Karibu the bestgalaxy na hapa katika makala tunaenda kuangalia SMS za kumsifia mpenzi wako. Hakuna raha kama kusifiwa na mtu unaempenda. Mtu ukisifiwa na unaempenda toka moyoni unaweza hisi Duniani upo juu na wathamani sana. Kiufupi maneno mazuri ya kusifu yakitoka kwa wapenzi au watu tunao wapenda huwa yanaupasua moyo kwa furaha na kufanya tuhisi kuwa tunathamani. Hivyo ukitaka kuugusa moyo wa mpenzi wako kwa kiasi hicho si vibaya ukatumia sms nzuri za mapenzi za kumsifia mpenzi wako. Hii inaweza kufanya awe na furaha, aione thamani yake na kujua umetambua thamani yake pia.
Kupitia ujumbe mfupi wa SMS, unaweza kumwambia mpenzi wako jinsi unavyomheshimu, kumjali, kumkumbuka na kwanini upo hivyo kwake. Unaweza fungua moyo wako kwake na kumwagia sifa zake zote nzuri.
Makala hii imekukusanyia ujumbe au sms ambazo unaweza kutumia kumsifia mpenzi wako mwanaume au mwanamke ili ajisikie vizuri na kujua jinsi unavyomthamini. Kama utahitaji unaweza ziangalia hapa sms chini
Zawadi za kumpa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
SMS za kumsifia mpenzi wako (mwanaume au mwanamke)
- Ninafuraha kwakua nina Bahati sana. Bahati ya kwanza ni kufikia siku ya Leo na bahati ya pili ni kuwa na wewe mpaka leo. Nitakupenda Milele mpenzi wangu, wewe ni mtu muhimu kwangu.
- Ivi ni nani alikufundisha Mapenzi? Yani hata kukuchiti siwezi, naona ushenzi. Nanenepa kwa Mahaba yako na chini ya shuka nakula mpaka mfupa, sitemi.
- Najua huwenda kunasiku unahisi umewahi niudhi na kuna pia siku unahisi unanifurahisha. Lakini ukweli ni kwamba nazifurahia siku zote nilizokua na ntazokua na wewe. Nakupenda sana furaha yangu.
- Hapo zamani nilikua naomba mungu nikutane na mwanaume jasiri, anaenipenda, anae nijali na kunithamini. Nashukuru mungu kwa kunileta karibu nawe. Mwanaume upo moyoni, unazunguka kwenye damu mpaka akilini. Nakupenda honey.
- Wanasema “mapenzi ni matamu” ni kweli, umenipa nikaamini. Wanasema “Raha ya mapenzi umpate anae kupenda na kuyajua” hata siwezi pinga maana Raha naiona tangu ulivyoungana na mimi. Nakupenda na sihitaji kutoka penzini.
- Mapenzi unayonipa yamenifanya nione maajabu. Siku hizi nikifumba macho sioni giza, nakuona wewe. Moyo unajawa na furaha, najikuta natabasamu kila nikikuwaza wewe. Yani naishi maisha ya furaha kwasababu nimekuchagua wewe.
- Kila siku nikikutazama nakuona mpya katika uzuri wako. Na unanivutia kiasi ambacho tukiwa karibu natamani kugusisha moyo wangu na wako. Nimeisha kuwa teja wa penzi lako.
- Nilikua natamani kupata na kumpenda mtu mwenyewe sifa nyingi nzuri. Nashukuru mungu kunikutanisha na wewe. Nimekupata sasa, nakupenda na napenda jinsi ulivyo.
- Nilipokua mdogo nilikua napenda sana kuangalia mwezi na nyota angani. Zilikua zinanivutia sana kila nikizitizama. Siku hizi napenda kuangalia macho yako. Ni mazuri zaidi sana.
- Lips tu ni tamu zaidi ya pipi, na vingine vitamu havielezeki, nitavitoa wapi kama si kwako? Huniishi hamu na wala wewe si bigG, hivyo sahau swala la mimi kuondoa moyo wangu kwako.
- Huwa napenda vile unavyo vaa, unajipatia wewe malaika. Ni msafi unaependeza. Unakua kama nyota inayong’aa angani ambayo mungu ameichukua amenipa.
- Ndoto yangu ya kuwa na mtu ninaempenda maishani, ilianza kutimia nilipokutana na wewe kipenzi changu. Kwasasa nipo pamoja na wewe, najiona naishi kwenye ndoto yangu, Nakupenda sana.
- Macho yangu yakikutana na yako, moyo wangu hulipuka kwa furaha. Wewe ni mzuri kama malaika ulieshushwa kwangu, namuomba mungu, usiote mbawa.
- Hakuna njia ya kuachana na mimi isio niumiza. Siwezi kukupoteza alafu nikwa na furaha au bila kuumia. Nimekuweka moyoni mpenzi, wewe ni muhimu kwangu . Nahisi nakupenda.
- Mambo mazuri yote nilianza kuyaona maishani nilipokupata wewe. Umekua ni mwanamke mzuri unaevutia mambo mazuri kama ulivyo wewe.
- Maua hufanya bustani ipendeze na kuvutia. Upendo wako wewe, hufanya nijione wa thamani kwenye hii Duniani. Nakupenda sana.
- Uwezo wako wa kunitambua na kuelewa ninachohitaji bila kusemwa, hufanya mahusiano yetu kuwa ya kipekee sana. Unanipenda sana, najua. Na Mimi nakupenda kuliko unanyojua. Nitaishi nikiwa nawe moyoni mpaka mwisho wa Dunia.
- Unajua kupenda malaika wangu. Penzi lako hufanya nione bahati kuwa na wewe. Sauti yako, hunibembeleza. Najihisi kuishi mbingu ya saba na upendo wako ndio umenileta.
Sms hizi zimewekwa hapa kwaajili ya watu wa Jinsi zote. Kama ni mwanaume unataka kumtumia mwanamke/mke unaempenda, unaweza pata sms inayofaa. Na hata ukiwa mwanamke pia unaweza pata sms kwaajili ya Mwanaume/mme. Wakati ukifurahia hayo, endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.
