SMS za mafumbo ya Mapenzi kwa umpendae

Kama umezoea kumtumia sms za kawaida za mapenzi mwenza wako ni jambo zuri lakini tambua kuwa kuna sms za mafumbo za mapenzi ambazo ni nzuri pia kumtumia mtu unaempenda. Sms za mafumbo ya mapenzi ni sms ambazo nyingi ujumbe au maana ya sms huwa inajificha kidogo. Sms hizi  zanafanya mpenzi wako ahusishe ubongo wake kidogo kutambua maana sahihi ya kilicho maanishwa katika ujumbe wa mapenzi anao usoma.

Ni SMS nzuri sana kwa mpenzi na hapa The bestgalaxy tumekuandalia jumbe au SMS za mapenzi zilizochangamana na sms chache za mafumbo unayoweza kutumia kwa mapenzi wako. Kikubwa ukumbuke kuchagua sms inayoendana na hali yenu.

Sms za mafumbo ya mapenzi

  • Sioni ajabu Nzi kufia kwenye kidonda maana hata mimi najiona naweza kubari iwe hivyo nikipambania ninapopapenda. Milele nataka niwe kwako maana ni mahali nimependa.
  • Natamani ujue kuwa wewe ndie umenifanya niijue Radha halisi ya tunda la upendo. Sikuwahi fikilia kuwa siijui mpaka uliponipatia. Staki kukupoteza mpenzi, nimeridhika kuwa nawe, nataka kuendelea kufurahia.
  • Nilikua kila nikisikia simulizi juu ya watu waliopendana mpaka wakaamua kuanza kuishi pamoja, nawaza “wanapendana kiasi gani mpaka wanafikia mawazo hayo?”. Kwasasa nimewaelewa maana hali yangu kwako ni kama yao.
  • Nimezama kwenye penzi lako na staki mtu yoyote wa kuniopoa. Sipatishida, napata Raha. Hata nikitapatapa ni penzi tu limejaa. Sehemu nyingi nimepita ili kwako nije kukaa.
  • Siku Jua likichomoza jioni na kuzama asubuhi huenda labla ndio siku naweza kuwa nimebadilika kwako mpenzi wangu. Napo inaweza kuwa siko sawa. Lakini kama sio hivyo milele utakua wa muhimu kwangu kama pumzi. Nakupenda kipenzi.
  • Hata ungekua ni wewe; fikilia umekutana na mtu maishani anakupa furaha na anajua kujali pia. Mbali na mambo hayo, Bado moyo wako unampenda na hautaki uondoke maishani pia. Hivyo ndivyo jinsi ulivyo kwangu kwangu, Nakupenda my dear.
  • Penzi lako hunifanya ni hisi nipo juu sana. Ni Mbali linanifikisha tena ni zaidi ya usawa wa milima. Sijiwezi, nimeisha chizika sasa, napenda linako nipeleka na nampenda sana anaenipeleka.
  • Ukiziba vizuri masikio kwa mikono yako utagundua kelele zote pembeni hupotea na utulivu tu ndio hubakia. Hivyo ndio penzi letu linaweza kuwa endapo maneno ya watu tutayapuuzia. Nakupenda sana my love.
  • Umekuja kwangu kipindi ambacho nipo kwenye giza nene lakini umekuwa mwanga unaoangaza kila pande. Sasa sijui kitu gani unahisi kitafanya nisikupende? Tambua moyo wangu wote upo kwako na si kipande. Naomba usiniumize.
  • Nimekupatia moyo wangu kama zawadi yako kwa mapenzi matamu unayonipa. Naomba ushike taratibu mpenzi usije ukaniumiza.
  • Wewe ni lile ua ambalo limeota pekee kwaajili ya moyo wangu. Moyoni mwangu unahisi furaha nikikuwaza, nikikusikia na hata kukuona wewe. Pokea salamu Toka kwenye moyo wangu, unakupenda sana.

Unahitaji sms nyingine? Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy. Sms hizi ni moja ya sms nyingi ndani ya The bestgalaxy. Unaweza pitia kurasa nyingine za the bestgalaxy ili kupata mengine zaidi.

Leave a comment