Hapa tunaenda kuangalia viashiria au dalili za kuwa mpenzi wako anakupendea pesa. Kuna jinsi pesa inaumuhimu kwenye mahusiano ya mapenzi ya sasa na hii sio kwenye mahusiano, ni maisha kiujumla. Hata watu wa jinsia tofauti mukiamua kuwa pamoja tu kwa kushirikiana bila kuwa wapenzi bado kuna jinsi maisha yatahitaji pesa kutokana na mahitaji mulionayo kama binadamu wa dunia hii ya sasa. Hivyo pesa sio kitu kibaya au kitu cha ajambu kwenye mahusianio ya mapenzi. Lakini kitu hatari kwenye mahusiano ni kuwa kwenye mahusiano na mtu asiekupenda wewe ila anaigiza kukupenda ili apate au kufurahia pesa zako tu. Hii ni hatari maana baada ya muda au baada ya pesa kuyumba, mtu aliependa kweli anaweza anza kuumizwa.
Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>
Dalili za kuwa mpenzi wako anakupendea pesa tu
Kila nyuma ya jambo la upendo ni pesa
Mtu asiekupenda wewe lakini anapenda pesa zako anaweza kuwa anatumia upendo wa kuigiza kupata pesa. Unaweza tanguliza kitu kinachoonesha anakupenda lakini hapo hapo unagundua lengo la yote ni kupata pesa toka kwako. Anaweza kuwa mgomvi na hakupigii simu wala kukutafuta lakini siku akitulia na akikutafuta ni siku ambayo anashida au anahitaji pesa toka kwako.
Vitu vya kushangaza ambavyo hutokea ukimpenda mpenzi wako sana BONYEZA HAPA>>>
Usipo husisha pesa hakuzingatii kwa chochote
Pia mtu asiekupenda anaweza kuwa na tabia ya kukupuuza unaposema hauna pesa . Yani mahusiano yako na yeye yanaweza fikia wakati unaona kabisa unapotoa pesa, anakuonesha upendo lakini usipotoa anakasirika na kukupuuza kabisa kiasi ambacho upendo wake kwako unakua haupo. Kiufupi pesa ndio inakua kitu pekee kinachofanya akuzingatie na kukwambia anakupenda. Usipompatia anatafuta kila sababu ya kukasirika, kutokukutafuta na kukufanya ujione umemkosea sana.
Hatoi au kutumia pesa zake kwenye matatizo yako
Yani hata iwe unaumwa au umepata tazizo linalomuhitaji yeye aje kwa nauli au anunue kitu kawaajili yako bado atakuhusisha kwenye pesa atazotumia. Kiufupi anataka ulipie kila kitu anachokifanya kwaajili yako. Unaweza pata shida inayohitaji aje kwako au aende sehemu lakini akiambiwa anaweza kujibu “Sina nauli, nitumie”. Hawezi tumia pesa yake kwenye jambo lako hata iweje, atakuomba pesa tu.
Hajali kuhusu muelekeo wako au mahusiano yenu
Unaweza fanya maamuzi mabaya kuhusu pesa mbele yake na asikwambie kitu kuhusu maamuzi hayo. Hana wivu na wewe kwenye mahusiano unapoonekana na watu wengine, kikubwa kwake ni kumpa pesa tu. Mipango ya mbele ya pamoja kuhusu mahusiano huwa haileti na hata ukiileta haonekani kuona inamaana sana kwake. Anaweza kuwa na matumizi ya pesa mengi sana yasio husisha kujenga familia au maisha ya pamoja.
Pamoja na kuyaona mambo hayo yote kwa mwanaume au mwanaumke unaehisi anakupendea pesa inaweza kuwa haimaanishi kwa asilimia 100 yupo hivyo. Hivyo ni viashiria tu ambavyo ukiviona, itabidi uchanganye na mawazo yako kuchanganua kuwa mwanamke au mwanaume ulienae anakupendea pesa au upendo wake ni wakweli.