Mambo unayotakiwa kujua kuhusu Simu za Mkopo

Siku hizi hauhitaji kujiumiza sana kupata simu Janja au smartphone maana kuna mpaka simu za Mkopo. Simu hizi zinasaidia sana watu katika kuingia kwenye ulimwengu wa kisasa na kufurahia matunda ya Teknolojia.

Kuna mambo mwengi mtu anaweza ya kosa akiwa hana simu hizi za kisasa. Na pia Kuna vitu vingi mno mtu anaweza nufaika navyo kupitia simu hizi. Ukiwa kama mtu unaeishi ulimwengu wa hivi sasa, smartphone ni kitu muhimu usichotakiwa kukikosa japo faida au umuhimu hutokana na matumizi yako.

Kuna watu wengi kwa sasa wanatumia simu za smartphone za Mkopo na zimekua msaada mkubwa kwao huku wakiendelea kulipa Mkopo kidogo kidogo. Pia kuna watu wameisha maliza malipo ya Mkopo na wanaendelea kufurahia simu wakiwa na umiliki wa simu hizi kwa 100%.

Unaweza ukawa ni mtu unaetumia au unahitaji simu hizi za Mkopo. Hapa The bestgalaxy, tunajaribu kukupa mwanga kidogo kuhusu simu za Mkopo kwa kuangalia mambo machache kuhusu simu hizi. Unaweza kupitia mambo haya kwa makini hapa chini.

Katika matumizi yako ya simu usifanye mambo haya BONYEZA HAPA>>>

Mambo unayotakiwa kujua kuhusu simu za Mkopo

Ni njia rahisi ya kupata simu mpya unayohitaji ukiwa na pesa ndogo

Kupitia huduma za Mikopo ya simu unaweza kupata simu mpya unayohitaji ukiwa hauna pesa ya kutosha kuinunua. Unaweza usiwe na shilingi laki 500,000 kamili mkononi lakini ukapata simu mpya yenye thamani ya pesa hiyo kwa Mkopo baada ya kutoa posa kidogo tu kama kianzio. Hivyo ni njia nzuri kama unatamani kupata simu mzuri mpya bila kuwa na pesa ya bei yake kamili.

Kikubwa unatakiwa kuwa na pesa ya kianzio tu ambayo mara nyingi hutegemeana na bei ya simu unayokopa na hata sehemu unayopata huduma ya Mkopo huo. Kama unakopa simu ya bei kubwa kianzio nacho huwa kinakua kikubwa.

Sio chaguo zuri kama hauna pesa ya uhakika ya kila siku

Kama unaona kabisa hautakua na pesa ya uhakika ya kulipia kila siku, simu hizi zinaweza kuwa sio chaguo zuri kwako. Simu hizi zinahitaji mtu alipie au awe amelipia malipo ya siku ili atumie. Kama mtu hatalipia, simu hua inajifunga na kumnyima mtumiaji nafasi ya kutumia mpaka atapo lipia.

Sasa ukiona hali yako ya pesa inaweza kufanya ukose pesa ya kulipia mpaka unafungiwa kwa muda mrefu, hili sio chaguo zuri sana. Ni vema ile pesa unayopanga kuweka kwenye kianzio ukachagua kununua simu used ya bei ndogo ambayo hautatakiwa kutoa pesa nyingine kuitumia. Kama hauna pesa za kulipia simu hizi unaweza kuona kero zinapojifunga wakati ni haki yao kukufungia.

Unaweza pata simu za mkopo kwenye Makampuni ya mawasiliano ya simu

Ukihitaji kupata huduma za simu za Mkopo, unaweza zipata toka kwenye maduka maalumu kwa mikopo hiyo yaliopo sehemu mbalimbali hapa Tanzania. Lakini pia hii mitandao ya mawasiliano ya simu kama Tigo na Vodacom, imejiingiza kwenye utoaji wa huduma za mikopo ya simu.

Unaweza kukopa simu kwenye mtandao wa simu unaotumia kama Vodacom au Tigo alafu ukawa unalipwa kidogo kidogo huku ukiendelea kuitumia. Unaweza wasiliana na mtandao wako wa simu kupata maelezo juu ya jambo hili. Uzuri wa kukopa katika mitandao ya simu ni kwamba unapewa OFA za vifurushi kwenye Laini ya simu. Lakini pia sehemu nyingine za kukopa simu zipo vizuri pia.

Taalifa za malipo hutunzwa

Unapotumia simu ya Mkopo ni vema ukajua taalifa zako na malipo yako mara nyingi huwa zinatunzwa ili kukusaidia pale unapokwama au usumbufu unapojitokeza. Taalifa hizi zinaweza kuwa ni namba uliotumia kulipia na hata kiasi.

Ni jambo zuri sana kama ni muaminifu lakini kama sio muaminifu kuna uwezekano wa kutafutwa kupitia taalifa hizo japo wengi hawafikii hatua hiyo. Na hata ukiibiwa taalifa za malipo anayotoa mtu anaelipia na kuitumia baada ya kuibiwa zinaweza tumika kujua simu ipo kwa nani.

Ni hayo machache katika ukurasa huu, Endelea kuwa nasi na usisahau kwa simu za mikopo ni msaada mkubwa kwa watu katika kipindi hiki. Hazina usumbufu wa kukunjana mashati na kuaibisha wakati wa kukudai.

Leave a comment