Robot 5 zilizoundwa kama Binadamu (Humanoid)


Katika dunia ya sasa maendeleo ya Teknolojia makubwa yamewezesha wataalamu kuunda robot zinazofanana na binadamu. Robot zilizoundwa kwa mfano wa Binadamu zinaitwa humanoid. Safari ya kutengeneza robot za muundo huu zilianzishwa muda kidogo na wataalamu mbalimbali na mpaka kufikia sasa Kuna uwepo wa robot zenye uwezo mkubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Kufuatia uwepo wa Teknolojia ya AI (Akili bandia) robot nyingi zilizo undwa kwa mfano wa Binadamu zimekua na uwezo mkubwa katika kuingiliana na binadamu halisi. Teknolojia ya AI ni kama inafanya kuzipa akili robot za humanoid na kuziwezesha kufanya baadhi ya mambo kama binadamu.

AI ni nini na inamatokeo gani katika Ulimwengu? BONYEZA HAPA>>>


Kadri Teknolojia ya AI inavyoendelea kukua ndio robot za Humanoid zinaendelea kuwa na uwezo mkubwa katika kufanya mambo kama binadamu. Inasemekana Teknolojia ya AI ikifika katika hatua za juu, humanoid robot zinaweza kuwa na uwezo mkubwa kuliko binadamu kwenye kufanya mambo mengi. Na pia tunaweza fikia wakati robot za mfano wa Binadamu zikaweza jichanganya na binadamu kufanya shughuli mbalimbali katika Maisha ya kila siku.
Inasemekana wakati huo roboti hizi za humanoid zitakua nyingi na zitakua zikitoa msaada na huduma katika sekta tofauti. Zinaweza kuwa kwenye huduma za afya, elimu, viwanda na hata burudani.


Roboti za humanoid nyingine tayari zimeanza kuwa sehemu ya maisha ya binadamu kwasasa. Kuna robot za muundo huu ambazo tayari zinafanya kazi au kutoa huduma.
Katika makala hii hatuta chimba sana kuhusu robot za humanoid sana. Kwasasa hebu tuangalie robot chache za humanoid zilizo tengenezwa vizuri Duniani.

Robot 5 zilizoundwa kama Binadamu (Humanoid)

Ameca

Ameca ni roboti lililoundwa kama binadamu wa kiume linalojulikana kwa uwezo wake wa kuingiliana na binadamu. Imetengenezwa na kampuni ya Engineered Arts ya Uingereza.
Ameca imewezeshwa na teknolojia ya hali ya juu ya AI kuweza kuelewa na kujibu mambo katika maongezi inayoyafanya na binadamu. Anauwezo wa kuona na kutambua vitu anavyo viona kupitia camera zilizoundwa kama macho. Katika lugha, Ameca huelewa na kuzungumza lugha zaidi ya moja.

Sophia

Sophia ni roboti mwingine ambae amekuwa na umaarufu sana duniani. Aliwahi kuzua gumzo baada ya kutamka kuwa atawaharibu wanadamu. Sophia alipokua katika mahojiano CNBC alijibu “Okay, I will destroy humans,” alipokua aliulizwa kuhusu kuharibu wanadamu.
Sophia robot yupo vizuri sana katika maongezi na hii ni Kwasababu umewezeshwa na Teknolojia ya juu ya AI. Anapoongea sauti inayotoka ni ya kike na hata sura pia Kwasababu ameundwa kuwa roboti wa kike. Aliundwa na kampuni ya Hanson Robotics.

Atlas

Atlas ni humanoid robot alieletwa na kampuni ya Boston Dynamics kwaajili ya kufanya kazi zinazohitaji nguvu na usahihi. Huwezi muweka katika kundi la Sophia robot au Ameca huyu maana yeye umeundwa kwaajili ya mambo yanayo jumuisha kukimbia, kuruka na kubeba vitu.
Ni robot mwenyewe Teknolojia ya juu inayomuwezesha kufanya vitendo mbali mbali kama binadamu mkakamavu. Anaweza hata kuruka sarakasi ya kujirusha na kujigeuza hewani bila kugusa chini na akatua salama.

Optimus

Optimus ni robot alietengenzwa kwaajili ya kusaidia katika shughuli mbalimbali kama vile kazi za nyumbani, viwandani na maeneno mengine kama hayo. Robot hili hufahamika pia kama Telsa bot, ni moja ya robot maalufu katika Ulimwengu wa Teknolojia. Limetengenezwa na kampuni ya Telsa ambayo ipo chini ya Elon musk ambae ni mmiliki wa mtandao wa X.
Optimus anaweza kuwa sehemu muhimu ya nguvu kazi katika Maisha ya baadaye, kwa kuwasaidia binadamu kupunguza mzigo wa kazi za kila siku.

Jia Jia


Huyu ni roboti wa kike wa kibinadamu aliyeundwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha huko China. Alizinduliwa rasmi mwaka 2016 na anajulikana kwa sura yake ya kuvutia na uwezo wa kuingiliana na binadamu katika maongezi. Imeundwa ili kuonekana kama binadamu, na yupo vizuri katika kusikiliza na kujibu maswali anayouliza na binadamu.

Roboti hizi zinaweza fanya mambo mengi kama binadamu lakini kiukweli robot hizi bado hazipo sawa kwa 100%. Kuna makosa na mambo mengi ambayo unaweza uoneshwe kwenye video au mitandao ya kijamii lakini fahamu kuwa kuna makosa yanafanywa na robot hizi. Zinaweza fanya makosa katika kujibu maswali au kufanya matendo.

Leave a comment