Katika maisha ya mahusiano na mtu kunakua na vitu vingi ambavyo mnaweza fanyiana ili kufurahishana mkiwa kama wapenzi. Maisha ya upendo yanakua na mambo mengi ya kufurahisha kiasi ambacho ukikaa na kuyafikilia, tabasamu linaweza kukujia tu. Matukio muliofanyiana kwa msukumo wa upendo mukiwa kama wapenzi ndio mara nyingi hubakia akilini na kufurahisha moyo kila mkiyakumbuka au kufikilia. Lakini pia Matukio haya huwa yanaumiza pindi mtakapoachana au mkishindwa kutimiza ahadi zenu za kuwa pamoja mlizojiwekea.
Kumfanyia surprise mpenzi wako ni jambo zuri la kumfurahisha mapenzi wako na pia hutengeneza kumbukumbu nzuri katika safari ya mahusiano. Watu wengi wanapotaka kuwafanyia surprise wapendwa wao huwaza mambo yanayohusisha pesa tu na kusahau kuwa surprise sio lazima iwe hivyo.
Kum-surprise mpenzi wako ni kufanya jambo au kitu cha upendo cha kumshangaza na kumuacha na furaha. Unaweza fanya jambo linalo husisha pesa kum-surprise lakini kuna mambo yasio husisha pesa unaweza yafanya pia na akafurahi. Hapa chini The bestgalaxy tumejaribu kukufungua kidogo kwa kukupa matokio au mambo ambayo unaweza fanya kumshangaza mpenzi bila kutumia Pesa.
Zawadi za kumpa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Mambo ya kum-surprise/kumshangaza mpenzi wako yasio husisha Pesa
Kumpiga simu usiku sana kumwambia umemkumbuka
Ikiwa mkombali na sio kawaida wewe na yeye kuongea kwa simu usiku, njia hii inaweza kuwa nzuri na itamshangaza zaidi. Subiri usiku ufike kisha jaribu kumpiga simu itakayo muamsha usingizini. Inaweza kwa sio rahisi kumuamsha kwa simu lakini kama ukifanikiwa akapokea basi atakua ameshangazwa na simu yako. Akili itakua inatamani kujua nini kimekufanya upige simu usiku na bila kusita unaweza kumwambia sababu ni kumkumbuka, yaani umemiss. Unaweza isindikiza sababu hiyo na maneno matamu kuonesha moyo wako ulikua unatamani sana kusikia sauti yake usiku huo mpaka ukashindwa vumilia kukuche.
Kumsaidia au kufanya kazi ambazo kikawaida hufanya yeye
Kama kuna kazi au mambo ambayo kikawaida mpenzi wako huwa anafanya yeye unaweza afanya wewe ili kumshangaza. Kama ni mwanaume unaweza mkupikia mwanamke wako au ukamsaidia kupika huku ukipiganae stori kama rafiki tu. Mbali na kupika unaweza msaidia kufanya usafi wa nyumbani ambayo kikawaida hufanya yeye. Jambo hili linaweza mshangaza sana mpaka akakuuliza. Unaweza mjibu kuwa “nimeamua kukusaidia tu mpenzi wangu, nakupenda sana” au maneno mengine kama hayo.
Kumuandikia barua ya karatasi ya kawaida kwa mkono wako
Kutokana na Teknolojia watu tunatumia sana simu katika kuwatumia maneno mazuri tunao wapenda. Lakini ukihitaji kumshangaza mpenzi wako kwa sasa, mfikishie ujumbe huo kwa karatasi ya kawaida. Hakikisha unaiandika kwa mkono wako mwenyewe na unaiandika kwenye karatasi ya kawaida tu na sio karatasi maalumu. Hatakama unapesa za kununua zile kadi za upendo zenye maneno ya mapenzi, fahamu kuwa njia ya kuandika mwenyewe ni yakushangaza zaidi. Kunajinsi mpenzi wako anaweza hisi unampenda mno na yupo kichwani mwako sana. Mbali na hayo utakua umeweka kumbukumbu isio sahaulika kirahisi akili mwake.
Maneno ya kumwambia mpenzi wako usiku BONYEZA HAPA>>>
Kumuimbia wimbo mzuri wa mapenzi
Ninapoongelea kuimba simaanishi uwe msanii alafu umtolee nyimbo ambayo atakua anasikiza kwenye Redio. Na maanisha kuimba mbele yake nyimbo yoyote ya msanii iliobeba ujumbe wa mapenzi kuhusu nyinyi. Sio lazima uwe na sauti nzuri, kikubwa ni umshangaze tu. Unaweza jitoa ufahamu kidogo ukamwambia akuangalie na kukusikiliza mpaka mwisho bila kukukatisha. Jambo hili ninaweza mshangaza sana kama sio kawaida yako na litatengeneza kumbukumbu nzuri kati yenu wapenzi.
Mambo tuliozungumzia hapo juu ni machache kati ya mengi unayoweza kufanya kumshangaza mtu wako bila pesa. Mambo madogo madogo kama haya kwenye mapenzi huwa yanaunda historia nzuri isioweza futwa kirahisi. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy, tunaenda kujifunza mambo mengine zaidi.