Hapa kwenye ukurasa huu tunaenda tena kuangalia za sms za mapenzi unazoweza tumia kwa mpenzi wako. SMS tunazozingatia hapa ni kama ilivyoelezwa kwenye kichwa cha makala hii, yani tunaenda kuangalia sms zile zinazoweza mfurahisha mpenzi. Sio kila sms tutazoangalia hapa zinaweza mfurahisha mapenzi wako lakini kupitia orodha ya sms za mapenzi tulizoweka hapa chini unaweza pata sms nzuri inayoweza kumfurahisha mpenzi wako.
Usimtumie sms bila kufikilia kama ataipenda kwa jinsi unavyo mjua mweza wako. Kiufupi unatakiwa kuchagua sms kulingana na hali ya mahusiano yenu au hali ya mpenzi wako wakati unamtumia.
Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>
Sms za kufanya mpenzi wako afurahi
- Asubuhi njema mpenzi wa moyo wangu! Kila siku ninapoanza na wewe, moyo wangu hujaa furaha na upendo siku nzima. Nakutakia siku yenye neema na mafanikio.
- Leo ni siku ya kipekee kwa sababu nakupenda zaidi ya jana. Na usiwaze kuhusu kesho maana uko moyoni mwangu milele na kesho ntakupenda zaidi ya leo.
- Ninapopitia picha zetu za pamoja, nakumbuka jinsi kila wakati tunavyopendana na kusaidiana. Kiukweli wewe ni nguzo yangu, na nakushukuru kwa kunifanya niwe na wewe maishani, Nakupenda sana.
- Nakupenda sana Mpenzi wangu. Unanifanya nihisi nipo kwenye bahari ya mapenzi ambayo kuzama kwenye maji ni Raha na kuibuka raha. Unajua kunisafisha nakuwa mweupe, stamani kwenda kwengine nikachafuke.
- Ningependa kushare nawe furaha yangu, maumivu yangu, na kila wakati wa maisha yangu. Kila ujumbe toka kwako hunijaza nguvu na matumaini. Nakupenda sana.
- Hakuna neno la kutosha kueleza jinsi unavyonifanya nijisikie. Kila wakati ninaiona picha yako mbele yangu, moyo wangu unagonga kwa furaha kiwaza kuhusu wewe. Nakupenda sana mpenzi wangu, usije niacha mwenyewe.
- Nashukuru kwa uwepo wako katika ulimwengu yangu. Umejaza moyo wangu furaha, upendo, na kufanya nitambue maana mapenzi ni nini. Kwangu maana ya mapenzi ni wewe. Nimeridhika kuwa nawe, Nakupenda.
- Unaponikumbatia, nahisi niko salama na nina amani. Hakuna mahali pengine napendelea kuwa zaidi ya mikononi mwako. Nakupenda na nipo tayari kula kiapo.
- Nimefurahi sana kuwa nawe katika kila hatua ninayoipiga maishani mwangu. Najua kwamba si kila changamoto tutayokutananayo maishani ni rahisi lakini siwezi yumba nikiwa na wewe kipenzi wangu.
- Nakupenda sana na napenda vile umejua kunipa ninachotaka na naridhika nikikipata. Nitataka nini tena wakati penzi lako tamu nimenikamata? penzi lako ni hadimu, mbali na wewe siwezi pata.
Ni hayo tu, tuliokuandalia hapa Kwenye ukurasa huu. Usiache kufuatilia The bestgalaxy ili kujifunza mambo mengine yanayoweza kuwa muhimu kwako.
Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook