Kutengeneza nyimbo kwa kutumia simu inawezekana? Ndio, inawezekana na nyimbo unayotengeneza kwa kutumia simu inaweza kuwa na mafanikio makubwa tu kama nyimbo za Studio rasmi. Kipindi cha nyuma, ukiwa kama msanii wa Muziki ilikua ni lazima uhusishe vyumba vya Studio rasmi vinavyomilikiwa na maproduser ili kufanya mazoezi ya nyimbo na kurekodi nyimbo zako. Lakini kwa sasa, hakuna ulazima sana wa kwenda huko kama hauna uwezo. Unaweza tumia simu yako ya mkononi kufanya mazoezi ya kurekodi nyimbo zako na hata kurekodi kabisa ukiwa nyumbani tu.
Jinsi ya kutengeneza au kurekodi nyimbo kwa kutumia simu
Unaweza tengeneza au kurekodi nyimbo iliokamilika kwenye simu ila utatakiwa kuwa na app maalumu kwa kazi hiyo. App zipo nyingi na kati ya app hizo kuna app ngumu kutumia, pia kuna app rahisi kidogo zisizo hitaji mambo mengi kwenye kuzitumia. Moja ya app ambazo ni rahisi kutumia ni app iitwayo “Voloco”. Inapatikana katika Playstore kwa simu za Android na hata Appstore kwaajili ya watu wa iPhone au vifaa vya iOS kwa ujumla.
App ya Voloco inahusiana zaidi na kuweka Voco kwenye Beat. Unaweza ingiza Beat lako mwenyewe au ukadownload humo humo ndani Beat zilizotengenezwa na watu wengine. Ni ngumu kukuelezea kila kipengele cha app hii kwa maandishi ili uweze kuitumia ila tumejaribu kukuelezea hapa chini kwa msaada wa picha vitu vya muhimu kuvijua utakapo fungua app hii.

Kutengeneza nyimbo ni project na kwenye app hii kitu cha kwanza utakachotakiwa kukifanya ni kutengeneza au kufungua project mpya. Ukisha fungua project mpya unaweza weka Beat unalotaka kuliimbia kwenye project hiyo alafu ukaanza kurekodi sauti au voco zako. Uzuri ni kwamba Ina Autotune hivyo kunajinsi sauti au voco zako zinaboreshwa.
Unashauriwa kuvaa Earphone unaporekodi voco zako. Baada ya kumaliza kila kitu kwenye project hiyo, unaweza itunza project yako kwenye app hiyo.
Ukihitaji kuitoka kama audio za kawaida unaweza ingia kwenye project ulizo tunza alafu ukabonyeza vidoti vitatu vilivyo kwenye project yoyote unayoyahitaji alafu ukaugusa “Download” ili kuidownload nyimbo uliotengeneza iwe kwenye simu yako. Utakua na chaguo la kutunza iyo nyimbo kama Audio au video. Nyimbo yoko itakua tayari lkuisikiliza japo unaweza pia kuipitisha kwenye software nyingine ili kuiweka kwenye ubora zaidi au kuibadilisha kuwa mp3 kama utahitaji.