Kwanini haufanikiwi kimaisha? Sababu hizi hapa

Kila mtu unaweza kumsikia akiongelea kuhusu mafanikio lakini unapaswa kujua kuwa watu hawana maana sawa ya mafanikio. Hata ukiwauliza “Mafanikio ya kimaisha ni nini kwako?” watu huwaza vitu ambavyo hutegemeana na jinsi mafanikio yana maana gani kwao.

Kiufupi Mafanikio ya kimaisha tunaweza sema ni hali au matokeo ya kuweza kufikia lengo au malengo fulani maishani. Tunaweza pia kusema mafanikio ni kufikia au kuzidi matarajio, malengo, au viwango fulani vya utendaji katika maeneo mbalimbali ya maisha kama vile kazi, elimu, biashara, mahusiano au maendeleo binafsi.

Watu hukutana na changamoto nyingi katika kuyakimbiza mafanikio ya kimaisha. Hapa The bestgalaxy tumeisha zungumzia kuhusu mambo muhimu ili kufanikiwa pamoja na changamoto nyingi njiani. Katika ukurasa huu tunaenda kuangalia upande mwingine ambao ni mambo yanayoweza fanya mtu asifanikiwe.

Mambo yanayoweza fanya usifanikiwe

Kutojua mafanikio kwako ni nini na yanapatikana upande gani

Kama tulivyoeleza hapo juu, Kila mtu kuna jinsi ambayo mafanikio yanaonekana kwake. Sasa unapaswa kwanza kujiuliza wewe unahisi mafanikio ni nini kwako. Ni elimu ambayo itakupatia kazi? Ni biashara ambayo itafanya vizuri mpaka itabadili maisha yako? Usiwe na vitu vingi kichwani, fahamu mafanikio unayoyataka hapa Duniani na fikilia utayapata upande gani.


Kuna mtu aliulizwa “Unata kufanikiwa kivipi?” Akajibu “Kama msanii diamond… Yani nyumba kali, gari Kali na watoto wazuri kama wote… Alafu navimba kama kwenye nyimbo yake moja hivi. Yani nikisimama watu wote shangwe” akaulizwa “kwani wewe ni msanii?” Akajibu “hapana” akaulizwa tena “Unaimba mziki?” Akajibu “ah amna hata siwezi. Na sijikufanya kabisa hizo mambo”
Huyu jamaa kitu anachotamani maishani au mafanikio anayoyatamani ni ya mtu ambae ni msanii. Sio kitu baya, lakini yanaweza timia vipi ikiwa haupo kwenye upande ambao yanapatikana?. Hapa ukizidi kutamani, utapata msongo wa mawazo.


Ni vema kujua mafanikio kwako ni nini na yanapatikana upande gani. Kama mafanikio yako unahisi yatapatikana kwenye biashara, kuwa upande wa biashara, bana upande huo ata uwe msaidizi tu. Tambua kitu unachokihitaji alafu usicheze nacho mbali, pambana kukisogelea.

kubadirisha au kuyakatia tamaa malengo yako

Kujiweka malengo ni hatua nzuri ya kuanza safari ya mafanikio. Lakini mara nyingi malengo huwa na changamoto zake katika kuyatimiza. Unaweza kukumbana na vitu vingi sana katika safari ya kuyatimiza. Lakini unatakiwa kuwa makini sana linapokuja wazo la kubadirisha au kuyakatia tamaa malengo uliojiwekea. kubadirisha au kuyakatia tamaa malengo uliojiwekea inaweza kuwa ndio mwanzo wa kupotea na kushindwa kufikia mafanikio unayoyahitaji. Ni vema kupambana na kuwa msimamo wa kutimiza malengo yako ili uweze pata mafanikio unayoyahitaji.

Kukosa utayari wa kuwa unaetakiwa kuwa au kuacha vinavyo rudisha nyuma.

Inasemekana kwamba kunawatu huwa wana mipango mikubwa kwenye vichwa vyao, tena inayoweza kuwatoa waliopo. Watu hawa wanajua kila kitu kinachohitajika kufikia pale wanapotamani kuwa kimaisha. Sio hayo tu, wanajua mpaka kinachowafanya wasifikie mafanikio lakini hawapotayari kubadirika au kuacha vinavyo zuia kufanikiwa.


Ukitaka kufanikiwa mara nyingi inabidi uwe ni mtu unaweza badirika, kujifunza vitu vipya na kuwa na utayari wa kuacha mambo unayoona kabisa yanakuzuia. Usipo chukua hatua kwenye kufanya mambo hayo, unaweza jikuta unayaona mafanikio unayoyataka mbele yako lakini huyafikii.

Woga wa kushindwa au kuwa tofauti

Kama mafanikio unayoyataka yanahitaji ufanye kitu ili kuyafikia lakini unahisi woga basi tambua kwamba baada ya miaka kadhaa unaweza jutia kuogopa kwako. Wengi tukitaka kufanya bishara au vitu vya maandeleo vitakavyo boresha maisha yetu, huwa tunaogopa kudondoka au kuogopa ndugu, majirani, marafiki na watu wengine waliotuzunguka. Lakini jambo hili watu hujutia baada ya kutambua kuwa walitaka kufanya vitu vizuri ila walishindwa kutokana na kuogopa au kuwawaza watu ambao hawajaungana na maisha yao. Kama umefuatilia simulizi ya utamu wa jumla unaweza nielewa zaidi hapa.


Njia rahisi ya kuondoa woga wakufanya kitu unachotaka kukifanya ni kuingia wenye mazingira yanayohusiana na unachokitaka kukifanya. Kama unataka kuwa mfanya biashara wa samaki, Tafuta marafiki wanaojihusisha na mambo hayo, au naenda kwenye mazingira ya hayo mambo.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Leave a comment