotezea muda na anajiona kabisa hayupo karibu na wewe hivyo kuwa makini.
Ni hayo tu katika ukurasa huu. Natumaini yanaweza kuwa msaada kwa mwanamke au mwanaume yoyote ambae yupo kwenye safari ya kutafuta mtu wa Maisha. Endelea kuwa karibu na ulimwengu wa The bestgalaxy.