Mkiwa kwenye mahusiano na mtu, inaweza kutokea mpenzi wako akawa na hasira kuhusu jambo flani au akaleta ukorofi tu. Kuna watu wanaweza kuwa na hali hiyo mara chache sana kiasi ambacho hatuwezi sema “Wana hasira sana” au ni “Wakorofi”.
Ukiachana na watu hao, kuna watu wengine hali ya kuwa na hasira au ukorofi ipo kwenye maisha yao kwa kiasi kikubwa. Watu Hawa wanaweza kuwa na hasira au ukorofi ambao hata wenyewe tu hawaupendi. Inaweza kuwa ngumu sana kuishi nao au kuwa nao kwenye mahusiano kama haujajua kuwa ni watu wenye hasira au ukorofi sana.
The bestgalaxy katika upande huu, tunakupa mwanga juu ya Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofi. Mambo ya yanaweza saidia pale mpenzi wako asie na hasira anapopata hasira au kukusaidia katika kuishi na mpenzi mwenye hasira na ukorofi sana.
Lakini kabla ya yote, fahamu kuwa hasira au ukorofi inaweza kuwa ni hali ya mwanamke au mwanaume kwenye mahusiano. Hali hii haina jinsia na inaweza kuwa tatizo kubwa zadi kiasi ambacho muhusika mwenyewe haipendi, kutokana na kumsukuma kufanya vitu ambavyo hakusudii.
Kutokana na hili unashauriwa ukiwa kwenye mahusiano ujue mambo ya fuatayo ili usipateshida kuhusu hasira au ukorofi toka kwa mtu unaempenda.
SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofi(Wanaume na Wanawake)
Onyesha hali ya kumsikiliza
Unapoona mpenzi wako ana hasira kutokana na jambo flani au ameibua ukorofi na anaongea na wewe, onyesha hali ya kumsikiliza. Usioneshe hali ya kumpuuza anachoongea maana anaweza ongeza hasira au ukorofi na kufikia hali mbaya. Jaribu kuonesha hali ya kuwa unasikiliza anasema nini wakati anaongea na wewe ili uweze kupunguza hasira zake. Muache apunguze kilichopo kifuani pake kwa kutoa maneno.
Usibishane
Hatakama atakua anaongea kitu kisicho cha kweli au cha ajabu, jaribu kujizuia usibishane. Unaweza mwambia au kujieleza pale anapokupa nafasi lakini kuwa makini sana mmapofika hali ya kuanza kubishana. Kubishana kunaweza ibua ugomvi mwingine ambao hata yeye hakukusudia. Watu wengi wenye hasira wakibishiwa hutaka kuja juu zaidi kiasi ambacho baadhi yao huingia kupigana kimwili.
Kutombishia kunaweza kuwa ni jambo gumu lakini uzuri wake ni kwamba mambo yote ambayo anaongea kwa msukumo wa hasira alafu sio ya kweli yanaweza kumjia kichwani akitulia na kuona makosa yake yote.
Vitu vya kushangaza ambavyo hutokea ukimpenda mpenzi wako sana BONYEZA HAPA>>>
Chagua wakati sahihi wa mazungumzo nae
Kama mpenzi wako kuna kitu ameongea vibaya, amekukosea au unahitaji kumwambia, tulia na utafute muda mzuri kwaajili ya maongezi yenu. Usijaribu kumwambia mpenzi wako mambo hayo wakati unaona yupo kwenye hali ya hasira au ukorofi. Wewe fanya kutafuta muda ambao unaona kabisa hana na hawezi kuibua hasira kirahisi. Mbane kwenye muda huo kwa utulivu sana huku ukichanganya maneno yanayoweza ugusa moyo wake kwa upendo kwenye maongezi hayo.
Watu wengine wenye hasira wakifanyiwa hivi hufikia mpaka hatua ya kuomba msamaha kabisa na kukili. Wengine wanaweza kuwa wabishi kidogo ila dawa inakuwa imewaingia. Na wengine wanaweza anza tabia ya kuchunga asira zao ili wasirudie makosa.
Maneno ya kumwambia mpenzi wako usiku BONYEZA HAPA>>>
Usiache kumuheshimu na kumuonesha upendo
Kama mpenzi wako mwanaume au mwanamke akiwa ana hasira na ukorofi lakini bado unaona mnapendanq, usiache kumuheshimu na kumuonesha. Kikubwa ni kumsoma tu tabia yake na kujua viwango vyake vya hasira kinafika wapi, anakua vipi na unatakiwa kufanya nini ili muwe na furaha. Upendo ni pamoja na kujuana pande zenu zote mbili, za furaha na hasira, hasa mukishaanza itana mume na mke.
Tafuta suluhisho na fanya mambo bila kukurupuka
Usije kukurupuka kufanya maamuzi pale unapoona wanaume au mwanamke wako ana hasira. Badala yake, tuliza kichwa na kufikilia nini ni suluhisho. Ukisha pata jibu kichwani, lifanyie kazi kwa utulivu ili kuweka mambo sawa. Kukurupuka kunaweza fanya na wewe ukafanya maamuzi mabaya ambayo baadae yanaweza kukujia kichwani na kugundua haukua sawa. Jitahidi usikasirike na kupandisha hasira pale mpenzi wako anapo waka. Tumia akili na usitumie hasira sana maana hasira zikikutana na hasira, hazizai kitu kizuri.
Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>
Mwisho; Hizi ni zama za kisasa na mambo ya ukatiri hayakubaliki karibu Duniani kote. Kama mpenzi wako wa kiume wa kike ana hasira au ukorofi unaomsukuma kukufanyia ukatiri, ni vema ukaachana nae au ukampeleka kwenye mamlaka husika hata kama tayari ni mume au mke wako.