Moja ya siku au tarehe ambazo watu wanaweza ya ona zina umuhimu sana kuzijua kwenye maisha yao ni siku ya kuzaliwa. Na ni kweli zina umuhimu maana katika mambo mengi huwa watu wanahitajika kutaja siku au tarehe ya kuzaliwa. Mara nyingi hii inaweza kuwa ni kwaajili ya kudhibitisha umri maana mtu anaweza kujua umri wako kwa kujua siku uliozaliwa(tarehe,mwezi au mwaka). Umri wa mtu ni tofauti kati ya siku mtu aliozaliwa na siku aliopo.
Katika jamii zetu siku ya kuzaliwa imewekwa mbele sana kwa baadhi ya watu kiasi kwamba inakua inakumbukwa kila mwaka na kusherehekewa. Sio jambo la ajabu na sio jambo la lazima pia.
Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>
Kama unampenzi au rafiki anaejali siku yake ya kuzaliwa, unaweza mfanyia jambo lolote la furaha katika siku yake ya kuzaliwa na akafurahi. Na inasemekana hata ambao hawazisherehekei na kuzijali siku zao za kuzaliwa, wanajiskia vizuri sana wakifanyiwa jambo lolote la furaha kuhusu siku yao hiyo. Hivyo ukiwa na rafiki au mpenzi hata ambae hajali kuhusu siku yake ya kuzaliwa, unaweza mfurahisha kwa kuonesha unaijali siku yake.
Katika birthday au siku ya kuzaliwa ya mtu, unaweza fanya mambo mengi kumfurahisha ikiwemo kumpa zawadi au kumtumia ujumbe kwenye simu. Hapa chini tumeweka baadhi ya jumbe au sms za kumtumia mpenzi au rafiki katika siku ya kuzaliwa.
SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Sms au Ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa mpenzi na rafiki
- Mtu ambea ni mwanga wa maisha kwangu ni wewe. Napenda kila wakati ukumbuke kuwa furaha ya moyo wangu ni wewe. Nakutakia siku ya kuzaliwa yenye baraka tele.
- Happy birthday rafiki yangu. Nakutakia maisha marefu na yenye furaha. Baraka na mafanikio ziwe katika Maisha yako na kila jema lisiache kukufuata.
- Heri ya siku ya kuzaliwa rafiki yangu kipenzi. Natumai siku yako itakua nzuri na furaha. Napenda kukuona na furaha hivyo napenda kuona ukifurahia siku hii muhimu kipenzi.
- Mpenzi wangu, Kuzaliwa kwako ni siku muhimu kwangu. Maana huo ni wakati zawadi yangu nzuri ililetwa toka kwa mungu. Nakupenda sana zawadi yangu, pia nakutakia maisha marefu yenye afya njema na furaha.
- Happy birthday rafiki mpendwa! Nakutakia kila wakati kupata nguvu na msukumo wa kutimiza matamanio yako hapa Dunia. Maisha ni safari na nakutakia kila jema kwenye safari yako rafiki yangu.
- Ninafuraha sana Leo maana ni siku mbayo malaika wangu ulizaliwa ili uje kuangaza maisha yangu. Kuwa na wewe na Raha sikufichi. Happy birthday my queen.
- Nakupenda sana. Napenda jinsi unavyonifanyia katika Upendo na maisha kiujumla. Nafurahi kuwa na wewe. Tunapitia mengi ila daima nitakupenda wewe. Hicho ndio kitu natamani ujue katika siku hii, happy birthday mpenzi!
- Nakutakia siku njema ya kuzaliwa rafiki yangu. Wewe ni mtu ambaye anamaanisha mengi kwangu na ambaye ninathamini sana wepo wako. Uishi maisha marefu rafiki yangu.
- Kila siku ninapokuwa nawe ni zawadi kubwa. Siku ya kuzaliwa yako ni fursa kwangu ya kusherehekea upendo wetu. Heri ya siku ya kuzaliwa, mpenzi!
- Upendo wangu kwako hauwezi kuelezwa kwa maneno yakatosha. Lakini katika siku hii ya kuzaliwa nataka nijaribu tu kwa kumwambia Nakupenda sana na uishi maisha marefu kipenzi changu. Happy birthday!
- Ningekua na uwezo ningeiweka siku yako ya leo iwe ni siku ya kitaifa my love. Natamani Kila mtu ajue siku ya leo ndio siku mtu alieuweza mayo wangu na kunipa furaha maishani amezaliwa. Nakutakia siku njema na maisha marefu.
Sms hizi au jumbe hizi zina maneno mazuri ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki na hata mpenzi. Unaweza zitumia bure kwa mpenzi wako mwanaume au mwanamke au rafiki. Kikubwa uchague ipi ni sahihi kuitumia kwa upande wako.
Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook.
