Ni ngumu kusema moja kwa moja mwanaume anaefaa kuwa mume anatakiwa awe vipi. Na ni ngumu kwasababu katika maisha, hii dhana ya “Mwanaume anaefaa kuwa mume” inafanya watu wazingatie kuangalia sifa za mwanaume. Sifa hizi huwa zinatofautiana kutokana na tamaduni, imani, na mtazamo wa mtu binafsi.
Lakini, kuna sifa muhimu ambazo mara nyingi akiwanazo mwanaume huwa zinaweza kuwa ni viashilia vya kuwa anaweza kuwa mume bora kwako katika ndoa. Baadhi ya sifa hizo tumezizungumzia hapa chini. Kama utakua ni mwanamke ambae unahitaji kujua kuhusu hili ni vema ukachukua muda wako kusoma. Kama wewe ni mwanamke hii inaweza kukusaidia katika safari yako ya kupata mume sahihi (husband material).
Sifa 5 za mwanaume anaefaa kuwa mume
Muaminifu
Mwanaume muaminifu kwako ni mwanaume ambae anaweza kuwa bora kuwa mume. Ni ngumu kuwa na mume ambae sio muaminifu katika ndoa maana kunaweza fanya uwe na wasi wasi ambao unaweza pelekea kukosa amani katika ndoa. Unaweza jikuta unamchunga kila mahari na bado unakutana na mambo mengi ya kukuumiza.
Mwanaume mwaminifu anaweza akakufanya usiwe na wasi wasi nae sana katika ndoa na hii inafanya uwe na amani nae na sio kumtilia mashaka kila mara. Na hata akiteleza unaona kabisa ni bahati mbaya.
Mvumilivu na mwepesi wa kusamehe
Mwanaume mwenye uwezo wa kuvumilia ni mwanaume anaefaa kuwa mume. Ndoa inamambo mengi sana ambayo yanahitaji uvumilivu na kuyasamehe. Kuna muda mwanamke unaweza kosea katika ndoa na kama mume wako sio mvumilivu au mwepesi wa kusamehe, inaweza kuwa ni hatari. Tukiwa kama binadamu, ni lazima tukosee katika mambo mbalimbali katika maisha. Hivyo ni vema kuwa na mtu anaeweza kuvumilia au kutusamehe. Na unatakiwa kujua kuwa uvumilivu sio muhimu kwenye kukoseana tu, hata kwenye kupambana na maisha tu bado unahitajika.
Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>
Anakufurahisha na unampenda
Unaweza kuwa na mwanaume ambae anahitaji kuwa mme wako au unahitaji kuwa mume wake lakini unapaswa kujiuliza “Anakufurahusha na unampenda?”. Usije ukajitupa kwa mtu ambae hakufurahishi wala humpendi kwa dhati ili tu uitwe mke wake na wewe umuite mume. Ni vema ukaangalia kwanza kama mnafurahia ukaribu wenu kabla hamjaitwa mume au mke. Angalia pia kama mnapendana kweli kabla hamjaingia kwenye ndoa.
Anaejali kuhusu wewe na hali ya maisha yake
Unajiuliza anaejali kuhusu wewe na maisha yake kivipi? Sawa, hii tunaweza sema ni jambo muhumu sana. Mwanaume anaekujali wewe ni mwanaume Bora kuitwa mume. Kujali kunaweza kusanya mambo kama kukusikiliza, kuwa karibu na wewe, kukusaidia kwenye baadhi ya mambo na kuonesha uhitaji wa uwepo wako kwenye maisha yake.
Akiwa anajali kuhusu hali ya maisha yake pia ni jambo zuri maana ukimuita mume utakua upo ndani ya maisha yake. Kujali kuhusu maisha yake au hali ya Maisha yake kunaweza jumuisha kuwa na ndoto anazozipambania, kujua alipo na anataka kwenda wapi kimaisha, kutatua changamoto za maisha yake na kuwa dereva mzuri wa maisha yake.

Anaweza kuwa rafiki yako
Hakuna furaha kama kuwa na mume ambae ni kama rafiki yako. Yani mnaishi kwa amani, manajuana tabia na mapungufu yenu, mnatunziana siri na mnashirikiana kwenye mambo mbalimbali kama marafiki mulio shibana na sio watu mnaoogopana sana au kuwa kama maadui Kila muda.
Ukitaka kupata mume kama huyu ni vema ukajiuliza mwanaume unaetaka awe mume anaweza kuwa rafiki yako au laa.
Mwisho; Ni hayo tu tulioyazungunzia hapa lakini kunavitu vingi zaidi ya hivyo unaweza angalia kupata mwanaume sahihi kuitwa mume. Ni vema kufahamu pia, baadhi ya wanaume hubadili tabia wanapoingia kwenye kuitwa “mume” hivyo nivema ukachagua unaempenda ili isiwe rahisi kuvumilia na kutojutia.
Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook