Jinsi ya kucheza game la Call of Duty Mobile bila kudownload kwenye Simu

Call of Duty mobile ni moja ya zile games hupendwa na watu ambao hupendelea magame ya kupambania ufalme wa vita. Game hili ni game maalufu kutoka Activision na lilitengenezwa na TiMi Studio Group kwaajili ya simu.

Watu wanaolipenda gemu hili ulimwenguni ni wengi na baadhi yao huwa wanatamani kujua jinsi ya kulicheza kwenye simu bila kudownload. Hii ni kutokana na game hili kuwa kubwa au kuhitaji simu zenye uwezo kuliko simu zao. Hapa The bestgalaxy tunaweka wazi moja ya njia mtu anaweza cheza game hili bila kudownload. Kama unahitaji kujua hili, basi tuwe pamoja hapa chini.

Jinsi ya kucheza game la Call of duty mobile bila kudownload

Now.gg ni moja huduma za cloud gaming zinazokuwezesha mtu kucheza magame mtandaoni bila kudownload au kuyapakua. Mbali na magame, pia kua app nyingine unaweza tumia kupitia huduma hii bila kudownload kwenye simu yako. Huduma hii kwasasa ndani yake Ina app ya Aptoide ambayo ukifungua utakutana na magemu mengi ikiwemo Call of duty mobile na utaweza kulicheza bila kudownload.
Unataka kujaribu? Sawa, fuata hatua zifuatazo kucheza hili la Call of duty mobile ili kulipakua kwenye simu.

  • Unanginisha vpn katika saver ya USA kama upo nje ya USA.
  • Ingia google na utafute “Call of duty mobile now gg” alafu chagua matokeo ya juu kutoka Now.gg
  • Baada ya hapo utaletewa ukurasa unaoionesha app ya Aptoide, bonyeza kitufe kilichoandikwa “Play in browser” ilicho chini ya Aptoide katika ukurasa huo.
  • Baada ya hapo utapelekwa katika ukurasa wa Aptoide na utatakiwa kutumia sehemu ya kutafuta kulitafuta game la “call of duty mobile” (Yani utaandika “call of duty mobile” kwenye kisehemu cha kutafuta cha Aptoide.
  • Ukishalipata, lichague kisha utabonyeza “INSTALL” na kuacha kwa muda mpaka utakapoona batani ya “OPEN” kwenye game hilo.
  • Ikisha tokea batani ya “OPEN” utalibonyeza ili kulifungua gemu na kuanza taratibu nyingine za ndani ya gemu pamoja na kulicheza.

Mwisho, unapotaka kucheza bila matatizo, hakikisha unazingatia muunganiko wako wa mtandao/internet. Inatakiwa uwe na mtandao wenye kasi na usio yumba maana huduma za cloud gaming huwa zinategemea internet zaidi.

Leave a comment