Linapokuja swala la simu kuingia maji, inaweza kuwa ni moja ya vitu watu hawapendi litoke hata kidogo. Ila kutokana na kazi tunazofanya au mazingira ambayo mtu upo, jambo hili linaweza tokea. Na simu ikiingia maji wote tunajua kinachoweza kutokea ni kuharibika kwa simu pamoja na kupoteza vitu vya muhimu vilivyo kwenye simu.
Ili kuzuia jambo hilo lisitoke, Makampuni ya simu huwa yanatoa simu ambozo zinasifa ya kuzuia maji kuingia kwenye simu. Simu hizi mara nyingi hutangazwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance”. Na watu wengi wakiwa wanataka kununua simu wakiona imetajwa kuwa ni “Waterproof” au “Water resistance” huwa wanajua ni simu zisizo ingia maji.
Kitu muhimu kujua hapa ni kwamba kuna utofauti kati ya Simu zinazosemwa kuwa ni “Waterproof” na simu zinazosemwa kuwa ni “Water resistance”. Na hapa chini The bestgalaxy tunaenda kukufungua kitu muhimu juu ya utofauti huo.
Tofauti kati ya Simu za Waterproof na simu za Water resistance
Simu za waterproof na simu za water resistance zina tofauti katika jinsi zinavyozuia maji. Simu za waterproof zina uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani yake kabisa. Lakini simu za water resistance zinakua na kiwango cha kuzuia maji kwa kiasi flani au namna flani.
Kiufupi simu hadi imeitwa “Waterproof” ni haiwezi ruhusu maji kupenya ndani kabisa. Lakini simu ikiitwa “Water resistance” huwa inaweza kuzuia maji lakini inategemeana na wingi wa maji, joto la maji, aina ya maji, muda iliokaa ndani ya maji au kina cha maji. Na unapotumia simu za Water resistance haushauliwi kuziweka kwenye maji makusudi maana zinaweza kuingia maji. Kuzuia maji kwake kuna kunailinda simu yako isiharibike pale unapo idondosha kwa bahati mbaya kwenye maji au sababu nyingine zisizo za makusudi.
Inasemekana kwamba simu nyingi huwa ni Water resistance na sio Waterproof. Na Kuna Makampuni yanaweza kuziita simu zao Waterproof kwa lengo la kibiashara lakini zikawa zinastahili kuitwa Water resistance na sio Waterproof. Kutokana na jambo hili, haushauriwi kujiamini sana kiasi cha kuiweka weka kwenye maji simu yako hovyo baada ya kuambiwa ni Waterproof.
Simu za Waterproof na Water resistance huwa zinawekwa vimipira na gundi kwenye nafasi ambazo maji yanaweza kupita. Mara nyingi simu za muundo huu huwa ni ngumu kuzifungua zinapotaka kurekebishwa kifundi na pia zikifunguliwa tu, huwa zinapoteza uwezo wake wa kuzuia maji. Mbali na jambo hil, simu hizi zinaweza poteza uwezo wa kuzuia maji baada ya kudondoshwa chini na kujigonga au kutumia kwa muda mrefu.
Ingress protection ratings (IP ratings) ni kipimo cha uwezekano wa kifaa cha kielectric ikiwemo simu zuia maji(vimiminika) na vumbi. Mfano wa IP rating ni “IP68” na imetajwa kuwa samsung galaxy s24 ultra inauwezekano huo. Namba ya kushoto “6” ni uwezekano wa kuzuia vumbi alafu namba “8” ni uwezekano wa kuzuia maji. Simu hii inafahamika kama ni “Waterproof” kutokana na uwezekano huo japo bado haushauriwi kujiachia nayo kwenye maji au vimiminika. Mwisho ningependa ufahamu kuwa Samsung Galaxy S24 ultra ni simu ya kwanza toka Samsung iliojikita kwenye Ai (akili bandia).